#COVID19 Mnaotishia watu wanaotaka kupata Chanjo ya UVIKO-19 mna shida vichwani mwenu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
Kabla ya kuchanja rasmi leo Chanjo yangu ya UVIKO-19 aina ya J&J nilijaribu kuwataarifu watu kadhaa, ila cha kushangaza wote waliishia kunitishia huku wengine waitaka ninunue kile cheti cha uthibitisho wa kupata chanjo kwa Tsh 30,000/= ila nisichanje kabisa, ila nikawakatalia na kuamua kuchanja na kupata cheti.

1. Nilitishwa nikichanja nitakufa hapo hapo cha kushangaza hadi muda huu napumua.

2. Nilitishwa nikichanja nitasikia kizunguzungu ila nashangaa hadi sasa sizunguki na kichwa changu.

3. Nilitishwa nikichanja nitasikia mno maumivu ya mwili ila hadi sasa sisikii maumivu yoyote zaidi tu ya hawa mbu wanaokesha nami usiku kucha.

4. Nilitishwa nikichanja tu nitaanza kujikuta naokota makopo (nadata mazima) ila hadi muda huu medulla oblangata yangu iko vyedi (vyema) kabisa.

5. Nilitishwa nikichanja tu nitakosa hamu ya kula na nashangaa mpaka muda huu nimeshafuta sahani tatu za ugali wa ulezi, mtama na kichuri na nimeomba nipikiwe mwingine.

6. Nilitishwa nikichanja uono wangu utakuwa hafifu (sitoona vizuri) ila ninaona vizuri kabisa

7. Nilitishwa nikichanja tu basi hapo hapo nyara baioloji yangu ya kufyatua watoto itazima mazima ila nikashangaa dakika 30 baada ya kuchanja imepitia majaribio na iko vizuri kabisa.

Asante sana Daktari uliyenichanja Chanjo ya UVIKO-19 leo na wale Majuha wote mnaotisha watu kuwa wasichanje kwakuwa itawaathiri acheni mara moja kufanya hivyo, ila wimbi la UVIKO-19 likija na kupukutisha ndugu zako usianze kusema kuwa umerogwa au una nuksi au Mwenyezi Mungu hakupendi.
 
Coronavirus ikikupata balaa yaani kichwa chote kinauma usingizi hupati hatari sana. Lakini kuchanja sichanji ngooooo🤣
 
hii kitu inanishangaza sana
 
Ni sababu ipi imekufanya upate chanjo ya UVICO 19 jana/Leo..?

Siku zote ulikuwa wapi, au ulikuwa unafanya research kuhusu usalama wa chanjo au tayari umeshapewa fungu lako ili ufanye campaign..?

Anyway....

Chanja kwa faida yako.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Wewe ngozi nyeusi unatazama usawa wa pua utajua mitego ya mzungu? acha kujidanganya mzee.
 
Kabla ya kuchanja rasmi leo Chanjo yangu ya UVIKO-19 aina ya J&J nilijaribu kuwataarifu watu kadhaa, ila cha kushangaza wote waliishia kunitishia huku wengine waitaka ninunue kile cheti cha uthibitisho wa kupata chanjo kwa Tsh 30,000/= ila nisichanje kabisa, ila nikawakatalia na kuamua kuchanja na kupata cheti.

1. Nilitishwa nikichanja nitakufa hapo hapo cha kushangaza hadi muda huu napumua.

2. Nilitishwa nikichanja nitasikia kizunguzungu ila nashangaa hadi sasa sizunguki na kichwa changu.

3. Nilitishwa nikichanja nitasikia mno maumivu ya mwili ila hadi sasa sisikii maumivu yoyote zaidi tu ya hawa mbu wanaokesha nami usiku kucha.

4. Nilitishwa nikichanja tu nitaanza kujikuta naokota makopo (nadata mazima) ila hadi muda huu medulla oblangata yangu iko vyedi (vyema) kabisa.

5. Nilitishwa nikichanja tu nitakosa hamu ya kula na nashangaa mpaka muda huu nimeshafuta sahani tatu za ugali wa ulezi, mtama na kichuri na nimeomba nipikiwe mwingine.

6. Nilitishwa nikichanja uono wangu utakuwa hafifu (sitoona vizuri) ila ninaona vizuri kabisa

7. Nilitishwa nikichanja tu basi hapo hapo nyara baioloji yangu ya kufyatua watoto itazima mazima ila nikashangaa dakika 30 baada ya kuchanja imepitia majaribio na iko vizuri kabisa.

Asante sana Daktari uliyenichanja Chanjo ya UVIKO-19 leo na wale Majuha wote mnaotisha watu kuwa wasichanje kwakuwa itawaathiri acheni mara moja kufanya hivyo, ila wimbi la UVIKO-19 likija na kupukutisha ndugu zako usianze kusema kuwa umerogwa au una nuksi au Mwenyezi Mungu hakupendi.
nenda mikumi ukapige story na fisi!!,kwani ukichanja wanyama wakali wanakuona kama mshikaji wao kimtindo!!
 
Ni uongo mbn Kuna jamaa yangu alipata chanjo ya Corona na anajitolea Damu Kila mwaka kuanzia mwaka jana ,na mwaka huu kachangia Damu.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Acheni propaganda uchwara.

Mimi nimepoteza ndugu zangu waliochanja na Damu ikawa inaganda.

Chanjo zilikuwa mara mbili, fake na lenyewe, msihadae watu.
 
Back
Top Bottom