#COVID19 Chanjo milioni 40 za Covid-19 kutupwa Afrika Mashariki muda wake ukikaribia kwisha, Tanzania yasema imevuka 50%

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,825
Nchi za Afrika Mashariki zinakabiliwa na hifadhi kubwa ya chanjo za Covid-19 zinazokaribia kuisha muda wake ambazo ilizinunua kwa nguvu kubwa kama yalivyofanya mataifa ya Ulaya kwa ajili ya raia wake.

Matokeo yake chanjo milioni 40 zinaweza kugeuka taka baada ya kubakiza miezi michache kuharibika huku mapambano ya kupambana na ugonjwa huo yakipungua nguvu kila kukicha kutokana na wananchi kutoufatilia tena.

Uganda imebakisha miezi minne chanjo zake milioni 13.4 kuharibika huku Kenya ikijiandaa kutupa chanjo milioni moja zinazoharibika mwezi ujao.

Tanzania imesema imevuka asilimia 50 ya chanjo hizo huku Dr. Derrick Sim, meneja wa Covax akisifia mpango enedelevu wa kuchanja miezi ya karibuni kama sababu iliyofanya wafanikiwe kufikia hatua hiyo.
 
 Waliochanjwa chanjo ya corona na ambao hawajachanjwa hakuna tofauti halafu pia corona ni ugonjwa wa kutengeneza kwa hiyo hata takwimu za korona zinatakiwa ziwe kutengeza kuwafurahisha wazungu lakini ukweli unajulikana.
 
Hahahah nasikia Zanzibar wanaenda kitaa kwa kitaa na kulazimisha na kulazimisha kuchanja. Hakika ni uuaji mkubwa sana.
 
 Waliochanjwa chanjo ya corona na ambao hawajachanjwa hakuna tofauti halafu pia corona ni ugonjwa wa kutengeneza kwa hiyo hata takwimu za korona zinatakiwa ziwe kutengeza kuwafurahisha wazungu lakini ukweli unajulikana.
Walio tengeneza wanasema ukikaidi utapigwa tu


Ipo siku wataleta CORONA MODIFIED VIRUS CMVD19
Hakika tutatafutana
 
Tanzania chanjo zetu zimebaki ngapi?

Naona mmewasengenya tu majirani.
 
Baadhi ya wanasiasa walihongwa pesa na makampuni ya kutoa chanjo ili waseme magufuli aliuwawa na corona. Angalia royal tour mwanzo mpaka mwisho utagundua mambo mengi ni ya mchongo.
 
Back
Top Bottom