Kwa huu mgao wa umeme tutalipaje kodi za Serikali kwa wafanyabiashara tunaotegemea umeme kwa ajili ya kuzalisha?

Isengelo

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
476
746
Habari wana jamvi,

Kwa hii hali ya kukosekana kwa umeme, hakuna shughuli yoyote ya uzalishaji unao endelea kwenye biashara zinazotegemea umeme, hiì itasababisha ugumu katika ulipaji wa kodi.

Je, selikali inalifahamu hili? Na inachukua hatua zipi ili kodi iendelee kukusanywa?

Kwa mfano sehemu nilipo umeme unawaka mara mbili kwa wiki.

Naiomba Serikali iliangalie suala hili kwa umakini vinginevyo uchumi wa nchi unakwenda kudorora na umasikini utatamalaki kwa raia
 
Jamaa unachekesha. Kodi nyingi inapatikana kwenye imported goods na sio zinazozalishwa ndani by comparison.

Alafu unatakiwa ujue anaekusanya kodi sio anaedili na umeme.
 
Jamaa unachekesha. Kodi nyingi inapatikana kwenye imported goods na sio zinazozalishwa ndani by comparison.

Alafu unatakiwa ujue anaekusanya kodi sio anaedili na umeme.
Acha ujinga, nini jukumu la serikali kwa wananchi wake.

Kama import duties inatosha kwa nini serikali iendelee kukusanya domestic taxes
 
Habari wana jamvi
Kwa hii hali ya kukosekana kwa umeme, hakuna shughuli yoyote ya uzalishaji unao endelea kwenye biashara zinazotegemea umeme, hiì itasababisha ugumu katika ulipaji wa kodi.

Je selikali inalifahamu hili? Na inachukua hatua zipi ili kodi iendelee kukusanywa?

Kwa mfano sehemu nilipo umeme unawaka mara mbili kwa wiki.

Naiomba serikali iliangalie suala hili kwa umakini vinginevyo uchumi wa nchi unakwenda kudorora na umasikini utatamalaki kwa raia
Napata wasiwasi 2025, CCM watajikuta hata baada ya kuiba Kura bado hazitatosha kupata Urais
 
leta sehemu yoyote iliondikwa kuwa jukumu la serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata umeme?
Aise na wasiwasi na elimu yako, hata kama unayo basi ni ya kukariri.

Hujui kama serikali inao wajibu wa kutengeneza mazingira wezeshi ili wananchi wake waweze kushiriki shughuli za ki uchumi, ikiwemo upatikanaji wa nishati ya uhakika kama; umeme, gas mafuta n.k


Alafu nimegundua kwenye Fiscal and Monetary Policy wewe ni mweupe,sijui nani alikuajiri kuwa mkusanya ushuru
 
🤣🤣🤣🤣🤣 vijana mko na tabu sana tafakari mimi nina ofisi ambayo kuzalisha pesa inategemea umeme pekee,umeme unakosekana kwa wastani wa siku 15 kwa mwezi,maana yake nimefanya kazi kwa siku 15 pekee,why serikali nayo isichukue kodi nusu maana ndio inayotakiwa unipe nisharti ya uhakika ili niweze kulipa kodi na kutimiza majukumu yangu mengine 👐👐👐 anyway kwa wale mnahitaji kufungiwa mifumo ya solar ,power backup,betri imara za solar na solar kwa bei nafuu , nicherk niko Mwanza
 
Back
Top Bottom