Tozo haijafutwa imehamishiwa kwenye majengo kupitia manunuzi ya umeme

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,869
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo imetangaza kuanza kwa viwango vipya vya ulipaji wa kodi ya majengo, ambao utawalazimu wamiliki nchini kulipa kiwango cha juu zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Mabadiliko mapya ni ya ukusanyaji wa kodi ya majengo, ambayo hulipwa kupitia ununuzi wa tokeni za umeme.

Hii inafuatia marekebisho ya Sheria ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (Ukadiriaji) (SURA 289) yaliyofanywa kupitia Sheria ya Fedha ya 2023.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo Julai 25, 2023; TRA imeeleza kuwa viwango hivyo kwa mwaka vitakuwa ni Sh18,000 kwa kila jengo la kawaida ndani ya kiwanja, kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kile cha Sh12,000 kilichokuwa kikitozwa hapo awali.

Kwa upande mwingine, mmiliki wa jengo la ghorofa moja katika miji, halmashauri za manispaa na majiji, yeye atatozwa Sh90, 0000 kutoka Sh60, 000 kwa mwaka.

Hata hivyo, kwa upande wa halmashauri za wilaya, nyumba za ghorofa, bila kujali idadi ya sakafu zitatozwa Sh90, 000.

Kwa mujibu wa TRA kila mnunuzi wa umeme atakatwa Sh1, 500 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na Sh7, 500 kwa mwezi kwa jengo la ghorofa.

Serikali ilianza utekelezaji wa malipo haya ya kodi ya majengo kupitia manunuzi ya tokeni za umeme toka Julai 2021.

FB_IMG_1690509310757.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 2701065

Sent using Jamii Forums mobile app
Tozo ya miamala hasa Kwa mtumaji imefutwa na hii ya kutolea imepungua Sana eg unaweza toa zaidi ya 800k Kwa atc Kwa chini ya 4,000 tofauti na Mwanzo.

Kwenye simu unatoa zaidi ya 100k Kwa chini ya elfu 3 hapo Mwanzo ilikuwa zaidi..

Afadhari ya kulipa umeme ni 15,000 tu Kwa mwaka kuliko ya miamala ilikuwa inauma yaani unajikuta ndani ya mwezi umelipa zaidi ya 15,000
 
Back
Top Bottom