Idimulwa
Platinum Member
- May 27, 2011
- 5,110
- 2,698
tanga kwetu,ccm wanahamasisha watu wao kupitia mabalozi wa nyumba 10 na kuwaandikisha usiku kama ilivyotokea Dodoma
Last edited by a moderator:
Wala hujakosea, si ulianza> sasa nguruwe nani hapo?
Unaonesha unawajuwa sana nguruwe, mnafuga wa biashara au kitoweo?
Kwi kwi kwi teh teh teh.
Hivi hakuna uwezekano wa kwenda mahakamani kusimamisha huu uhuni unaofanywa na hii tume kwa kunyima watu fursa ya kujiandikisha?
Ndo maana mdomo wao na wako sawa sawa
Audhu bi Llahi min dhalika.
Hasbunna Allahu wa nee'ma L'wakil.
Nnajuwa muono wako ni finyu na nnayoyaandika ni zaidi kimo chako lazima ufikirie hivyo. Muono wako ukikuwa, kama utakuwa, utakuja kunielewa tu.
Yaani FF mumekubali awazidi akili?!Au ni wageni JF?Tujadilini mada
Nilitaka tujiridhishe ujinga wake huyu bibi kwa kumchokonoa
Wakuu naombeni radhi kwa kuchafua mada..
_________
Wewe unachobisha ni nini haswa? Tanzania hii imejaa wahamiaji haramu kila sehemu. Sasa wewe mtu mpaka mashine inamkataa unafanya maskhara?
Sasa ndiyo na mashine ziweze kuwatambua wahamiaji haram?kama ni hivyo basi watanzania tumefika mbali kuwazidi hata watengenezaji wa mashine wenyewe.
Wewe wasema. Ni wajibu na haki yangu kuhakikisha nashiriki uchaguzi ili nichague viongozi BORA wasio na mawaa. Hata hivyo siasa ni uwanja mpana ulio wazi kwa mchezaji yeyote. Mfano kwa upande wa ubunge unatakiwa ujue kusoma na kuandika ima kiswahili au kiingereza.Pole sana nakuhurumia unavyoteseka kujenga daraja kwa ajili ya wanasiasa kushika madaraka na kukuibia rasilimali zako.
Wewe wasema. Ni wajibu na haki yangu kuhakikisha nashiriki uchaguzi ili nichague viongozi BORA wasio na mawaa. Hata hivyo siasa ni uwanja mpana ulio wazi kwa mchezaji yeyote. Mfano kwa upande wa ubunge unatakiwa ujue kusoma na kuandika ima kiswahili au kiingereza.
Muda huu nipo kituoni nikisubiri kuandikishwa kwenye BVR. Hili ni jaribio langu la nne. Uandikishaji ulianza tarehe 09/06/2015 na siku ya kwanza nilienda kituoni nikapewa na 56 mashine iliandikisha watu 42 tu, tar 10/06 /2015 mashine iliandikisha watu 79, nikiwahi kituoni watu walikataa kututambua sisi tuliobaki Jana yake.
Tar 11/06 /2015 niliamka saa 8 usiku na kuwahi kituoni nikapewa na 64. Mashine iliandikisha watu 40 hadi saa 7 ikazima sikuweza kuandikishwa.
Leo nimefika kituoni saa 9 alfajiri na nimepewa na 86. Sijui kama leo nitaandikishwa. Nipo kituo cha Nyanza kata ya Mkolani wilaya ya Nyamagana.
Mtaa wetu una watu si chini ya 1500 wenye sifa za kuandikishwa lakini tija na ufanisi wa kuandikisha ni duni. Mwamko wa watu kujiandikisha upo juu na wamejitokeza kwa wingi lakini vitendea kazi na watenda kazi hakuna. Lengo la serikali ni nini?
Mkuu MANI ccm wana agenda ya kutaka uchaguzi uahirishwe lakini hawaisemi kwa uwazi hii.. Kinachofanyika sasa ni ku-frustrate zoezi zima la uandikishaji wa watu kwenye daftari kwa mashine za bvr kutoa muda mfupi kuandikisha wananchi wachache..
Upinzani ukilalamika na kwenda mahakamani maana yake watakuwa wamecheza ngoma ya ccm ya kuhairisha uchaguzi.. Maana ukumbuke ccm wanaamini (na wako sahihi kwa hili)
asilimia kubwa ya hawa wananchi ambao wanakesha kwenye vituo vya uandikishaji sio wao..Na wanajiandikisha kwa wingi ili waje kupiga kura na kuitoa ccm madarakani..! So kwa ccm ni kutafuta mbinu na sababu za kuendelea kuishi kwa siku nyingine..
chadema.we ni chama gn mkuu!
Mahatma Gandhi alisema "Kama ukitaka kubadili dunia anza kwanza wewe". Kwa maana hiyo mabadiliko ni wewe na si kulaumu. Waweza kugombea ukajitahidi uwe mbunge wa Mfano usiesahau wapiga kula wako.Hao viongozi bora utawaona sasa hivi tu wakati wa kukuomba ridhaa lakin wakifika mjengoni utakuja nikumbuka. Sikushawishi usijiandikishe lakini dah!