Serikali haitaki kuniandika kwenye BVR?

Serikali haitaki kuniandika kwenye BVR?

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,322
Muda huu nipo kituoni nikisubiri kuandikishwa kwenye BVR. Hili ni jaribio langu la nne. Uandikishaji ulianza tarehe 09/06/2015 na siku ya kwanza nilienda kituoni nikapewa na 56 mashine iliandikisha watu 42 tu, tar 10/06 /2015 mashine iliandikisha watu 79, nikiwahi kituoni watu walikataa kututambua sisi tuliobaki Jana yake.

Tar 11/06 /2015 niliamka saa 8 usiku na kuwahi kituoni nikapewa na 64. Mashine iliandikisha watu 40 hadi saa 7 ikazima sikuweza kuandikishwa.

Leo nimefika kituoni saa 9 alfajiri na nimepewa na 86. Sijui kama leo nitaandikishwa. Nipo kituo cha Nyanza kata ya Mkolani wilaya ya Nyamagana.

Mtaa wetu una watu si chini ya 1500 wenye sifa za kuandikishwa lakini tija na ufanisi wa kuandikisha ni duni. Mwamko wa watu kujiandikisha upo juu na wamejitokeza kwa wingi lakini vitendea kazi na watenda kazi hakuna. Lengo la serikali ni nini?
 
Inaonyesha wazi jinsi hilo zoezi lilivyojaa uhuni wa hali ya juu. Unahitaji majaribio manne ili kujiandikisha kutimiza haki yako ya kupiga kura!? Inasikitisha sana. Kuna kila sababu ya UKAWA kulivalia njuga hili swala kabla Watanzania wengi hawajaibiwa haki yao na Tume ya Uchaguzi na hivyo kukosa kujiandikisha na kutoruhusiwa kupiga kura. Watanzania wangapi wanaweza kuwa na moyo kama wewe kwenda kutuoni kujiandikisha mara nne!? Wengi wasingerudi baada ya siku ya kwanza. Poleni sana Mkuu na hongera kwa juhudi zako.
 
Ni jambo la kusikitisha kuona mashine ni moja, lakini hata hiyo moja haifanyi kazi kwa ufanisi.
 
Hakika molari ya watu kujiandikisha ipo juu sana, mathalani, nyanda za juu kusini, mbeya, watu wanaenda kupanga foleni ya kujiandikisha ktk BVR saa nne usiku pamoja na balidi kali lililopo sasahv ktk kanda hizo na wakati zoezi hilo huwa linaanza saa mbili kamili hata tatu asbh ya siku nyingine mpaka saa kumi na mbili jioni.

Inavyoelekea kuna uwezekano watu wakapiga kura kwa kutumia kadi za BVR na zile za zamani, maana unakuta mtaa wenye watu karbia 1000 walio na umri wa kujiandikisha, watahitaji siku 20 za kujiandikisha ktk hizi mashine za BVR zenye uwezo wa kuandikisha watu 50 kwa siku, sasa hizo mashine zipo kwa siku saba tu kwa kila mtaa ambayo ni sawa na kuandikisha watu 350 ambao ni sawa na asilimia 35 ya hao watu.
 
Ngwananzengo

Yaani kwa siku inasajili watu 40 tu? hii ni hatariiii sana aiseeee,mwaka huu wengi hatutaandikishwa basi zoezi lingekuwa 24 hours.
 
Last edited by a moderator:
Yaani kwa siku inasajili watu 40 tu? hii ni hatariiii sana aiseeee,mwaka huu wengi hatutaandikishwa basi zoezi lingekuwa 24 hours.

nafikiri hilo zoezi haliwezi kuwa saa 24 vile zile mashine zinafanyakazi kutegemeana na mwanga wa jua (solar power)
 
Yale majamba wazi kky. Hela wamekula wamenunua mashine mbovu. Nadhangaa mnunuzi hajaadabishwa mpk sasa. Na ss waTZ wajinga kupindukia. Hv kweli unaacha usingizi wako masaa yote hayo unaenda pigwa brd loooote kisa umsaidie fisi wadi mmoja kuendelea kutafuna hela zetu???? Kamata wote piga galagaza yote tushayachoka haya majitu yanachezea akili zetu. Nakumbuka zmn za Mkulu wetu JKN waziri gulani alienda nunua ndege akaleta bomu ikawa nyumba ya popo pale airpirt. TZ NI SHEEEEEEDDAAAAAAHH
 
Yaani kwa siku inasajili watu 40 tu? hii ni hatariiii sana aiseeee,mwaka huu wengi hatutaandikishwa basi zoezi lingekuwa 24 hours.
Siku ya kwanza uandikishaki ulianza saa 5 wakaandika watu 42, siku ya pili watu 79, siku ya Tatu watu 40 lakini mashine iliharibika saa 6 mchana ndio maana tuliandikishwa wachache.
 
Mkuu nakutakia ufanikishe na tafadhali pigana bila kukata tamaa hadi.utimize azima yako

Nia yangu nakuomba upigie kura ccm...
 
Ngwananzengo

Pole mkuu komaaa tuondoe udhalim wa magamba...ila naomba ututupie picha ya hiko kituo...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakutakia ufanikishe na tafadhali pigana bila kukata tamaa hadi.utimize azima yako Nia yangu nakuomba upigie kura ccm...
Samahani sana kiongozi, siwezi fanya huo ujinga. Kwa kipi kunilaza nje siku 4.
 
Wewe itakuwa ni mhamiaji haramu mpaka mashine inakukataa!
 
Wewe itakuwa ni mhamiaji haramu mpaka mashine inakukataa!
Pamoja na heshima kubwa kwako hata kama kifikra tuna tofauti leo hujaelewa mada. Mashine haijanikataa Bali uandikishwaji unasuasua kiasi sifikiwi. Muda huu fujo imeanza na waandikishaji wametoa taarifa Polisi.
 
Pamoja na heshima kubwa kwako hata kama kifikra tuna tofauti leo hujaelewa mada. Mashine haijanikataa Bali uandikishwaji unasuasua kiasi sifikiwi. Muda huu fujo imeanza na waandikishaji wametoa taarifa Polisi.

Haufikiwi kwa kuwa mashine inakukataa.

Pole sana, jaribu tena, usichoke, kuna siku itakukubali tu.
 
Ni masikitiko kwa mwamo mkubwa wa wananchi kuja kujiandikisha halafu vitendea kazi na watendaji wake wako chini ya viwango.

Kwenda kituoni kujiandikisha zaidi ya mara nne ni moyo mkuu unaonyeshwa na wazalendo kama wewe, kuleta mabadiliko ndani ya nchi kunahitaji uvumilivu wa hali ya juu.

UKAWA wanahitaji kufanya tathmini ya jumla ya zoezi hili na kwa sasa tuachane na mchakato wa kuwaza uchaguzi, kama watu hawajajiandikisha ni kazi bure kujipanga kwa uchaguzi, na zoezi hili lisipofanikiwa waathirika wakuu ni UKAWA, ccm wana mbinu nyingi sana, sasa sisi tukisinzia hapo kwenye kuhakikisha watu wameandikishwa hatuta fikia malengo ya MABADILIKO!!!!!!!!!!!!!!
 
Wewe itakuwa ni mhamiaji haramu mpaka mashine inakukataa!

FF, kumwita mwenzio mhamiaji haramu unaona ni sawa, uko wapi utu uzima wako na ukomavu wa kuwa mtandaoni kwa muda mrefu na ukapewa sifa ya kuwa JF Senior Expert Member.

Tofauti ya kimtizamo, ukada,dini, jinsia n.k isitutoe ufahamu na kupost unachojisikia.
 
Back
Top Bottom