Mkandara,Mchambuzi,
Ni wapi umepata wewe kuwa serikali mbili ilikuwa swala la chama? au hujui waliweza vipi kufikia maamuzi hayo?
Mkuu kwanini unatumia jicho moja kuangalia na kusoma mambo?Mkandara;10319551]Labda nirudie kusema hivi, Zanzibar wana kila sababu ya kulalamika na malalamiko yao yapo wazi kabisa. Chukulia moja Wazanzibar walidai kwamba rasilimali zetu zinazojulikana kama za Tanzania (muungano) iwe dhahabu, mafuta au gas hawafaidiki nayo, hakuna mgao maalum unaoeleweka ktk muungano huu japo jina la Tanzania linatumika.
Vema kabisa Mkuu.Nguruvi3,
Mkuu wangu bado wanisikitisha sana na hoja zako ambazo kila wakati unayemlaumu ni Mkandara pasipo kurudi na majibu ya kuridhisha isipokuwa chuki yako bunafsi na Utanganyika wako ambao mwalmu alisema ni sawa na kula nyama ya mtu.
Hao Wazanzibar unawasema kila mara ni katika kundi lako hivyo sioni tofauti yako na wao hivyo mjadala wako umejengwa kwa hja zile ziole za Uzanzibar na Utanganyika, mimi hazinisaidii kupata majibu yote.
Haya sasa umekuja na hili la kwamba Zanzibar hawachangii hata sentyi moja ktk mfuko wa Taifa na unatumia Jeshi sijui hilo jeshi linapata wapi mapato yake maana nijuavyo mapato ya serikali yanatokana na vifungu hivi hivyo nakuomba uanishe hapa jinsi mapato hayo yanavyokusanywa maana pande zote mbili yaani Upande wa bara na wa Zanzibar wote wamesema moja ya kero yao ni 1. Mkanganyiko wa uchangiaji na ugawanaji wa mapato. Sasa wewe uloelewa hili kuliko hata rais alokuja kufungua Bunge la katiba na hakueleza uchangiaji na ugawanaji mapato ukoje wewe twambie unafanywa vipi. Na hata wajumbe wa tume wamefikia wao kusema uundwe mfuko wa pamoja hivyo tueleze wewe mwanzo ilikuwaje usanyaji wa mapato ya taifa na ugawajai uko vipi kiasi kwmaba wengine wote washindwe kuelewa isipokuwa wewe na wenzako.
Vyanzo vya mapato ya Taifa vletu ni hivi hapa:-
[TABLE="width: 508"]
[TR]
[TD="colspan: 4"]Mapato ya kodi (TRA) - 46%[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 4"]Mikopo ya Misaada ya nje – 29%[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 4"]Mikopo ya masharti ya Biashara - 9.4%[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 4"]Mikopo ya Ndani – 9%[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 4"]Mapato yasiyo ya kodi – 4%[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 4"]Mapato ya Halmashauri za miji – 2.6%[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Hujanijibu bado unazunguka mbuyu mkuu wangu..wewe unayesema hawachangii ndio tueleze jinsi gani fedha hizi hupatikana nimekupa vyanzo vyake halafu wewe twambie kwa takwimu ulokuwa nazo..Vema kabisa Mkuu.
Nikuweke sawa, taifa letu ni lipi? Znz wana taifa lao, nasisi tumo humo kwa mujibu wa katiba ya 2010?
Au taifa letu ni Tanganyika.
Twende na chanzo kimoja baada ya kingine.
Mapato ya kodi - Znz inachangia kiasi gani TRA ya taifa na Tanganyika kiasi gani
Narudia tena, Salimin Awaadh, mwenyekiti wa kamati ya fedha ya BLW na mjumbe wa halamashauri kuu ya CCM kasema hivi'' Kwasasa znz haichangii hata senti moja''Hujanijibu bado unazunguka mbuyu mkuu wangu..wewe unayesema hawachangii ndio tueleze jinsi gani fedha hizi hupatikana nimekupa vyanzo vyake halafu wewe twambie kwa takwimu ulokuwa nazo..
Nguruvi3, Mchambuzi et al,
Kwa kuchangia zaidi, nitoe maoni yafuatayo mintarafu ya mtafaruku huu wa S2 au S3 na hatma ya JMT:
1. UKAWA inajumuisha CUF, na CUF ndiyo iliyoshinikiza mabadilko ya Katiba ya Znz kutamka kuwa Znz ni nchi katika kile kinachojulikana kama Muafaka.
2. Naamini Watanganyika/ Watanzania Bara wengi wamezoea kuamini kuwa Znz si nchi, hivyo mfumo wa S2 unawaridhisha (conservatives). Na wengine wanasema hata hayo mabadiliko ya kusema Znz ni nchi hayana maana, kwani Znz inatambulika wapi kimataifa?
3. JK pia alichukua msimamo huu wa kubariki mabadiliko ya Katiba ya Znz bila kujua athari zake mbele ya safari, kwa upande mmoja akitaka kuonekana kama mpatanishi na ili akubalike kwa Wanzanzibari, lakini pia kwa upande mwigine akitarajia kuwa ataanzisha mchakato wa Katiba ya JMT itakayokuwa juu ya ile ya Znz: alitaka kupumua. Ikumbukwe pia kuwa Karume mtoto alikuwa na msimamo wa Znz ni nchi. Hivyo, kwa namna fulani JK ni lame duck kwenye utata wa suala la utaifa wa Znz.
4. Wale wanaounga mkono S3 wanafanya hivyo kwa msingi wa retaliation (a la Mchambuzi)
5. Mtaji wa CCM kwenye kukosoa Rasimu uko kwenye sehemu tatu:
a. Takwimu za Tume,
b. Hoja kuwa serikali ya Muungano itakuwa haina uhusiano na mwananchi wa kawaida (kwa madai kuwa mwananchi anataka mbolea na masoko, na panadol na chumvi na mafuta ya taa!). Binafsi sijaridhika na maelezo na utetezi wa Tume kuhusu uwakilishi wa takwimu zao na uwiano wa hoja
c. Athari/changamoto za S3 kama zilivyobainishwa na Ripoti ya Tume (hisia za utaifa nk) kwa ujumla ni killer assumptions za Union Project.
6. Naamini Tume ilipendekeza S3 ikiamini ni njia ya kuilazimsha (serikali ya) CCM ishughulikie kero za muungano za miaka nenda rudi. Iliamini pia pendekezo litaibua mjadala chanya wa umma kuhusu aina ya muundo /muungano unaofaa. Naamini, kinyume na matarajio ya Tume, hata hivyo, pendekezo hilo la S3 limeibua hisia kali, mjadala hasi na hata kuibuka kwa UKAWA.
Kwa ujumla na kwa kifupi, pendekezo hilo na jinsi lilivyobebewa bendera na UKAWA kwa upande mmoja, na msimamo wa baadhi ya wajumbe wa Tume kwa upande mwingine, kumeleta mgawanyiko miongoni mwa jamii ya Watanzania. Badala ya mjadala wa Katiba mpya kuchangia kujenga jamii yenye umoja, kuna hatari ya kumalizika kwa mchakato huu tukiwa tumegawanyika zaidi. Nadhani kina Warioba sasa wanajuta kwani nchi inaweza kuingia kwenye machafuko kama misimamo hii mikali ya UKAWA na Tanzania Kwanza itaendelea.
Way Forward
1. UKAWA wakajenge hoja bungeni huku viongozi wao wengine wakiwa nje ya bunge wakielimisha wananchi. Hili litawafanya wasionekane kama kikundi cha watu wanaotaka vurugu.
2. Wajitokeze wanasheria (Lissu hawezi hili?) kujenga hoja na hata kufungua shauri mahakamani kupinga mabadiliko ya katiba ya Znz kuwa yalikiuka katiba. Najua alikuwa akipinga sana ukiukwaji huu wakatiba huko nyuma kwenye mijadala mbalimbali.
Hapana na si kweli. Aliyeridhia mabadiliko ya katiba ya 2010 ni makamu mwenyekiti wa CCM zanzibar, Amani Karume. Sheria ilipitishwa na BLW bila kupingwa wakiwemo CCM. Wananchi wakapiga kura ya maoni na 61% ikaridhia mabadiliko hayo. Hivyo mabadiliko ya katiba ni zao la Wazanzibar si chama kama unavyotaka umma uelewe.
Unataka kusema kutotambuliwa kimataifa kunatoa fursa ya znz kuwa juu ya katiba ya JMT. Isingelikuwa nchi, ni wapi kuna taifa moja lenye wakuu wa nchi wawili wakipokezana madaraka, kuanzia maamuzi hadi ulinzi na usalama.Mwanagenzi;103289742. Naamini Watanganyika wamezoea kuamini kuwa Znz si nchi, mfumo wa S2.mabadiliko ya kusema Znz ni nchi hayana maana, kwani Znz inatambulika wapi kimataifa?
JK alitaka kuwafurahisha wznz. Madhara ya kufanya hivyo ni wznz kuwa na mapembe dhidi yake.Mchakato aliuanzisha ili kuua mjadala wa S3. Unakumbuka Sitta alivyokumbana na kituko kule znz.Makosa ya JK ilikuwa kudhani kufanya alivyofanya ilikuwa bora, athari zake hakuziona wakati huo.​Mwanagenzi;103289743. JK pia alichukua msimamo huu wa kubariki mabadiliko ya Katiba ya Znz bila kujua athari zake mbele ya safari, kwa upande mmoja akitaka kuonekana kama mpatanishi na ili akubalike kwa Wanzanzibari, lakini pia kwa upande mwigine akitarajia kuwa ataanzisha mchakato wa Katiba ya JMT itakayokuwa juu ya ile ya Znz: alitaka kupumua. Ikumbukwe pia kuwa Karume mtoto alikuwa na msimamo wa Znz ni nchi. Hivyo, kwa namna fulani JK ni "lame duck" kwenye utata wa suala la utaifa wa Znz.
Si kweli, hujamtendea haki Mchambuzi.4. Wale wanaounga mkono S3 wanafanya hivyo kwa msingi wa retaliation (a la Mchambuzi)
CCM ilitumia takwimu chache katika tume ya Nyalali. Matokeo ya takwimu hizo hayakuangaliwa kwa namba bali kwa analysis. Hapa ndipo wengi mnapochanganya mambo5. Mtaji wa CCM kwenye kukosoa Rasimu uko kwenye sehemu tatu:a. Takwimu za Tume, b. Hoja kuwa serikali ya Muungano itakuwa haina uhusiano na mwananchi wa kawaida (kwa madai kuwa mwananchi anataka mbolea na masoko, na panadol na chumvi na mafuta ya taa!). Binafsi sijaridhika na maelezo na utetezi wa Tume kuhusu uwakilishi wa takwimu zao na uwiano wa hoja
Ndio maana tunasema kuna bias. Mbona hujaangalia S2 na atahri zake.c. Athari/changamoto za S3 kama zilivyobainishwa na Ripoti ya Tume (hisia za utaifa nk) kwa ujumla ni "killer assumptions" za "Union Project".
Tume iligundua kuwa kwasasa hakuna namna ya kunusuru muungano isipokuwa S2. Ilibaini kuwa kero zinazosemwa si kuwa zilipuuza, bali hazikuwa na majibu na ufa ni mkubwa zaidi.6. Naamini Tume ilipendekeza S3 ikiamini ni njia ya kuilazimsha (serikali ya) CCM ishughulikie kero za muungano za miaka nenda rudi. Iliamini pia pendekezo litaibua mjadala chanya wa umma kuhusu aina ya muundo /muungano unaofaa. Naamini, kinyume na matarajio ya Tume, hata hivyo, pendekezo hilo la S3 limeibua hisia kali, mjadala hasi na hata kuibuka kwa UKAWA.
Well, wewe hulioni tatizo la kupuuzwa kwa maoni ya wananchi. Huoni tatizo linalosababishwa na CCM katika kuburuza umma. Unaridhika kabisa kuwa CCM inafanya mambo mema. Ni maoni yako na una hakiKwa ujumla na kwa kifupi, pendekezo hilo na jinsi lilivyobebewa bendera na UKAWA kwa upande mmoja, na msimamo wa "baadhi ya wajumbe " wa Tume kwa upande mwingine, kumeleta mgawanyiko miongoni mwa jamii ya Watanzania. Badala ya mjadala wa Katiba mpya kuchangia kujenga jamii yenye umoja, kuna hatari ya kumalizika kwa mchakato huu tukiwa tumegawanyika zaidi.
Kama kuna tume yenye heshima ni ya Warioba. Na wala hata siku moja hawatajuta ndio maana wapo wanajibu mapigo tena kwa hoja na mantiki. Hii ni moja ya tume zenye heshima katika historia ya nchi yetu.Nadhani kina Warioba sasa wanajuta kwani nchi inaweza kuingia kwenye machafuko kama misimamo hii mikali ya UKAWA na Tanzania Kwanza itaendelea.
Kwani sasa UKAWA wanaonekana hivyo?Way Forward
1. UKAWA wakajenge hoja bungeni huku viongozi wao wengine wakiwa nje ya bunge wakielimisha wananchi. Hili litawafanya wasionekane kama kikundi cha watu wanaotaka vurugu.
Kwamba unaona tatizo ni katiba ya znz na ndio maana UKAWA wapo nje!!2. Wajitokeze wanasheria (Lissu hawezi hili?) kujenga hoja na hata kufungua shauri mahakamani kupinga mabadiliko ya katiba ya Znz kuwa yalikiuka katiba. Najua alikuwa akipinga sana ukiukwaji huu wakatiba huko nyuma kwenye mijadala mbalimbali.
Hapana na si kweli. Aliyeridhia mabadiliko ya katiba ya 2010 ni makamu mwenyekiti wa CCM zanzibar, Amani Karume. Sheria ilipitishwa na BLW bila kupingwa wakiwemo CCM. Wananchi wakapiga kura ya maoni na 61% ikaridhia mabadiliko hayo. Hivyo mabadiliko ya katiba ni zao la Wazanzibar si chama kama unavyotaka umma uelewe. Unataka kusema kutotambuliwa kimataifa kunatoa fursa ya znz kuwa juu ya katiba ya JMT. Isingelikuwa nchi, ni wapi kuna taifa moja lenye wakuu wa nchi wawili wakipokezana madaraka, kuanzia maamuzi hadi ulinzi na usalama.
Hoja kubwa ni kutumia neno nchi kuvunja katiba kwanza kabla hatuvuka mipaka. JK alitaka kuwafurahisha wznz. Madhara ya kufanya hivyo ni wznz kuwa na mapembe dhidi yake.Mchakato aliuanzisha ili kuua mjadala wa S3. Unakumbuka Sitta alivyokumbana na kituko kule znz.Makosa ya JK ilikuwa kudhani kufanya alivyofanya ilikuwa bora, athari zake hakuziona wakati huo.
Haya tunayoyaona ni matokeo na madhara ya maamuzi ya JK kuhusu kuwafurahisha wznz. Si kweli, hujamtendea haki Mchambuzi.
Alichosema Mchambuzi ni kuhusu G55 na retaliations. Akaongeza, ilikuwa ni suala la matter of principle.
Mchambuzi na Bongolander wakaenda mbali kusema tatizo sasa limefikia economic injustice.
Hujamtendea haki hata kidogo kwa kuchukua nusu ya alichosemaCCM ilitumia takwimu chache katika tume ya Nyalali. Matokeo ya takwimu hizo hayakuangaliwa kwa namba bali kwa analysis. Hapa ndipo wengi mnapochanganya mambo
Takwimu zinasaidia katika analysis, hazisimami zenyewe kama conclusions.
Uchambuzi wa tume ulihusisha takwimu na maoni. Huwezi ku-quantify maoni, unaweza kuyafanyia qualitative analysis.
Kuhusu uhusiano wa serikali na wananchi, kumbuka ile ni serikali kuu.
Uhusiano wake umejengwa kwa serikali 2 zenye ukaribu na wananchi.
Ni sawa na sasa ambapo kuna serikali za mitaa. Je, kuna umbali na serikali kuu.
Serikali kuu kazi yake ni majukumu ya pamoja ya nchi husika.
Ndiyo maana tume ikaondoa baadhi ya mambo ili yashughulikiwe na serikali husika.
Utawezaje kuwa na wizara ya madini ikiwa znz haiwezi hata kuchoma mkaa.
Znz inahitaji wizara ya uvuvi yenye nguvu, mkazo huo hauwezi kuwa sawa na uvuvi wa TanganyikaNdio maana tunasema kuna bias. Mbona hujaangalia S2 na atahri zake.
Je, kwasasa sisi ni taifa moja zaidi ya miaka 20 iliyopita au tumegawanyika.
Changamoto za tume zilikuwa kuwasaidia wajumbe kuona namna ya kukwepa hali hiyo.
Hivyo tukubaliane kuwa tume ilikuwa deep and scientific kuliko ilivyowahi kutokea.Tume iligundua kuwa kwasasa hakuna namna ya kunusuru muungano isipokuwa S2. Ilibaini kuwa kero zinazosemwa si kuwa zilipuuza, bali hazikuwa na majibu na ufa ni mkubwa zaidi.
Haiwezekani tume ya watu makini iamini kuwa kero za miaka 50 zinaweza kutatuliwa kwa changamoto chanya unazosemaWell, wewe hulioni tatizo la kupuuzwa kwa maoni ya wananchi. Huoni tatizo linalosababishwa na CCM katika kuburuza umma. Unaridhika kabisa kuwa CCM inafanya mambo mema. Ni maoni yako na una hakiKama kuna tume yenye heshima ni ya Warioba. Na wala hata siku moja hawatajuta ndio maana wapo wanajibu mapigo tena kwa hoja na mantiki. Hii ni moja ya tume zenye heshima katika historia ya nchi yetu. Kwani sasa UKAWA wanaonekana hivyo?
Nadhani hujaelewa maana ya kuondoka bungeni Kwamba unaona tatizo ni katiba ya znz na ndio maana UKAWA wapo nje!!
Mabadiliko ya katiba ya znz yalifanyika kwa mujibu wa sheria zao.
Mwenye uwezo wa kuhoji ndiye aliyewapa nafasi hiyo.
Nilidhani ungeshauri Rais awe impeached kwa kuruhusu katiba kuvunjwa.
Hili ni jambo jema sana unalosema, ingawa sina uhakika kama unamtakia mema JK.
Mkuu mimi sikatai kabia kuwepo kwa serikali 3. Ila nachosema Tanganyika mnayoidai ipo na katiba hii ya Muungano ni ya Tanganyika.Mkuu Nguruvi3, Mchambuzi, Mkandara
Tukiangalia huko nyuma karibu tume zote zilizoundwa na CCM zinakuwa ni tume makini. Tatizo ni kuwa CCM wanapounda tume wanasahau kuwa tume zinafanya kazi kitaaluma, sio kisiasa, ni kama kauli za kuunda tume wanazotoa viongozi wa nchi zinalenga kuonesha demokrasia, lakini sikumbuki kama kuna siku CCM imewahi kukubali maoni ya tume.
Nakumbuka tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Nyalali na kulikuwa na tume nyingine ya Warioba kuhusu rushwa...hakuna kilichopendekezwa na tume hizo kichokubaliwa na CCM kama kuna kilichikubaliwa, basi kilikubwaliwa kidogo na kwa shingo upande. CCM iko mstari wa mbele kuunda tume na kukataa yanayopendekezwa na tume.
Kinachofanywa na tume ya Jaji Warioba kujibu mapigo ni jambo sahihi, hasa ukizingatia kuwa baada ya tume kufanya kazi zao, pamja na kufanya kazi kwa moyo wanaishiwa kupokea kejeli na kupotosha yale waliyokusanya. Kwa maoni yangu mzee Warioba yuko sahihi kabisa.
as to whether JK alifanya makosa kuruhusu ukiukaji wa katiba na kufanya nchi iote ndani ya nchi, hilo ni kweli, lakini sioni kama ndani ya CCM kuna mwenye ubavu wa kukosoa hilo. Warioba amelisema wazi mara nyingi kuwa sasa Zanzibar ni nchi kisheria, kwa hiyo umewekwa msingi wa kisheria pia kudai Tanganyika.
Samahani kwa kuchelewa kujibu.Mkuu Kobello,
Pengine nikuulize - je, tunaweza fanya mambo yote ya Tanganyika na Zanzibar yawe ya muungano?
Kuhusu gharama - je ni Zipi hizo zitakazo ongezeka ambazo chini ya serikali Mbili hazipo?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hivi Kobello, ukimwita waziri mkuu Rais wa Tanganyika utakuwa umeongeza gharama gani? Ukiita wizara ya kilimo, afya, ujenzi n.k. wizara za Tanganyika utakuwa umeongeza gharama gani?Samahani kwa kuchelewa kujibu.
Hatuwezi kufanya mabo yote yawe ya muungano.
Gharama za kuanzisha na kui-maintain judiciary ya Tanganyika, separate from Tanzania and the total overhaul of the court system.
Administrative costs za idara mpya zitakazoanzishwa (bearing in mind hizi zilizopo zitakuwa either za Tanganyika au Muungano) eg. Ofisi ya rais, mamlaka za kodi na ofisi zitakazosimamia wizara zote zilizopo Bara na Visiwani.
Bunge jipya na ofisi yake.
Wazo la mfuko wa pamoja ni matokeo ya tume ya Amina Salum si tume ya Warioba, FYINguruvi3,
tatizo lako wewe unapoulizwa swali unakurupuka na majibu kisha unaendelea kuzungumzia kwa nini nimeuliza. Nimekuuliza swali rahisi kabisa ya kwamba wewe unayejua Zanzibar haichangii Muungano nimetaka kujua huo Muungano uko wapi ikiwa wananchi wamekanganyikiwa kuwepo na uchangiaji ana ugawanaji wa mapato ya muungano. Sii rais wala tume wameweza kujibu hilo na ndio maana tume hiyo imekuja na wazo la kuunda mfuko wa Pamoja hivyo ni kusema hakuna kitu Muungano bali tuna serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar. Ndio maana nikauuliza kijanja ili nipate kujua huo mfuko wa Muungano ( wa pamoja)ambao Tanganyika pekee huchangia uko wapi?
Na kero ya Wazanzibar imeelezwa wazi ktk maswala yote ambayo yanaunda huu muungano ambao haupo kiuhalisia isipokuwa jina lake kutumiwa na serikali ya Tanganyika. Na kama umenifuatilia nilionyesha wazi tulikotoka na sasa tumefika wapi kiasi kwamba utaona zamani kulikuwepo ushirikiano mkubwa baina ya Tanganyika na Zanzibar wakati wa mwalimu chini ya Ujamaa lakini baada ya kuingia Ubepari na kuunda vyama vingi kimsingi tumeharibikiwa, hapa ndipo panapotakiwa kutazamwa. Kifupi serikali isokuwepo ni ya Muungano maana hakuna mfuko wa pamoja na wewe mwenyewe umeshindwa kutuonyesha wapi Tanganyika na Zanzibar wanakutana.
Hivyo kama tulikuwa na mambo 22 hatukuungana, iweje tuwe na 7 ndio tuungane wakati watu ni wale wale na akili ni zile zile?
Tume zote ziliundwa na wenyeviti wa CCM.Mkuu Nguruvi3, Mchambuzi, Mkandara
Tukiangalia huko nyuma karibu tume zote zilizoundwa na CCM zinakuwa ni tume makini. Tatizo ni kuwa CCM wanapounda tume wanasahau kuwa tume zinafanya kazi kitaaluma, sio kisiasa, ni kama kauli za kuunda tume wanazotoa viongozi wa nchi zinalenga kuonesha demokrasia, lakini sikumbuki kama kuna siku CCM imewahi kukubali maoni ya tume.
Nakumbuka tume ya Jaji Kisanga, Tume ya Nyalali na kulikuwa na tume nyingine ya Warioba kuhusu rushwa...hakuna kilichopendekezwa na tume hizo kichokubaliwa na CCM kama kuna kilichikubaliwa, basi kilikubwaliwa kidogo na kwa shingo upande. CCM iko mstari wa mbele kuunda tume na kukataa yanayopendekezwa na tume.
Kinachofanywa na tume ya Jaji Warioba kujibu mapigo ni jambo sahihi, hasa ukizingatia kuwa baada ya tume kufanya kazi zao, pamja na kufanya kazi kwa moyo wanaishiwa kupokea kejeli na kupotosha yale waliyokusanya. Kwa maoni yangu mzee Warioba yuko sahihi kabisa.
as to whether JK alifanya makosa kuruhusu ukiukaji wa katiba na kufanya nchi iote ndani ya nchi, hilo ni kweli, lakini sioni kama ndani ya CCM kuna mwenye ubavu wa kukosoa hilo. Warioba amelisema wazi mara nyingi kuwa sasa Zanzibar ni nchi kisheria, kwa hiyo umewekwa msingi wa kisheria pia kudai Tanganyika.