Serikali 3 na gharama zake

Serikali 3 na gharama zake

Naomba niambie gharama hizo zilizokuwa highlited (njano) zitafutika kabisa kwenye gharama za serikali mpya ya Tanganyika?

Mimi naweza kukuonyesha ni kivipi zitaonekana tena, kwenye serikali mpya ya Tanganyiaka, kwa sababu baadhi yake zipo serikali ya Zanzibar.

Angalia pia vote 22 (3.3 trillion) na uniambie, pamoja na ku-service hiyo Debt, Tanganyika itakuwa na madeni yake apart from that??

Halafu utuambie kama gharama zitaongezeka au la.

Nguruvi3
Mkuu nitakujibu baadaye, nipo leo mzigoni. Ila tu gharama uloziweka zitakuwa ni gharama za Tanganyika kasoro zile ambazo umeziwekea mstari wa njano ambazo zita serve serikali mbili badala ya moja ilivyo sasa.
 
Kobello,
Mkuu wangu aidha mimi ndio sifahamu muundo huu wa serikali 3 ama kuna upotoshaji mkubwa kwa wananchi kuhusu matumizi ya neno hili - Mambo ya Muungano. Na ndio maana nikasema pengine tukiweka mambo yote ya Muungano litaeleweka vema zaidi.
Ni hivi Tunapozungumzia wizara ya Fedha kuwa ya Muungano, hii haina maana kwamba tutakuwa na wizara moja tu ya Fedha ya JMT hapana, ukweli ni kwamba Zanzibar watakuwa nayo na sisi bara tutakuwa nayo. Na ndivyo ktk wizara zote muhimu na kwamba kinachozungumziwa hapa ni Sheria mama za pamoja na zile ambazo zitaachwa chini ya nchi washirika. Serikali kuu lazima iwe na idara za ukusanyaji mapato yake, serikali ya Tanganyika itahitaji waziri wake wa fedha kuwakilisha bajeti yake ktk bunge lake na kadhalika.

Kwa mfano hapa Canada tuna waziri wa Afya wa serikali kuu na tuna waziri wa Afya wa kila nchi ktk shirikisho hili. Na hata Ukitazama Marekani nadhani wao waziri wa shirikisho huitwa Secretary hivyo utaona wana secretary of Health wa taifa na pia kila states ina Department of health. Pia utakuta hapa Canada, ile Province (State) ya Quebec mbali na kutii sheria mama ya Afya bure kwa wote wao wana vijisheria vyao ktk Afya ambavyo havipo Ontario kwa sababu sheria hizo ndogo zimeachwa ktk majimbo haya kusimamia na yote haya yanafanywa kutokana na utekelezaji bora wa huduma hizi kwa watu wake. Hili ndilo tazamio langu la kuongezeka kwa matumizi ikiwa kweli tutafuata muundo wa Shirikisho kama wafanyavyo walotutangulia.

Kwa hiyo nachotaka kusema mimi ni kwamba wizara zote ulizoainisha kuwa ni za Muungano haina maana hapatakuwa na wizara hizo ktk nchi husika ama kinyume chake bali zinainishwa sheria mama ambazo hazitakiukwa na nchi washirika ktk upitishaji wa sheria zao. Unaweza kupitia Ministries za Canada za serikali kuu na kisha tazama ktk Province (states) zake utazikuta pia zina mawaziri wake, kwa maana hiyo sisi tutakuwa na ongezeko la wizara za shirikisho ambazo gharama zake zitatokana na kodi za wananchi haswa wa bara maana huko Zanzibar ni kama hakuna kitu.

Mimi sidhani kama rasimu inamaanisha kwamba maadam AFYA sii jambo la Muungano basi serikali ya Muungano haitakuwa na wizara ya Afya - hawawajibiki, kiasi kwamba ikitokea swala la Ebola basi kila nchi ita deal nalo watakavyo hii ndio nasema ni kugawana umaskini. Nachofahamu mimi zipo sheria zinazowapa mamlaka serikali za nchi na zingine kuu ambazo hazitakiwi kukiukwa. Na kama kweli ndivyo itanavyotakiwa kuwa, mimi ndio skuelewa vema. Je, serikali hii ya Muungano itaweza vipi kuliweka swala la kuondoa Ujinga, Maradhi, na Umaskini ikiwa haya sii mambo ya Muungano? Sii tutakuwa tumerudi pale pale kwenye misaada ya MKUKUTA kuwa ni mambo ya Tanganyika!.

cc humprey
 
mimi sidhani kama rasimu inamaanisha kwamba maadam AFYA sii jambo la Muungano basi serikali ya Muungano haitakuwa na wizara ya Afya - hawawajibiki, kiasi kwamba ikitokea swala la Ebola basi kila nchi ita deal nalo watakavyo hii ndio nasema ni kugawana umaskini. Nachofahamu mimi zipo sheria zinazowapa mamlaka serikali za nchi na zingine kuu ambazo hazitakiwi kukiukwa. Na kama kweli ndivyo itanavyotakiwa kuwa, mimi ndio skuelewa vema. Je, serikali hii ya Muungano itaweza vipi kuliweka swala la kuondoa Ujinga, Maradhi, na Umaskini ikiwa haya sii mambo ya Muungano? Sii tutakuwa tumerudi pale pale kwenye misaada ya MKUKUTA kuwa ni mambo ya Tanganyika!.
Hilo ndilo ninalotaka kuzungumzia mimi. Hapo ndipo niliposimama mimi.
Angalau mwenzangu una-experience ya kuishi kwenye Federation (kwa muda mrefu nadhani ,siyo miezi kadhaa) kama mwananchi na siyo kuishi bwenini bali kufanya kazi, kwenda gengeni kununa vitafunio na mboga, kupeleka mtoto shule, hospitali, kuomba mikopo etc... kama mwananchi wa kawaida.

Tuna experience hiyo, watatubishia humu ila itabidi tu-reason nao hawa jamaa.
 
Kobello, Mkandara,

..mimi nadhani badala ya kuangalia Canada mngeangalia hapa nyumbani.

..serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na wizara zake inaweza kutusaidia kujua nini kitakuwepo kwenye serikali ya Tanganyia ikiwa CCM wataridhia ianzishwe.

..sasa sina uhakika kama SMZ ina wizara zote ambazo zipo ktk serikali ya muungano, na zinabainishwa kwamba wizara zinazohusiana na masuala ya muungano.

..kwenye SMZ kuna wizara ya fedha, na suala hilo linaeleweka. lakini SMZ hawana wizara ya ulinzi, wizara ya mambo ya ndani, idara yake yenyewe ya uhamiaji, pamoja na wizara nyingine ambazo zimebainishwa kushughulikia masuala ya muungano.

..pamoja na maoni yangu hayo, mimi nawashauri mrudi kwenye rasimu muangalie ni mambo gani yamependekezwa yawe ya muungano, halafu mjiridhishe kama serikali za Tanganyika na Zanzibar zitalazimika kuwa na wizara zake zenyewe zinazoshughukia masuala yaliyopendekezwa kuwa ya muungano.

cc Mchambuzi, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Kobello, Mkandara,

..mimi nadhani badala ya kuangalia Canada mngeangalia hapa nyumbani.

..serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na wizara zake inaweza kutusaidia kujua nini kitakuwepo kwenye serikali ya Tanganyia ikiwa CCM wataridhia ianzishwe.

..sasa sina uhakika kama SMZ ina wizara zote ambazo zipo ktk serikali ya muungano, na zinabainishwa kwamba wizara zinazohusiana na masuala ya muungano.

..kwenye SMZ kuna wizara ya fedha, na suala hilo linaeleweka. lakini SMZ hawana wizara ya ulinzi, wizara ya mambo ya ndani, idara yake yenyewe ya uhamiaji, pamoja na wizara nyingine ambazo zimebainishwa kushughulikia masuala ya muungano.

..pamoja na maoni yangu hayo, mimi nawashauri mrudi kwenye rasimu muangalie ni mambo gani yamependekezwa yawe ya muungano, halafu mjiridhishe kama serikali za Tanganyika na Zanzibar zitalazimika kuwa na wizara zake zenyewe zinazoshughukia masuala yaliyopendekezwa kuwa ya muungano.

cc Mchambuzi, Nguruvi3
Mkuu wangu sidhani kama ni busara kuwasikiliza Zanzibar ikiwa tunaelewa muundo wa serikali 3 ndani ya SHIRIKISHO unaundwaje na inakuwa vipi na ndio chanzo cha mjadala huu maana tayari tunayo rasimu ilopendekeza. Kama kweli tutashirikiana katika mambo yale tu yaloorodheshwa na sii kinyume ina maana tunaunda JUMUIYA baada ya kuvunja muungano. Ni ushirikiano kama ilivyo Jumuiya ya EAC kila mtu ana chake, na tutashirikiana tu kwa yale ambayo yamekubaliwa.

Sasa ya nini yote haya ikiwa tunayo EAC halafu tunaunda tena Jumuiya ya Tanganyika na Zanzibar? maana haiwezekani tukawa na shirikisho tukakutana kwenye mambo hayo, Tanganyika na Zanzibar zikalazimika kutokuwa na waziri wa fedha kwa sababu atakuwepo wa serikali kuu ya Muungano, Hizo bajeti za nchi zao zitawakilishwa vipi? na je sio ndio kurudisha makosa yale yale tulokuwa nayo ila tumeyapa jiko moja zaidi?. Na zaidi ya yote, hata hiyo Jumuiya ya EAC, Kenya wana vyombo vyao vya kukusanya ushuru, sisi tuna yetu, Uganda vile vile tunachokubaliana ni sheria moja itumike kutunufaisha sote. Haiwezekani kabisa kesho tukawa na shirika moja la ndege la EAC ndipo tutaanza kuumizana vichwa tena.

Na muda wote nimekuwa nikiwaeleza ya kwamba maadam tumegundua kuwa mambo yote ya Muungano hayakuwa ya Muungano ila ya Tanganyika, hii inadhihirisha kwamba mfumo wetu ndio ulokuwa na kasoro, sio serikali ngapi kwani dhamana walopewa serikali ya Muungano kwa nchi hizi mbili waliitumia kwa maslahi ya Tanganyika tu. na hawakuwaruhusu wao waunde wizara hizo ndani isipokuwa za serikali ya Muungano ambayo haikuwahudumia. Sielewi kama ilikuwa kosa la kimfumo ama viongozi wetu na Ubinafsi wao waliamua kufanya hivyo baada ya kubadilisha mfumo wa kiuchumi na kisiasa. Kwa hiyo ndio maana mimi toka mwanzo niliyaelewa malalamiko ya Wazanzibar, na kukubali kuwa dhamana ilopewa serirali kuu, sisi Bara tuliitumia vibaya kujinufaisha.

Hii inanipa wasiwasi sana na muundo huu ulopendekezwa na utakuwa wa kipekee vile vile, na ndio maana nimekuwa nikiwasikiliza Mchambuzi na Nguruvi3 ambao wao wamependekeza tuvunje huu muungano tugawane mbao na kuunda Jumuiya kama itahitajika kutokana na chuki ilotokea baina yetu (yale alotuasa mwalimu). Na ukweli ni kwamba kilichotakiwa ni kuhakikisha yale mambo 22 yalokuwepo yatunufaishe sote kama taifa moja na kama chaguo ni serikali 3 tukubali pia kuna gharama zake badala ya kuudanganya Umma.

Hivi kweli kuna watu walifikiri kina Mwalimu walikuwa wajinga kiasi gani kusema serikali 3 zina gharama kubwa na itakuwa mzigo kwa Tanganyika? Hivi kweli hao wanasiasa wetu na hasa UKAWA wanaweza kutuambia maneno yale yalikuwa na maana gani? Kwa nini kina Nyerere walisema serikali 3 itakuwa mzigo kwa Tanganyika, wao walielewa vipi? na nanyi nyote mnaopendekeza serikali 3 mlielewa vipi kuhusu muundo wa serikali 3 zilizokataliwa na waasisi wetu wa Muungano - Ukweli ni kwamba Waasisi walitazama mzigo huo utakuwa wa wananchi, lakini wanasiasa wa leo wanatazamia sana mapato ya gas na mafuta!

Jingine, ukiisoma rasimu vizuri utakuta wametumia sana neno NCHI moja ya Tanzania, hii inazua mkanganyiko mwingine juu ya NCHI hii kwa sababu mara nyingi nchi huwa haina Soveregnity, ni state ndani ya Taifa -Sasa kama Tanzania ni nchi sio Taifa, yenye sovereign ni nini?
 
Back
Top Bottom