Kwani tunauunganisha kila kitu? Nijuavyo mimi tunaunganisha baadhi tu ya mambo na ndivyo walivyokubaliana waasisi. Hatuunganishi kilimo na ufugaji, hatuunganishi tawala za mikoa na serikali za mitaa, hatuunganishi rasilimali nk. Tunaunganisha ulinzi na usalama, tunaunganisha mambo ya nje. Yale mambo ambayo huunganishi yatashughulikiwa na serikali washirika. Yale tunayounganisha yatashughulikiwa na serikali ya muungano. Ugumu unatoka wapi? Kwanini unanga'ng'ania serikali ya Tanganyika iwe na Wizara za muungano pia? Kwa nini leo hii Zanzibar haina Membe wao? Mimi nadhani tunachamba mno na matokeo yake ndiyo haya.
Mkuu nakuomba sana unisome kwa taratibu upate kunielewa. Sing'ang'anii kitu chochote ila hunielewi tu. Kila jambo na wakati wake mkuu wangu hakuna nchi serikali kuu na hasa chombo kama TRA hawana mamlaka ya kodi ya wananchi wake ila nchi washirika ndiyo mambo yao! na kodi zetu zipo katika kila jambo hivyo umuhimu wa serikali kuu kuwa ni yake pia upo. Hii habari ya mfuko wa pamoja sijui nchi zichangie mfuko wa hazina inatisha!
Narudi kwa Waasisi wetu na historia kwa ufupi.
Waasisi wetu waliandika katiba hii ya mwaka 1977, awali katiba hii ilitanguliwa na katiba kama nne hivi toka Uhuru wetu na kama sikosei ni katiba ya mwaka 1964 baada ya Muungano ndio ilikuwa na mambo 11 tu kutokana na kwamba tulikuwa na Jumuiya ya Afrika mashariki ambayo ndio ilishika mambo mengine 11. Hivyo Zanzibar ikawa mshirika moja kwa moja wa Jumuiya hiyo ndani ya Tanzania na hayo mambo 22 yalikuwemo vile vile ktk ushirika wetu. Pili, Zanzibar haikuwa na katiba yake ila ikiongozwa na Amri za Rais (Presidential Decrees) hivyo chama cha ASP na baraza la mapinduzi ndio walokuwa executive council na law maker kwa muda wote kabla na baada ya katiba ya mwaka 1977.
Hivyo katiba hii ya mwaka 1977 ilitokana na kuungana vyama vya TANU na ASP na kufuatiwa kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika mashariki mwaka huo huo. Hawa wanaouliza haya mengine 11 yametoka wapi ni kutokana na kutofuatia Historia ya muungano wetu na tumetoka wapi na tulikuwa tukienda wapi. Utawala wa CCM waliweka msingi mikuu ya Utawala wao wa Kiumla, chama kimoja, kujenga Ujamaa na muundo wa serikali mbili ilihali Zanzibar hawakuwa na katiba nadhani hadi hapo utaona waasisi wetu walielekea wapi. Misingi yote hii ilikuwa ndio kiini cha kuandikwa katiba hiyo ya Taifa na ikaitwa katiba ya kudumu. Kwa hiyo katiba hii ilipitishwa na bunge maalum lililoteuliwa na Rais baada ya masaa machache sana, kutokana na mwongozo na mwelekeo wa chama chao bila ridhaa ya wananchi.
Kwa hiyo katiba ya mwaka 1977 iliandikwa katika wakati tofauti kabisa na mazingira ya leo, walilazimika kufanya hivyo kutokana na hali halisi ya wakati ule bado siasa ya Ujamaa uliipa serikali milki ya kuhodhi njia zote za uchumi. Kila dola ilikuwa bado ikitaka kujua inamiliki vitu gani na hivyo maridhiano ya katiba ile ilikuwa baina ya viongozi wa ASP na viongozi wa TANU ilihali leo tunasema katika nchi ya kidemokrasia msingi mkuu wa Katiba ni ule unaoweka mamlaka yote mikononi mwa wananchi. Na wananchi wenyewe ndio sisi Watanzania sio Utanganyika wala Uzanzibar Je utayaweka vipi mamlaka hayo kwa wnanchi kwa kugawa kwanza mambo ya Muungano wao kama sii kuwagawa wao ili wagawane umaskini?
Hivyo katiba hii lazima itupe mwanga na maono ya mbele, inaondoa utawala wa kiumla, chama kimoja, Ujamaa wa seerikali kuhodhi njia za uzalishaji, haki sawa, ubaguzi, idumishe udugu wetu, na iwe sheria mama kwa nchi washirika hivyo sheria za nchi hazitakiwi kukinzana nayo hata kidogo. Hivyo kutokea kwa mapungufu haya ya katiba ya mwaka 1977 yalosababisha kuandika kwa katiba mpya ya Zanzibar ilokinzana na katiba hii ni kutokana na ukweli kwamba katiba hii haikidhi mahitaji ya sasa ambayo yametokana na mabadiliko makubwa ktk mfumo wa kisiasa na Kiuchumi. Sasa wenzetu hawakutaka kuendelea na sheria mama ilowabana ktk utawala wa kiumla, utawala wa chama kimoja, na Ujamaa ambao sisi bado ndio unaweka pamoja. Huu ni wakati tofauti kabisa mkuu wangu lazima tuone mbali..