Series (Special thread)

Kuna mzigo mwingine huu hapo...Duniani kunatokea sitofahamu na wanakufa watu wote ila wanao survive ni wale tu wenye Y Chromosome
...kaseries kazuri sana haka

Kuna mwamba mmoja atabaki sasa kuna sehem alijichanganya akakutana na watoto wa kike kama wote


Ina season one na iko na episodes 10!!

Itafutane hii
 
Kesho huu mzigo ndio unatoka season 3....Too bad ndio utakuwa mwisho wa hii series na haitoendelea tena

View attachment 2020615
Wahuni wa Napoli wamerudi tena mzee...Kitu kizuri ni kuwa Ciro anaonekana ali survive baada ya lile tukio la kupigwa risasi na kutupwa katikati ya bahari kwenye season 3..

Niliwahi kukuambia kuwa baada ya Gomorrah kutoa hadi season 4,jamaa walitoa movie mwaka jana inayoitwa The Immortal,humu ndani hasa hasa wanamzungumzia Ciro,kama unakumbuka toka Gomorrah inaanza Ciro walikuwa wanamuita "The Immortal "kama a.k.a...sasa kwenye ile movie ya The Immortal wametuonyesha Ciro alianzia wapi toka anazaliwa anakuwa majanga aliyopitia hadi kuitwa The Immortal..na wakati inaisha ile movie mwishoni kabsa Ciro alionekana anakutana na Gennaro..

Sasa kwenye hii season ya tano ambayo ni final season Ciro karudi...wote tunajua mabalaa ya Ciro


Huwa ni mgumu sana kufatilia ongoing series,ila kwa hii naenda mdogo mdogo
 

Attachments

  • Screenshot_2021-11-24-21-27-58-47.jpg
    23.3 KB · Views: 24
Duuuh! Kama huyo mwehu karudi basi hapatoshi Aisee...Ngoja niisubirie yote imalizike ili niushushe wote maana sitaki kusubiria week baada ya week mimi.
 
Hii ni series gani kiongozi
 
Umeipakua wap net naija siioni ?
 
Nikishabonaga series inasomeka NARCOS najua humo ndani ni balaa.madon wa mihadarati wanawatumikisha sana watumishi wa serikali tena wenye mamlaka za juu, kwa ajili ya njaa njaa zao...
 
Peaky Blinders mbona Kama najiforce kuikubali hiviii...
Season one siona maajabu yani au zinazofata ndo zipo moto
 
Shida sio kuielewa shida ni haina maajabu yanii....
Dah


Peaky Blinders leo haina maajabu?tulia nenda nayo taratibu Kiongozi

Peaky Blinders ni kama hizi series Breaking Bad,Ozark na zinginezo,ukisimulia utaambiwa ni kali balaa,ni kweli kali ila zipe muda,huko mbele utakuja kushukuru hapa

Ila ukienda na imagination zako kuwa ni kali,episodes za mwanzo tu zitakushinda maana kile ulichokitegemea hautakuwa umekiona kwa muda ule..

Acha nisubiri final season ya sita,inayotoka mwakani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…