Series (Special thread)

Cypher season 2 inatoka lini mdau?
 
Mkuu movie yenyewe kama ndio mbona ya kitambo sana!

 
Sasa nani analeta masikhara na ubishi wakati namuuliza Betram vitu alivyonielezea mzee? Na hatubishani hapa tunaeleweshana kwa facts that why mwisho wa siku tumekubaliana kila mtu anapenda anavyotaka.
Ukiangalia point yangu hapo kasema series zako ulizotaja zipo juu ya 7 na Money heist ni utani sasa mbona ina rate ya 8.3?
Na ukisema series G.O.A.T izo series Embu tupe sifa za izo series na uziweke hapa maana hata nikiangalia izo series zako ulizozitaja hakuna hata 1 ambayo imeizidi money heist hata kuwa na asilimia kubwa kupendwa na Google users tu na kama hauna facts kama hizi unaweza potezea tu.πŸ‘‡πŸ‘‡

 
Nani kakuambia Money Heist sio series kali mzee!?
Ni series kali tu mkongwe, ila ni series kali kulinganisha na series gani!?
 
Mzee, kuna post yako hapo juu umeuliza mbona Money Heist haipo katika top ten ya series kali za muda wote katika IMDB!
Hapa hauwezi kuwa serious mzee, hiyo series ni kali lakini bado haina ubavu wa kuingia katika top ten ya series kali za wakati wote.
Mzee, nimeshakuambia sababu ya watu kuikubali hiyo Money Heist zaidi za series zingine, siwezi kurudia tena.
 
Mzee mimi nimeona umefanya utani kuitaja Money Heist hapa. Unahoji kwanini hauioni katika top ten ya series kali za muda wote hapo IMDB. Nimekuambia hauko serious, sijakuambia Money Heist sio series kali, lakini kutaka kuiona katika ten G.O.A.T TV series, kwangu mimi huu ni utani, haiwezi kuwa hoja serious.
 


Kwa hoja yako hii, inaonekana Money Heist ni kali kuliko The Wire. Vipi wewe mkongwe, unaamini Money Heist ni series kali kuliko The Wire?
 
Nani kakuambia Money Heist sio series kali mzee!?
Ni series kali tu mkongwe, ila ni series kali kulinganisha na series gani!?
Anhaa! Kumbe kali so hapa unataka kulinganisha ukali.
Kabla sijaenda kwenye kulinganisha ukongwe Embu niambie sababu ya kuifanya hii series inaifanya WATU WOTE duniani waseme kali? Nipe vigezo au viashiria vya kuifanya hii iitwe series?
Niambie mkongwe wangu na hapo utajua sababu zangu za kukupinga kuhusu rate za IMDb
 
Sorry nenda kasome tena vizuri sijataja money heist tu bali na Game of Thrones why hazipo kwenye top 10?
Vigezo gani hasa vinazinyima izo mbili kutoingia kwenye iyo top 10 na kuifanya Chernobyl 🀣🀣🀣 kuwemo na wao hawapo? Au wanangu wa series ya 24 why series yao pendwa haipo?
 
Sijataja Money heist tu kuna Game of Thrones pia why haipo?
Ukisema watu wanafuata action tv shows Kuna series kibao za action kama strike back, Arrow, Warrior, Nikita, Into the badlands na nyingine kibao sijazitaja maana izo zikitoka husikiii reactions za watu kupost dunia nzima iwe clips, hashtags, characters wanaowapenda na wengine hata kuumizwa either mtu kuuwawa au kuteswa bali ni watu wachache sana wanaozifuatilia.
Ila goma la money heist na The Game of Thrones ni dunia nzima ndugu yangu na zinafuatiliwa na watu kibao.
Swali la kujiuliza why series kama Chernobyl na The wire ambazo ni G.O.A.T series kwa mujibu wa IMDb mbona hazikuweza kukubalika au kusubiriwa kwa hamu kuliko Game of Thrones na money heist?
Hata The wire wakati inatoka kipindi iko why watu wengi walikuwa hawaikubali maana kipindi iko tv shows zilizokuwa zinatamba ni 24 na Prison Break?

KAMA KITU NI KIBAYA WHY KINAPENDWA NA WATU WENGI DUNIANI AMBAO TUMETOKEA KWENYE MATABAKA TOFAUTI?
 
View attachment 1824193

Kwa hoja yako hii, inaonekana Money Heist ni kali kuliko The Wire. Vipi wewe mkongwe, unaamini Money Heist ni series kali kuliko The Wire?
Yes money heist ni series Kali kuliko The wire kwasababu imeuza sana, inafuatiliwa dunia nzima, Tuzo za kutosha, inapendwa na Google users(Umeshaprove tayari) na pia ukiingia kwenye source yako pendwa ya IMDb πŸ˜ƒ nenda kaangalie category ya the most watched TV shows of all time Money heist ipo juu ya The wire.
Ngoja nikusaidie Top 20 tu za The most watched TV shows of all time za IMDb ni:
1:Game of Thrones.
2:Stranger things.
3:The walking dead.
4:13 reasons why.
5:The 100.
6: Orange in the new black.
7:Riverdale.
8: Grey's anatomy.
9: The flash.
10:Arrow.
11.Money heist.
12.The bing bang theory.
13:Black mirror
14: Sherlock Holmes.
15: Vikings.
16πŸ˜›retty little liars.
17: The vampire diaries.
18: American horror story.
19: Breaking bad.
20: Lucifer.

Hapo nimekuletea ushahidi wa why the money heist ni kali kuliko the wire so nipe za kwako ambazo hata tunaingia kwenye sources kubwa tunazikuta na sijacompare story maana series zote duniani zina stories tofauti zingekuwa sawa wangeshapelekana mahakamani.
 

 
Wewe ndugu yangu Embu nikuache kidogo maana hujui nini tunabishana.
Hivi kuna series duniani ambayo story yake haijapondwa? Nitajie iyo series ili nikuletee watu wanavyoichambua series

Wewe ndio wale Fanboys ambao hata muambiwaje hamuelewi siwezi poteza mda maana nkikutajia series hapa utaenda kutoa statistics zako za kipuuzi huko kwenye web
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ YES MONEY HEIST NI KALI KULIKO THE WIRE, acha acha acha kabisa mkongwe!!!
Naona Breaking Bad ipo nafasi ya 19 katika hiyo list πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚, Stranger Things namba 2.
Mzee hii Money Heist ni series ya kawaida sana kulinganisha Breaking Bad, Chernobyl au The Wire. Ngoja nikuchekeshe zaidi, hii Money Heist haiifikii hata Lost, ingawa Lost haipo katika hiyo list ya TV shows zilizowahi kutazamwa zaidi ila bado ukiziweka pamoja hiyo Lost inashinda asubuhi na mapema (kwa wanaojua contents and quality lakini).
Mjomba kwa huu mtazamo wako, nafikiri haushindwi kusema Drake ni mwana Hip Hop bora kushinda Kendrick Lamar. Populality and quality are different terms Broh.
 
Ukiondoa documentaries, GOT ipo katika top 10 mzee. Kwanza bado ni makosa kuzitaja GOT na Money Heist katika sentensi moja, yaani hapo ni sawasawa na kuwataja Eminem na 6ix9ine katika sentensi moja, kwasababu tu 6ix9ine amevunja rekodi iliyowekwa na Eminem katika mtandao wa YouTube.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…