Series (Special thread)

Acha kabisa mkuu. Unakumbuka walivyomuua renee walker? Alishikwa na hasira za hatari
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kabisa mkuu. Unakumbuka walivyomuua renee walker? Alishikwa na hasira za hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatari sana!Scene nyingine kali ni ile alivyokuwa amekamatwa na kufungwa china,akiwa huko aliteswa sana lakini hakuisaliti nchi yake japokuwa serikali ilikuwa imemtelekeza!Sasa kuna magaidi walikuwa wanamuhitaji Jack ili wamuue kama kisasi kwa Jack kumuua moja wa ndugu wa magaidi hayo!Sasa wakaiambia serikali iwape Jack ili nao wawape location ya gaidi hatari Assad!Serikali katika kipindi hicho iliamua kunegotiate na China ili warudishiwe Jack ili wamtoe sadaka kwa magaidi hayo!Jack akakubali na ikafanyika exchange,Jack akaingia mikinoni mwa jamaa ambaye ndugu yake ndiye aliuwawa na Jack!
Basi jamaa akamchukua Jack kwa ajili ya kumpa kifo cha taratibu na cha mateso!Daaah,namna Jack alivyochomoka hapo ni hatari maana nakumbuka alizamisha meno kwenye koo la mmoja wa magaidi na kuondoka na koo lote!Hiyo scene nilikuwa nairudia rudia!
 
Halafu ilikua vigumu sana kutabiri msaliti atakua nani. Ila chloe o brian alikua humble na obedient sana kwa jack bauer

Sent using Jamii Forums mobile app
Yes,nakumbuka mme wa Chloe alitekwa na kulazimishwa kutengeneza program ya kulunch nuclear head,alipogoma jamaa walizamisha drilling machine ya mbao kwenye bega la jamaa!Mshikaji akalainika!
 
Ujue series ni kama mpenzi wako wewe umempenda na kumuona mzuri ila mwenzako anamuona mbaya ndo vivo ivo kwenye series wakati wewe unaiona kali mwenzio anaona upuuzi mtupu sio siri mimi strike back kwangu ni kali kuliko 24 maana 24 niliangalia episode 2 nikaifuta hapohapo. So kila mtu angaalie anachopenda
 
Hakyanan umenipa mzuka wa kurudia whole season
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama uliangalia episodes 2 ukatupa basi hujafaidi kabisaaa!
Strike back haina story kabisa,nimeangalia season 1 na sasa nimeanza season 2!Yaani ni risasi tu,mission zimefanywa kuwa simple sana!Yaani kila episode,more than 75% ni mapambano ya risasi!
Halafu kila muda inaonekana wanajua adui yuko wapi,hata akitoroka unakuta wanajua hapo hapo na wanaelekea eneo aliko,risasi zinaamza upya!
Pia nimeshangazwa na kisa kimoja,eti jamaa ana bunduki halafu yuko kwenye mapambano na adui,adui tayari ameishiwa risasi halafu eti jamaa linaweka bunduki pembeni ili wapambane kwa ngumi!Daah nilivyofika hapo nikasema,shiiit!
 
Hahaha, waambie mkuu. Ili wakawajue kina tony almeida, bill bucchanan, kanali ike dubaku na yule jamaa alikuaga mlinzi wa rais mogan baadae akawa anatifua bi martha mke wa rais. Vipi kuhusu president palmer? Alikua assassinated mdogo wake akajaribu kuvaa viatu ila ikawa patashika nguo kuchanika. Unakumbuka yule dogo gaidi wakiarabu alijiconseal kwenye room kavaa mabomu anataka kujilipua halafu ghafla anshangaa bauer anakuja na mama yake mzazi pale? Renee walker wa FBI alikua aridhishwi kabisa na interrogation techniques za bwana bauer ila baadae naye akaja kua konki. Acha kabisa 24

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa sirudii series ila hiyo naweza kuirudia kila nikianza kuisahau!
 
Daah, nimeingia chaka!Strike back hamna series humo!

Huwezi kufananisha strike back na 24

Haiwezekani 24 ni moto ule na ukiachana na breaking bad hakuna kitu kikali kama kile na hakitakuwepo mkuu

Kama hujaangalia 24 angali

Strike back nimeangalia pia ila ya kawaida sana.


Pamoja na hizo zote ni kwamba mtu akiwa mzuri majority watamkubali hata mwenyewe angalia majority.

24 is next level mzee acha kabisa

Yaani unaangalia epsode mbili tu unasema hakuna kitu haupo serious

Kama uliangalia serious za kuanzia 2007 kurudi nyuma utakubaliana na mm now day hakuna mawe

Prison break

24

Lost

Breaking bad

Na zingine ni bouma achana na mastrike back hayo




Mkuu kutupa bunduki ili mpigane kwa mkono kwenye movies na series mbona ipo sana

Tafsiri yake ni kwamba adui anataka asionekana kakuonea kwahiyo anatupa bunduki ili muwe sawa.
 
Pia nimeshangazwa na kisa kimoja,eti jamaa ana bunduki halafu yuko kwenye mapambano na adui,adui tayari ameishiwa risasi halafu eti jamaa linaweka bunduki pembeni ili wapambane kwa ngumi!Daah nilivyofika hapo nikasema,shiiit!

nimecheka hapo juu..na huwezi amini style yangu ya kuangalia movie ni kama nasikiliza radio

huwa siangalii kwanza ninachofanya ni kui play kisha na minimize window naendelea fanya

mambo mengine kwa PC huku nasikiliza story ya movie bila kuona picha,ninaposikia story tamu

naacha ninachokifanya "nacheki hiyo movie" ila nikiwa nasikia kila saa milio ya risasi kama (strkbck)

natoa naweka movie ingine,hapa nilikua nasikiliza strikeback,huku nasoma comment zake hapa JF

kwenye kusoma si ndio nikakutana na hiyo comment yako hapo juu,sikutaka kufikiria mara mbili

nimeshaitoa na sitoiangalia tena,napenda season za type ya Money Heist,Blacklist,shooter,nk.

Kama kuna unazozijua za type hiyo naomba nisaidie majina au yeyote anaezijua movie za namna hyo

zisizo na makelele,story tamu,unaangalia movie mpk roho inakudunda wewe muangaliaji "such type"
 
Mkuu kutupa bunduki ili mpigane kwa mkono kwenye movies na series mbona ipo sana

Tafsiri yake ni kwamba adui anataka asionekana kakuonea kwahiyo anatupa bunduki ili muwe sawa.

movie ya namna hyo ikifka eneo hilo,naitoa siangalii

movie piganeni kwa silaha ndio movie,sio mnatuigizia

hadi kupigana ngumi,eti ngumi 1 tu mtu kafa (ushenzi mtupu)
 
Umeshaangalia 24?Iangalie hutojutia!
 
Yeah,24 nimeangalia kwa sasa kama mara 3 season 1 mpaka 8!
Kwenye hiyo strike back labda sikueleza vizuri,ni kwamba adui alikuwa anajua kabisa anapambana na kikosi na wote wapo eneo la tukio!Akajikuta one to one na mmoja wapo,wakapambana kwa risasi mpaka anayepambana naye akaishiwa risasi na kujikuta wako uso kwa uso!Eti badala ya kummaliza ili aendelee kupambana na wengine,eti anaweka silaha pembeni wapigane ngumi wakati huo huko risasi zinasikika wenzake wakiendelea kupambana!Daaah nikasema nini hiki?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…