Series (Special thread)

Series (Special thread)

Link 1080 Size ni 7.7GB
Link 720 Size ni 1.1GB
Link 480 Size ni 417MB
Network haiko sawa kwa sasa nitimalizia kesho
Screenshot_20260327-232659.png
 
Episode 1 nimeikata

Series ni kali sana ikielezea Police anayeitwa Harry Hole anayejaribu kufufua kesi ya miaka mitano ya Bank Robbery iliyohusisha na mauaji ambapo muuaji alivaa mask.

Harry Hole anaji organize na team ya wadada wawili katika upellezi wa tukio hilo la miaka 5 iliyopita.

Taratibu upelelezi wao unaanza kuonyesha mwanga kwa kuja kubaini kuwa aina ya silaha iliyotumika katika mauaji ya tukio la Bank Robbery ilikutwa na kikosi cha Narcos kilichokuwa kinafanya operation ya kukamata wauza unga.

Katika ufuatiliaji wao wana connect dots kwa kulinganisha matukio, kuwa kulingana na silaha hiyo kuwa adimu basi ni lazima kutakuwa na connection ya hao wauza unga kuhusika na tukio la Bank Robbery au hao wauza unga yawezekana ni wauzaji pia wa silaha na kwamba hiyo silaha waliwahi kuuza kwa mtu aliyefanya ujambazi Bank na kuua.

Sasa ile team ya wadada wawili wanaosaidia huu upelelezi wanaamua kuomba surveillance footage kutoka kwenye kikosi cha Narcotic kujaribu kuangalia kama wataweza kuona mtu yeyote ambaye ana link kwenye kesi yao ya Bank Robbery.

Katika kuangalia zile footage wanakutana na sura ya mtu ambaye ni office mate yao yani ni polisi mwenzao. Maswali yanakuwa mengi kwanini aonekane kwenye tukio la kujihusisha na magenge ya wauza unga?

Wanamshirikisha Harry Hole ambaye ndio kiongozi wa hiyo Op, na sasa wanakubaliana kwamba waende moja kwa moja kwa huyo Afisa mwenzao na wamuhoji kivipi akutwe kwenye tukio la wauza unga.

Jamaa anaoneshwa picha yake lakini anapinga kuwa huyo sio yeye na washkaji wanakosa ushahidi mwingine wa kuthibitisha.

Kuanzia hapa ni kwa msaada wa AI

Mambo yanabadilika ghafla pale mmoja wa maafisa wa kike anaingia kwenye ufuatiliaji binafsi. Anamfuma live yule polisi akifanya mauaji ya mtu ambaye tayari alikuwa akifuatiliwa na timu ya Harry Hole. Mshtuko ni mkubwa, sasa hakuna tena kukanusha, macho yake yameshuhudia ukweli.

Kwa bahati mbaya, hatua yake ya kumfuatilia inageuka kuwa hatari. Afisa huyo mchafu anamgundua na kumshambulia, na hatimaye anamwua mwanamke huyo. Ni tukio la kushtua, linaloonyesha jinsi usaliti ulivyo ndani ya mfumo wa polisi na jinsi mtu wa karibu anaweza kuwa adui mkubwa.

Wakati huo huo, Harry Hole yupo mbali na simu yake, akijaribu kujenga uhusiano wa kifamilia kwa kucheza na mtoto wa mpenzi wake kwenye swimming pool. Scene hii ya utulivu na furaha inakuwa kinyume kabisa na machafuko yanayoendelea. Simu inalia, lakini Harry yupo busy diving na mtoto, akishindwa kuipokea. Hii inazidisha tension—wakati Harry anashughulika na maisha binafsi, timu yake inavunjika na mmoja wao anapoteza maisha.



View attachment 3563488
Inavutia kutizamwa
 
Naangalia Zeta hivi hizi movie za wa-colombia, wanaomiliki cartel naona wanaoandaa cocaine wanawake wako uchi, sio movie ya kwanza naona hivi, ni kwanini wanabaki na 👙tu?🤔
So they don't steal
So they don't compromise quality/don't contaminate the product
So they don't leave any trace

Ni kama maabadar tu ya kutengeneza product ambayo haitakiwi ibaki mwilini kw mtengenezaji au ichafuliwe kwa namna yoyote na Sababu zingine ambazo wakongwe akina Vincenzo Jr Scars dosho12 All watakuja kuzieleza
 
So they don't steal
So they don't compromise quality/don't contaminate the product
So they don't leave any trace

Ni kama maabadar tu ya kutengeneza product ambayo haitakiwi ibaki mwilini kw mtengenezaji au ichafuliwe kwa namna yoyote na Sababu zingine ambazo wakongwe akina Vincenzo Jr Scars dosho12 All watakuja kuzieleza
Duhh sawa asante kunielewesha nimekuwa nikijiuliza sana hilo swali!
 
So they don't steal
So they don't compromise quality/don't contaminate the product
So they don't leave any trace

Ni kama maabadar tu ya kutengeneza product ambayo haitakiwi ibaki mwilini kw mtengenezaji au ichafuliwe kwa namna yoyote na Sababu zingine ambazo wakongwe akina Vincenzo Jr Scars dosho12 All watakuja kuzieleza
Naunga mkono hoja Cc Seran

Kacheki na movie hii ndio ilikuwa ya kwanza kuweka watu wakiwa wanachakata kokeini wakiwa nusu utupu new jack city
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom