Series (Special thread)

Mhhh! Siku hizi movies/series zimekua nyingi mno hadi unakosa muda wa kutazama mambo yanakupita.

Halafu ukija kugusa tu unakutana na blunder iyo hatarii wakati huo mitandaoni unakuta washaihype sanaa!
Unaweza kuangalia movie kwa siku 5 bila kuimaliza.

Tunabaki kumiss old moments unaona bora urudie tu vyuma vya zamani. Ule utunzi wa zamani sijui umeishia wapi aisee!

Season 3 ongoing 🍟
 
Nilimisi zile harakati za gereza la sona sio powa hata panya akipita kwenye sinyenge anakula shaba
 
Nilisikiliza baadhi ya nyimbo kwenye album yake nimeipenda Run away na nyimbo iliyobeba jina la album
Fundi sana huyu na Kuna enjoy the show mule pia Kuna mkwaju wa take me back to la na timeless ni miongoni mwa wasanii ninao wachangia sana hela kule Spotify
 
Nilimisi zile harakati za gereza la sona sio powa hata panya akipita kwenye sinyenge anakula shaba
Sona kumechangamka sana na nyapala wa mule hachekeshi.
Ndo gereza ambalo Scofield aliingia akiwa hajui anatoka vipi. Humo wakina Mahone na Bellick wote walikua ni wachumba tu, wanasubiri muijiza ya Scofield amtoroshe mwamba anaeitwa Whistler ili watoke nae.
 
Lile gereza sio powa mkuu
 
Nipo episode ya pili ya dare devil naomba niseme kwamba nilichelewa kukijua hiki kigongo na nnajuta kwanini sikuangalia dare devil zilizo pita😊😊😊

Nilikuwa nazifananisha na mamuvi ya spiderman The Adam, Dead pool, Agent of shield n.k kumbe nilikuwa nakosea.

Kwanza ina episode za kutosha, pili ina kamkong'oto ndani yake, tatu ina stori nzuri nne utaongezea mwenyewe
kuna dirt cops wamekipata walichokuwa wanakitafuta
 
Nne haina utoto kama movie nyingine za MCU
 


Daredevil season 2 tunaipata mwakani kama unaweza zitafute Daredevil original zipo season 3
 
Hiyo ya karma hata Mimi nimekutana na hilo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…