Series (Special thread)

View attachment 3177281

Hili toto linazua mijadala mikubwa mitandaoni kama mtu mbaya The Jackal ameliua au la!

Kwa ninavyowajua wabongo watakua wamelipendea msambwanda Tu hakuna kingine🤕

😀😀😀 si unatujua wabongo 😀😀😀

Demu lina jeuri, linajiona lijanja kisa tu linajua majina ya silaha mbali mbali na kushika bunduki. Wenzake wameangamizwa katika msako wa the Jackal ila yeye bado hajifunzi kumuendea kiakili zaidi. Yeye anataka kumdaka tu mwamba kwa gharama yoyote ile 😃😃. Alizidisha ujuaji. Sijui kipi kilimfanya afikirie eti ataweza kumdaka kirahisi rahisi tu top sniper kama Jackal nyumbani kwake, apajuapo kila kona na huenda kaset kila aina ya mtego...yeye anajiendea endea tu...

Ila sambwanda lipo, hivyo wabongo tukamvumilia
 
Season 2 utamuona tena 😎😀😄
 
Season 2 utamuona tena 😎😀😄View attachment 3177883
Natamani kusema 'nakuhakikishia hata kuwepo' ila haya mambo huwezi jua.

Hakuna mantiki ya kumfufua na hakuna namna ya kutuaminisha alipona kule Spain. Ukimuangalia huyu demu kwa jicho lingine, unaweza kusema yeye ndiye alikuwa adui na Jackal ndiyo steringi eti... Na Season 2 itamfanya Jackal awe main protagonist huku akina Isabel, Mzee Winthorp na Whitelock wakiwa main antagonists.

Jackal ataendelea kutembeza adhabu kwa wahuni kwenye system, huku akifukuziwa na akina Osita (na Osita atakuwa anamsaidia kisiri siri ili amshughulikie kwa ndani Isabel), huku pia akijitahidi kunusuru ndoa yake na kuwalinda awapendao. Itakuwa rahisi zaidi ya audiences kuconnect na Jackal na kumpa support.
 
Hii series kalii sana mwaka huu tumepata series nyingi kalii sana huu mwaka mzuri sana
 
Hii series kalii sana mwaka huu tumepata series nyingi kalii sana huu mwaka mzuri sana
Hii series kalii sana mwaka huu tumepata series nyingi kalii sana huu mwaka mzuri sana
Naomba recommendations za nyingine kama hii. Hii yenyewe nimeibahatisha tu maana nilikuwa na kile kitabu ila sikukisoma mpaka nikaja kukipoteza. Adaptations za vitabu napenda maana nilikuwa napenda kusoma vitabu vya action. Authors niliokuwa nawakubali sana ni Lee Child na David Baldacci, hivyo Reacher sikuiacha inipite maana nimesoma vitabu kama 6 hivi vya jack Reacher.

Cross nimeangalia Season 1 japo sijawahi kusoma vitabu vyake. Jack Ryan nimeshindwa kuielewa baada ya season 1 tu.
 
The penguin
The diplomat
A man in full
Paris has fallen
The night manager
Bodyguard
Eric
Fallout
Traitor
Patriot
Fubar

Hizo mkuu hapo niongeza ni
The Americans na Tulsa kings
 
NEXT SEASON
Akishampata Mama Watoto Wake Nuria,
Utamu Wote Wa Msimu Wa Pili Utahusisha Kuzitaka Pesa Zake Ambazo Hajalipwa.

Je Bianca Wakati Huo Atakuwa Upande Upi
View attachment 3177940
Bianca tunampenda ila ndiyo hivyo tena mkuu.

Episode ya kwanza itaanza na shot ya juu ikiangalia miamvuli meusi ikinyeeshewa mvua nyepesi. Camera itapan huku na kule kuonyesha magari meusi yakilindwa na majamaa yenye suti nyeusi, miwani meusi na vi earpice vyeupe vyenye coils masikioni. Tutagungundua kuwa watu hao wapo makaburini na litaonyeshwa jeneza lililofunikwa na bendera ya UK likishushwa kaburini mdogo mdogo. Picha ya Bianca kwenye frame itaonekana kwa pembeni, halafu watatupa shots za Isabel akiwa na sura ya ukauzu, huku Paul, mume wa Bianca, na mtoto wake wakiwa wanalia....


Baada ya hiyo scene ya mazishi itakayokkuondolea kila doubt kwamba demu hayupo tena duniani, ndiyo utaanza kuona makeke ya Jackal sasa.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…