Godfather of Harlem nimeimaliza rasmi jana na iko poa sana kama rate yake ilivyopewa.
Kitu kimoja tu ambacho nilikuwa naanza kuona kama director alikuwa anaenda kutukatili ni kuitamatisha Series kwa season 3.
Kiu ya audiences ni kuona muendelezo wa maisha ya Bumpy Johnson yanakuwaje baada ya yeye kuacha u-drug dealer.
Na vipi kuhusu kiapo chake cha kulipiza kisasi cha rafiki yake Malcom.
Na vipi Harlem itaweza kuwa kwenye utulivu chini ya imaya ya Chin Gigante ambaye amepewa full authority na Bumpy baada ya kujitoa kwenye game.
Lakini baada ya kuona hii picha kwenye ukurasa wa mmoja kati ya actor wa hiyo series nikajiridhisha kuwa director anaenda kukata kiu yetu.
View attachment 3072921