Ni kweli kuna tofauti kubwa ya idadi ya waumini wa dini hizo kati ya mwaka 1957 na 1967. Lakini inavyoonekana hapa ni kwamba waisilamu wanaamini kwamba sensa ya mwaka 1957 ndio yenye takwimu sahihi na ya 1967 haina takwimu sahihi. Mimi swali langu ni hili; je, haiwezekani kuwa kinyume chake; kwamba sensa ya mwaka 1967 ndio yenye takwimu sahihi na ya 1957 haina takwimu sahihi? Kama wanafunzi wawili wamekosa jibu la swali moja katika mtihani, iweje mmoja ang'ang'anie kwamba jibu la mwenzake sio sahihi (huku hata yeye akiwa amekosa)? Wanaojenga hoja kwa misingi ya sensa za 1957 na 1967 nashindwa kuwaelewa. Kama mtu ana nia hasa ya kujua idadi ya waumini, aangalie mchanganyiko wa sample mbalimbali kwenye makundi kadhaa ya kijamii, maybe atapata idea!
Nakubaliana na wewe 100%. Unajua sisi tatizo letu ni ELUMU sii Waislaam wala Wakristu na ujinga huu ndio umepelekea kufika hapa tulipo. Hakuna uhakika wa takwimu zote zilizowahi kutolewa nyuma na kibaya zaidi tumeendelea kuamini kwamba tofauti zetu za kiimani zinaweza kusababisha UDINI kumbe kutokuwa na taarifa hizo ndiko kunajenga Udini zaidi.
Binafsi yangu sikubaliani na dhana ya baadhi Waislaam inayotafsiri kitendo cha Nyerere kuondoa kipengele cha imani ya dini ktk sensa. Yeye kama Mjamaa na mtu alotaka kujenga taifa moja lenye kuondoa tofauti zetu alifanya hivyo makusudi na kuhakikisha kwamba ni jukumu la serikali yake kupeleka maendeleo moja kwa moja kwa wananchi na ndio maana alitaifisha shule na hospital zote za dini akaacha zile za watu binafsi ili serikali ndiyo ipeleke huduma hizo kwa wananchi. Serikali ikawa ndiye mgawaji (sole supplier) wa vitu hivyo..Hivyo mfumo wake uliendana na dhamira yake na akaweka uzalishaji na usambazaji kuwa chini ya serikali..
Tatizo la leo lilofikia mimi kupingana na sensa hii ni kwa sababu vita hii muhimu ktk maendeleo ya WATU maskini vimerudishwa ktk mikono ya watu binafsi na hasa vyombo vya dini (kurudisha utengano), hivyo serikali ya Mwinyi, Mkapa na JK zote hazina mamlaka moja kwa moja na usambazaji wa Elimu na Afya kwa wananchi isipokuwa kuviwezesha vyombo na asasi mbali mbali kushiriki ktk kusambaza huduma hizi.
Hapa ndipo matatizo yanapoanzia, maana unapokataza Udini ni muhimu zaidi kufikiria utaweza vipi kuwahudumia wananchi wote sawa pasipo kupendelea. Maadam tumeondokana na Ujamaa wa Nyerere, hii dhana ya kujenga Taifa la
Ujamaa na
Kujitegemea wakati tunatumia sera za Kibepari, lazima pia iondoke kwa sababu tumerudisha mamlaka hayo mikononi mwa wananchi na kwa bahati mbaya tumerudisha mfumo wa kikoloni ulowadhalilisha Waislaam kabla ya Uhuru..
Leo tunawawezesha Matajiri wakati Wakulima na Wafanyakazi wakikwazwa halafu mnataka sisi tunamini kuwa nchi hii ni ya Wakulima na wafanyakazi?. Tupeni hesabu ya Wakulima na Wafanyakazi nchini halafu tuone juhudi zinazofanywa kuwaendeleza hapo ndipo tutaweza kupima maendeleo yao. Je ni wakulima na wafanyakazi kiasi gani wametoka ktk umaskini?. Kiasi gani wanategemea kilimo, na wafanyakzi wangapi hawana ajira ktk fani zote mbili. Kujua idadi ya wafanyakazi haina maana unajenga uhasama baina ya wenye kazi na wasiokuwa na kazi ama wafanya biashara, huu ni ujinga mwingine.
Matokeo ya mfumo huu mbovu uliopo, umerudisha Udini nchini na ipo kila sababu ya wananchi kuhesabiwa kwa dini, makabila, jinsia ili vyombo vya kidini na asasi tofauti zipate kuwa na takwimu kamili zitakazo wawezesha kusambaza huduma hizi kw awalengwa. Lazima tukubali yao makabila yanayosahaulika leo tofauti na wakati wa Nyerere na tumeendelea kutumia siasa za Ujamaa na Kujitegemea wakati tukitumia mbinu za kibepari kk maendeleo ya Kiuchumi..
Huwezi kuogopa kuwahesabu Waislaam na Wakristu kwa kuchelea Udini wakati tayari umesha ruhusu Utandawazi na soko huria kama ndizo njia za kukuza Uchumi. Leo shule na Hospital za Wakristu zinashirikiana na serikali kutoa huduma hizi wakati waislaam wameachwa nje, hii inatupa fursa sisi kujiuliza kama we are the minority or second citizen. Huwezi kusimamisha USAWA mahala ambapo hakuna HAKI kwa kutumia UHURU kuficha ukandamizaji wa wazi.
Nitarudia kusema UHURU, HAKI na USAWA ni vitu vinaendana sambamba huwezi kuacha kimojawapo kwa kuchelea matokeo wakati tupo ktk mfumo wa kibepari ambao unawapa nafasi na fursa wananchi wenyewe kusimamia uzalishaji na usambazaji wakati serikali ikijenga sera (policies na mikakati) kuwawezesha wananchi hao kuzalisha na kusambaza kulingana na mahitaji yao. Tusidanganyane, tunaweza kuwa wajinga lakini sii wajinga hivyo!.. Serikali haipeleki maendeleo kwa wananchi moja kwa moja ktk ubepari bali inawawezesha wananchi wake kwa sera na mikakati bora ili wao kujipatia maendeleo na ndio maana inakusanya kodi toka kwa wananchi..