Sensa 2012: Yanayojiri

Sensa 2012: Yanayojiri

boycott census.jpg census foot.jpg

Nimekaa home na bakora na kilemba km ilivyo mila za kiislam; jamaa wa sensa kapita nyumba yangu '' nn tatizo la kunipita ?
 
Una maana gani unaposema kila nchi ina misingi yake? je sensa ya mwanzo baada ya uhuru mbona kipengele cha dini kilikuwepo? tulifata msingi wa nani? na kwanini nyerere alikitoa kipengele hicho mwaka 77? au ndio ilikuwa kwa malengo maalum kama ulivyosema?
Kama kilikuwa na umuhimu wakati ule ndio lazima umuhimu huo uwepo wakati huu?
 
Muache Mungu aitwe Mungu, UK Waislamu wanapewa haki ya kuabudu ikiwemo kubadili matumizi majengo wanayonunuwa, wenye akili fupi wanadhani eti ndio wanaungamiza Ukristo! huu ni upuuzi to the maximum, ndio maana sishangai Wakristo kubanwa na kukosa haki ya kuabudu kwenye nchi za kiislamu, na hiyo ndio ajenda iliyojificha kwenye nchii & we will not allow or tololence this.
Mkuu kwa mgogoro huu ambao baadhi ya wahuni wa kiislam wameuanzisha wasitegemee mafanikio kwenye madai yao yoyote yenye msingi wa kihuni huni kama huu
 
Huo ni upumbafu..mbona hawasimamishi ndege..yaaani hii nchi bana

Nadhan Hii ni sawa kwani safari ya kigoma ni more than one day na Ukiwa unasafiiri unajikuta umeamkia ndani ya Treni Hivyo ni Busara kweli kuwahesabu hapo kwani ndio walikoamkia!! Ila ilitakiwa makarani waendelee kukaa ndani ya treni bila kuwasumbua na wasafiri nao hadi watakapomaliza ndio washuke!!
 
Jamani wadau hebu tushirikiane kufikiri katika hili. Mimi ni miongoni mwa makarani wa sensa hapa Dodoma kata ya K/NDENGE, jana nilipewa madodoso 40 na nikamaliza yote, leo nampigia simu msimamizi ili aniletee madodoso mengine naambiwa niende ofisi ya kata nikachuke, kufika hapo ofisini nakutana na vioja eti,ofisi imefungwa na mwenye ufunguo hayupo, hapo nikakutana na makarani wenzangu wenye tatizo kama langu tukaamua kupiga simu kwa mratibu wa sensa Dodoma mjini ambae anaitwa CHE MPONDA anajibu kwamba, madodoso ndiyo yapo GAIRO yanaletwa kwahiyo tusubiri.Nikajaribu kufuatilia kwa makarani wenzangu kata mbalimbali naambiwa yaani zoezi ni la kisiasa zaidi kwani maandalizi yanaoneka ni ya zimamoto bz hata baadhi ya vifaa vingine kama mabox ya kuhifadhia,sare,penseli 2-HB vichongeo nk havitoshi, halikadharika ramani za EA hazitoshi hivyo nyingine ikabidi zichorwe kwa mkono. Wadau plz tupieni maoni yenu hapa.

Una moyo mtanzania!
 
Una maana gani unaposema kila nchi ina misingi yake? je sensa ya mwanzo baada ya uhuru mbona kipengele cha dini kilikuwepo? tulifata msingi wa nani? na kwanini nyerere alikitoa kipengele hicho mwaka 77? au ndio ilikuwa kwa malengo maalum kama ulivyosema?
Nazungumzia vitu vidogo ambavyo hauhitaji kuingia sana kwenye historia ili uvitambue. Jana nilitoa mfano wa Ujerumani.
Nikasema serikali inakusanya kodi ya kanisa(kirchensteur) kwa wakristu kusaidia kuondesha shughuli za Kanisa. Ni secular lakini kuna vitu vinaashiria imeegemea sana kwenye ukristu.

Nchi nyingi za Europe na zenyewe zipo more or less the same. Zipo baadhi ambazo hadi serikali inalipa mishara ya shule za kidini za wakristu. Nchi nyingi za Europe kunakuwa na public holidays kwenye siku za sherehe za wakristu . Ukienda huko UK yako ndiyo unamkuta malkia akiwa head of the church of England. Kwenye bunge lao house of lords kuna maaskofu n.k.

Ninachosema hapa ni kwamba hizi nchi(siyo zote) pamoja na kwamba zinajiita za kisecular lakini zimeegemea upande Ukristu na kwao ina maana kubwa wanapoweka kipengele cha dini kwa sababu serikali zao zinahusika moja kwa moja kwenye kusaidia kuendesha mambo ya Kanisa. Naomba usiingieze MOU hapa, ni vitu tofauti.

Sisi ni watanzani na ni lazima tuangalie mazingira yetu. Siyo kila kitu wanachofanya nchi zilizoendelea na sisi tuige.
Hivi mkuu wangu, Waislam wanashindwa kutengeneza utaratibu wao wa kujihesabu wenyewe kwenye Misikiti yao?
Hivi hizo data za dini zikiwekwa kwenye sensa ni dini ipi itakubali hizo data?

Kila dini itakayoonekana ina watu pungufu itasema data zimechakachuliwa. Nakuhahakikisha 100% hakutakuwa na kukubaliana na mwisho wake utakuwaje??
Tusiige kila kitu wajameni.
 
Jamani wadau hebu tushirikiane kufikiri katika hili. Mimi ni miongoni mwa makarani wa sensa hapa Dodoma kata ya K/NDENGE, jana nilipewa madodoso 40 na nikamaliza yote, leo nampigia simu msimamizi ili aniletee madodoso mengine naambiwa niende ofisi ya kata nikachuke, kufika hapo ofisini nakutana na vioja eti,ofisi imefungwa na mwenye ufunguo hayupo, hapo nikakutana na makarani wenzangu wenye tatizo kama langu tukaamua kupiga simu kwa mratibu wa sensa Dodoma mjini ambae anaitwa CHE MPONDA anajibu kwamba, madodoso ndiyo yapo GAIRO yanaletwa kwahiyo tusubiri.Nikajaribu kufuatilia kwa makarani wenzangu kata mbalimbali naambiwa yaani zoezi ni la kisiasa zaidi kwani maandalizi yanaoneka ni ya zimamoto bz hata baadhi ya vifaa vingine kama mabox ya kuhifadhia,sare,penseli 2-HB vichongeo nk havitoshi, halikadharika ramani za EA hazitoshi hivyo nyingine ikabidi zichorwe kwa mkono. Wadau plz tupieni maoni yenu hapa.

Bomu hilo linangoja kulipuka....WATU OFISI YA RAIS WAMEGAWANA KAZI YA KUNUNUA VIFAA VYA SENSA ..NA KUACHA MAKAMPUNI YENYE UZOEFU WA SENSA MIAKA YOTE....WAMETUMIA MAKAMPUNI YAO YA MIFUKONI.........HAYA NDIO MATOKEO.....WEWE TANGIA 2010 ....WALISHAPANGA TAREHE YA SENSA ....INAKUWAJE VIFAA VISIFIKE...........

TUNASUBIRI KAMA WAMEWAPA KAZI WAKE ZAO ...,WATOTO WAO ..UTAWASHWA MOTO BUNGENI....NA KESI YA MATUMIZI MABAYA YA BILIONI 120 ZA SENSA ...INANUKIA ..2016!!
 
Phillimoni umenena. haiingii akilini kama tarehe ilishapangwa iweje vifaa visifike kwa muda muafaka? huu ni ufisadi mwingine
 
Nazungumzia vitu vidogo ambavyo hauhitaji kuingia sana kwenye historia ili uvitambue. Jana nilitoa mfano wa Ujerumani.
Nikasema serikali inakusanya kodi ya kanisa(kirchensteur) kwa wakristu kusaidia kuondesha shughuli za Kanisa. Ni secular lakini kuna vitu vinaashiria imeegemea sana kwenye ukristu.

Nchi nyingi za Europe na zenyewe zipo more or less the same. Zipo baadhi ambazo hadi serikali inalipa mishara ya shule za kidini za wakristu. Nchi nyingi za Europe kunakuwa na public holidays kwenye siku za sherehe za wakristu . Ukienda huko UK yako ndiyo unamkuta malkia akiwa head of the church of England. Kwenye bunge lao house of lords kuna maaskofu n.k.

Ninachosema hapa ni kwamba hizi nchi(siyo zote) pamoja na kwamba zinajiita za kisecular lakini zimeegemea upande Ukristu na kwao ina maana kubwa wanapoweka kipengele cha dini kwa sababu serikali zao zinahusika moja kwa moja kwenye kusaidia kuendesha mambo ya Kanisa. Naomba usiingieze MOU hapa, ni vitu tofauti.

Sisi ni watanzani na ni lazima tuangalie mazingira yetu. Siyo kila kitu wanachofanya nchi zilizoendelea na sisi tuige.
Hivi mkuu wangu, Waislam wanashindwa kutengeneza utaratibu wao wa kujihesabu wenyewe kwenye Misikiti yao?
Hivi hizo data za dini zikiwekwa kwenye sensa ni dini ipi itakubali hizo data?

Kila dini itakayoonekana ina watu pungufu itasema data zimechakachuliwa. Nakuhahakikisha 100% hakutakuwa na kukubaliana na mwisho wake utakuwaje??
Tusiige kila kitu wajameni.

Sensa ya mwanzo ya Tanzania huru iliyoungana iifanyika mwaka 1967 na hii ilikuwa ni sensa ya mwisho kuuliza swali la dini. Sensa zilizobaki zilifanyika mwaka 1978, 1988 na 2002. Sensa ya mwaka huu, 2012 itakuwa ni ya saba katika historia ya nchi yetu na ya tano ya Tanzania huru iliyoungana.

Sensa ya mwisho ya Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza katika mwaka 1957 ilionyesha kuwa Tanganyika ina Waislamu 58%, Wakristo 32% na Wapagani 10%. Uwiano kati ya Waislamu na Wakristo ilikuwa ni karibu 2:1 yaani kila penye watu watatu, 2 ni Waislamu na 1 ni mkristo, vile vile unaweza kusema waislamu walikuwa ni karibu mara mbili ya wakristo kiidadi Tanzania.

Mwaka 1967 ndio uliotoa matokeo ya ajabu ambayo mpaka leo sio tu Waislamu bali mtu yoyote aliye na akili timamu ana haki ya kuhoji matokeo hayo. Matokeo haya yalionyesha mgawanyiko wa kidini kama ifuatavyo: WAKRISTO: 33.5% yaani wameongezeka kwa 1.5% kulinganisha na sensa ya 1957. WAISLAMU: 31.4% yaani wamepungua kwa 26.6% katika kipindi cha miaka 10 tu. Hii haikuwahi kutokea sehemu yoyote Duniani iwapo sehemu hiyo haikukabiliwa na janga kama vile vita au jambo lolote lilisababisha idadi kubwa ya watu kufariki. Hata china ambayo imeweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu basi haikuwahi kupungikiwa na watu au kundi fulani la watu katika nchi yao. WAPAGANI: 34.3% yaani wameongezeka kwa 24.3% kwa kipindi cha miaka 10.

Haya nayo ni maajabu, yaani unaweza ukadhani labda Tanzania ina tatizo la Waislamu kuwacha dini yao na kuwa wapagani. Hili nalo halina ushahidi wowote kuwa lilitokea katika kipindi hicho.
 
Hebu lets say Tanzania 100% ni Waislamu so what!? ndio Mahakama ya kadhi ilipiwe kwa kodi zetu? nchi ijiunge na OIC? au watu wote wasilimishwe?
I don't get the point hapa, au ndio yale yale ya Zanzibar Waislamu 99% halafu hawa 1% mnawachomea makanisa? upumbavu mtupu. jengeni vyuo vikuu kwanza ndio Priority ya Waislamu kwa sasa.
 
*Dodoma makarani wakosa vitambulisho, madodoso
*Singida nako wakosa vitendea kazi na kofia
*Dar makarani watishia kugoma, kisa posho
*JK, Dk. Bilal, Maalim Seif, Dk Shein wahesabiwa

SENSA ya Watu na Makazi iliyoanza jana nchini kote, iliingia dosari baada ya kutawaliwa na kasoro mbalimbali. Taarifa zilizopatikana jana kutoka katika maeneo mbalimbali nchini, zilisema baadhi ya makarani hawakuwa na vitendea kazi na hivyo kufanya kazi kwa wasiwasi wakihofia kutoaminika kwa wananchi.

Taarifa zilizopatikana kutoka mkoani Dodoma zinasema kuwa, zoezi hilo la Sensa lilikumbwa na dosari baada ya baadhi ya makarani kulalamika kutopewa vitambulisho.

Mbali na vitambulisho, makarani hao wamedai kuwa na uhaba wa madodoso hali iliyosababisha baadhi yao kupewa madodoso machache.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya makarani hao walisema kuwa, hali hiyo inaweza kusababisha washindwe kufanya kazi hiyo ya kuhesabu watu kwa ufanisi kutokana na kutoaminika kwa baadhi ya wananchi.

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mmoja wa makarani katika Kata ya Hombolo, alisema hadi jana alikuwa hajapata kitambulisho wala fulana za kumtambulisha kuwa yeye ni karani wa Sensa.

“Sasa sijui kama tukienda huko kwenye kuhesabu watu watatuamini na kukubali wahesabiwe au watakataa kwa sababu hatuna vielelezo,” alisema.

Akizungumzia kasoro hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, alikiri kuwepo kwa kasoro hizo.

Alisema kwa upande wa vitambulisho ni kweli vilikuwa havitoshi na kuwa vilitarajiwa kuwasili jana mchana.

“Upo upungufu wa vitambulisho na majaketi ambapo vifaa hivi vilichelewa, lakini vitawasili leo mchana
010812.jpg
(jana),” alisema.
 
Sensa ya mwanzo ya Tanzania huru iliyoungana iifanyika mwaka 1967 na hii ilikuwa ni sensa ya mwisho kuuliza swali la dini. Sensa zilizobaki zilifanyika mwaka 1978, 1988 na 2002. Sensa ya mwaka huu, 2012 itakuwa ni ya saba katika historia ya nchi yetu na ya tano ya Tanzania huru iliyoungana.

Sensa ya mwisho ya Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza katika mwaka 1957 ilionyesha kuwa Tanganyika ina Waislamu 58%, Wakristo 32% na Wapagani 10%. Uwiano kati ya Waislamu na Wakristo ilikuwa ni karibu 2:1 yaani kila penye watu watatu, 2 ni Waislamu na 1 ni mkristo, vile vile unaweza kusema waislamu walikuwa ni karibu mara mbili ya wakristo kiidadi Tanzania.

Mwaka 1967 ndio uliotoa matokeo ya ajabu ambayo mpaka leo sio tu Waislamu bali mtu yoyote aliye na akili timamu ana haki ya kuhoji matokeo hayo. Matokeo haya yalionyesha mgawanyiko wa kidini kama ifuatavyo: WAKRISTO: 33.5% yaani wameongezeka kwa 1.5% kulinganisha na sensa ya 1957. WAISLAMU: 31.4% yaani wamepungua kwa 26.6% katika kipindi cha miaka 10 tu. Hii haikuwahi kutokea sehemu yoyote Duniani iwapo sehemu hiyo haikukabiliwa na janga kama vile vita au jambo lolote lilisababisha idadi kubwa ya watu kufariki. Hata china ambayo imeweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu basi haikuwahi kupungikiwa na watu au kundi fulani la watu katika nchi yao. WAPAGANI: 34.3% yaani wameongezeka kwa 24.3% kwa kipindi cha miaka 10.

Haya nayo ni maajabu, yaani unaweza ukadhani labda Tanzania ina tatizo la Waislamu kuwacha dini yao na kuwa wapagani. Hili nalo halina ushahidi wowote kuwa lilitokea katika kipindi hicho.
Angalia nilipo underline. Nimekuuliza awali hivi kuna dini inaweza kukubali matokeo yatakayoonyesha ina wafuasi pungufu?
 
Watu wawili wa kijiji cha Dosidosi Wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara wanashikiliwa katika kituo cha police iliyopo wilayani hapo kwa kuhamasisha watu kugomea kuhesabiwa.

Kazi kweli ipo!
 
Wanamgambo wa Kiislamu wa Taliban wamewachijna wanawake wa kiislamu kwa kosa la kuhudhuria kwenye muziki huko Kandahar.
Source: DW mchana huu.

My Take: kelele zote hizi ni kutaka kutuletea sheria za kishenzi na kiuwendawazimu kama hawa Waislamu wa Taleban.
 
Angalia nilipo underline. Nimekuuliza awali hivi kuna dini inaweza kukubali matokeo yatakayoonyesha ina wafuasi pungufu?

Jibu ni hakuna na hakuna kwasababu swali lako linajibu kuwa Sensa ya mwisho ya Tanganyika chini ya mkoloni wa Kiingereza katika mwaka 1957 ilionyesha kuwa Tanganyika ina Waislamu 58%, Wakristo 32% na Wapagani 10%. Uwiano kati ya Waislamu na Wakristo ilikuwa ni karibu 2:1 yaani kila penye watu watatu, 2 ni Waislamu na 1 ni mkristo, vile vile unaweza kusema waislamu walikuwa ni karibu mara mbili ya wakristo kiidadi Tanzania.

Sensa ya 1967 ilipokuja na takwimu WAKRISTO: 33.5% yaani wameongezeka kwa 1.5% kulinganisha na sensa ya 1957. WAISLAMU: 31.4% yaani wamepungua kwa 26.6% katika kipindi cha miaka 10 tu. Hii haikuwahi kutokea sehemu yoyote Duniani iwapo sehemu hiyo haikukabiliwa na janga kama vile vita au jambo lolote lilisababisha idadi kubwa ya watu kufariki. Hata china ambayo imeweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu basi haikuwahi kupungikiwa na watu au kundi fulani la watu katika nchi yao!

Swali ambalo lilikuwa likiogopwa kitakwimu ni kwamba laiti sensa ingefichua idadi kubwa ya Waislamu nchini, hoja ya msingi ingekuwa hii; kwa nini kielimu na kimadaraka Waislamu walikuwa wachache?
Wabunifu wa Mfumo uliojengwa kwa misingi ya dhuluma dhidi ya kundi la Waislamu katika jamii ya Watanzania waling’amua kuwa mikakati yao ya kuwapunja Waislamu taaluma na madaraka ingefichuka kirahisi kama sensa ingeonesha idadi kubwa ya Waislamu nchini.
Hivyo, kwa maslahi ya mkakati huo wa dhuluma, ilibidi wafiche Idadi ya makundi ya dini ili umma usije kuhoji mbona katika daftari la sensa Waislamu ndio wengi lakini katika nafasi za elimu, utumishi na madaraka ni wachache?
Wakati vigezo vya sensa vya Umoja wa Mataifa vinajumuisha utambulisho wa dini, Tanzania licha ya kuwa mwanachama wa Umoja huo, ikakiuka utaratibu huo wa kuweka wazi hesabu za watu wa makundi ya dini. Kwa bahati mbaya, mwamko kwa Waislamu ulikuwa bado mdogo au hafifu juu ya ajenda ya kuondosha utambulisho wa dini katika sensa za Kitaifa, hivyo, jambo hilo halikupigiwa sana kelele.
Laiti ingetosha kuwa, Idadi za Watu wa makundi ya dini hazifahamiki kwa sababu hazijumlishwi kupata wastani katika daftari la sensa, huenda kila mmoja angeamini kuwa uamuzi huo ulikuwa wa kizalendo.
Lakini ajabu ambayo imeonekana Kitaifa na Kimataifa ni kwamba, taasisi kadha wa kadha zimekuwa zikitoa au kutumia takwimu zinazoonesha kuwa kundi la Wakristo ndilo linalounda jamii kubwa ya Watanzania likifuatiwa na lile la Waislamu!
Hiyo ni kusudi ya wabunifu au tuseme waasisi wa mfumo kandamizi uliohujumu nafasi ya Waislamu kielimu na kiutumishi katika nyadhifa za juu na madaraka. Kwa nini walifanya kusudi hiyo? Kwa sababu walitaka jamii na dunia iamini kuwa uchache wa Waislamu katika maeneo hayo ni matokeo ya uchache wa idadi ya jumla!
 
Back
Top Bottom