Sensa 2012: Yanayojiri

Sensa 2012: Yanayojiri

wakuu jf,
nimetoka kuhesabiwa sasa hivi. nina furaha sana. karani kanambia hakupata matatizo yoyote huku mbezi morogoro rd na mimi nimekuwa ni mtu wa mwisho ktk eneo letu. kaweka tick mlangoni kanambia anapeleka makabrasha nyumbani kwake halafu huyooooooooo CHIKAS PUB mbezi luisi akale bata. vipi mwananyamala na tandika hukooooooo?
 
Mtaani kwetu yamejaa mabango ya(mimi muislam sihesabiwi) hivyo makarani wanapita tuu...cjui itakuwaje?
 
Kuna karani mmoja rafiki yangu yeye kapangiwa Mwananyamala Kisiwani ananiambia mpaka saa 9 kaishahesabu nyumba 12 tu kila nyumba akiingia anakutana na upinzani mkali watu hawataki kuhesabiwa.

Mkuu, hii kitu imekuwa serious sana, mm kuna kijana nimekutana nae nikamuuliza umeishahesabiwa, Akaniambia sina muda huo, anadai hata UN wanataka kipengele cha dini kiwepo, sasa anasema haoni faida ya kuhesabiwa bila kujua dini yake, na pia anadai hata kama wakiwakamata watawapeleka wapi wakati Magereza hayatoshi? Nimefadhaika sana!
 
Mtaani kwetu yamejaa mabango ya(mimi muislam sihesabiwi) hivyo makarani wanapita tuu...cjui itakuwaje?

Mtz. Mzalendo, nina wasiwasi data zitakuwa siyo sahihi, kiukweli watu wengi sana wamegoma kuhesabiwa, ni hatareeee!
 
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni. Kuna mtu katembelewa na karani wa sensa na akawajuza wadau wake kwamba yule karani aidha ana uwezo mdogo sana wa kusoma na imechukua saa nne kukamilisha mahaojiano!!! Kwa spidi hii ya saa tatu kaya moja si katika siku moja (12 day light hours) karani huyu atapitia kaya tatu tu, na kwa mtaa aliopangiwa karani kama huyu atachukua miezi miwili kumaliza. Sijui ndiyo laana ya kuwaacha waalimu, au huyu karani alikuwa anategea lunch ya dezo maana labda hajalipwa posho ya kazi.

Ha ha haaaaa, huyo kweli alikuwa na lake, mbona inachukuwa dakika chache sana, na pia , maswali yapo straight sana na mafupi?
 
Ni takriban dakika 10 zilizopita nimekuwa na ugeni nyumbani kwangu wa karani wa sensa na imenichukua kama dakika 7 au 8 hivi kukamilisha zoezi zima la kuhesbiwa. Maswali aliyouliza ni watu wangapi wamelala kwenye nyumba usiku wa kuamkia leo, umri wa kila mmoja, elimu yao, je mko katika mfuko wa hifadhi ya jamii au bima ya afya, kuna mlemavu yeyote katika familia, kuna kifo chochote kimetokea kati ya mwaka jana na sasa, kuna ndugu yeyote yuko nje ya nchi? Ni hayo tu, nawasihi wale wanaoogopa na kuhofia mambo kibao wasifanye hivyo maana ni very interesting. I suggest tuwape ushirikiano makarani wa sensa maana takwimu hizi zitatumika kwa miaka 10 mbele hivyo ni muhimu sana. I wish you all the best, week end njema!

Escobar: nimekupa LIKE mkuu, kitufe cha like sikioni, Nimepapenda hapo, kwenye red, kumbe nimeshahesabiwa nami, huku niliko.
 
Wakuu,

Naisikitikia sana nchi yangu Tanzania. Raia tumeanza kuongea lugha tofauti kama wajenzi wa mnara wa babeli.
Yatupasa kuchukua hatua kurekebisha hali hii, wananchi waipende nchi yao, wajivunie utanzania wao, wakisikia kuna sensa wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa. Tumekosea wapi? Tuliowapa madaraka ya kutuongoza hawaoni tatizo?
Ingewezekana kabisa kufanya sensa, vitambulisho vya taifa na daftari la kudumu la wapiga kura kama zoezi moja, na tungeokoa pesa nyingi za watanzania ambazo zingetumika katika shughuli nyingine za maendeleo, tuliowapa madaraka ya kutuamulia hawawezi kuliona hili.
Hata hivyo nitarudi nyumbani kesho jioni, (unless nipate tatizo la flight connection), na ikiwezekana nitahesabiwa. Siyo safari maalum kwa ajili ya sensa ( is just a coincidence)!
Ni muhimu sana tukajua idadi yetu na uwezo wetu katika nyanja muhimu ili tuweze kupambana na changamoto za maisha ya hapa duniani.
 
Nijuavyo mimi sensa itaendelea through 7days. Sasa kisa cha kuwasimamisha abiria ninini? Na wewe umekubaliana na jambo hilo?
Ungekuwa uchaguzi ningeelewa.

mkuu Paka Jimmy ni kuwa pamoja na kuwa sensa itaendelea kwa siku hizo saba tarehe rasmi ni ter.26 usiku na data zinapatikana kwa kujua siku hiyo tar 26 ni watu wangapi walilala kwenye kaya hivyo hata makarani wa sensa wakifika tar.29 wakamkuta mtu ambaye hakulala kwenye kaya husika tarehe hiyo hawatamwesabu
 
Hapa kwangu wameshapita kuhesabu ingawa sikuwepo, waliokuwepo wametoa taarifa zote zinazohitajiwa.
Nimeshangaa saa moja iliyopita nimeshuhudia msafara wa magari sita, mawili ni pick ups za polisi; moja imesheheni Polisi lingine liko tupu. Sijajua kilichosababisha hali hiyo maana ktk jirani zangu sioni hata mmoja mwenye ule msimamo wa 'sitahesabiwa'.
 
Nimeamka asubuhi nikaanda chai kwa mhesabuji lakini hakutokea. Nimeanda chakula cha mchana na soda hadi saa hii hajatokea. Sasa sijui na kesho nijiandae tena maana serika ilisema tujiandae kwa sensa
 
Mpaka sasa, idadi kubwa ya waislamu wamegoma laivu bila kujificha. Msikubali kudanganywa. Watu wengi nilio ongea nao wameniambia wamekataa kuandikishwa. Nimeaongea na mwandishi mmoja wa sensa akaniambia hali ni tete serekali imekula hasara kwa kiburi chao. Tunasubiri mswada bungeni wa kutokua na imani na rahisi. Tuchague raisi mwengine.
 
Wakuu,

Naisikitikia sana nchi yangu Tanzania. Raia tumeanza kuongea lugha tofauti kama wajenzi wa mnara wa babeli.
Yatupasa kuchukua hatua kurekebisha hali hii, wananchi waipende nchi yao, wajivunie utanzania wao, wakisikia kuna sensa wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa. Tumekosea wapi? Tuliowapa madaraka ya kutuongoza hawaoni tatizo?
Ingewezekana kabisa kufanya sensa, vitambulisho vya taifa na daftari la kudumu la wapiga kura kama zoezi moja, na tungeokoa pesa nyingi za watanzania ambazo zingetumika katika shughuli nyingine za maendeleo, tuliowapa madaraka ya kutuamulia hawawezi kuliona hili.
Hata hivyo nitarudi nyumbani kesho jioni, (unless nipate tatizo la flight connection), na ikiwezekana nitahesabiwa. Siyo safari maalum kwa ajili ya sensa ( is just a coincidence)!
Ni muhimu sana tukajua idadi yetu na uwezo wetu katika nyanja muhimu ili tuweze kupambana na changamoto za maisha ya hapa duniani.

kwa wanayo yafanya viongozi hawa wa ccm hakuna mwenye moyo na nchi yake......
kwa jina la mwenyezi mungu sijawaona hao watu wa sensa wala hata kwa mbali na nipo mjini
 
Serikali na vibaraka wake hawawezi kulazimisha wananchi kufanya sensa ambayo haina malengo ya kupanga na kuchagua ni maendeleo gani yanayotakiwa kwa Watanzania wote. Hata muuza nyanya sokoni anajua fika ana vitunguu vingapi, machungwa mangapi, ndizi, mananasi na mapapai vibichi, vilivyo sana, japokuwa manunuzi na mauzo ya vitu vyote hivi huingia mfumo mmoja..

Huwezi kuhesabu watu kama kitu kimoja na ukatumia neno SENSA.. hili neno ni zito zaidi ya fikra zozote za kibaguzi ama utengano ni fikra za KUFIKIRIANA na KUTEGEMEANA bila kujali tofauti zetu kabisa. Huwezi kupanga maendeleo ya Ukerewe pasipo kuanza na ujenzi wa ramani ya mji (blue print) na ktk ramani hiyo haiwezi kubeba tu idadi ya watu wake..blue priint inakuw ana taarifa zote za mahitaji ya mji huo kutokana na watu na mazingira yake. Huwezi kutenga maeneo ya kujenga misikiti 10 Ukerewe wakati ukweli ni kwamba kuna asilimia 2 tu ya waislaam kati ya wakazi wake! vivyo hivyo sehemu nyinginezo na kwa dini na madhehebu mengine asasi zake wanahitaji takwimu hizi kujiandaa na huduma zao wakiwa wadau na asasi za kijamii zinazoshiriki ktk sensa hii.

Sio kila kitu kinafanywa na serikali isipokuwa serikali inaandaa policies kuwezesha wananchi kujipatia maendeleo. Ardhi ndio utajiri mkubwa wa Mtanzania iwe uzalishaji wa viwanda, kilimo au ufugaji ni muhimu kuelewa wananchi wake ni ktk makundi yapi ili kuandaa sehemu zao muhimu ktk uzalishaji na usambazaji. Haiwezekani tukahesabiwa kama machungwa sokoni mkafikiria kwamba tunajenga, hii dhana itatumika tu kama tulikuwa na Udini na hivyo tunahofia ukweli kuonekana.

Kama Tanzania hakuna udini hakuna sababu kabisa ya kuogopa maana tunahesabiwa wote. Kukataa kuweka kipengele hiki inadhihirisha wazi kuna kitu kinafichwa na hofu yenu ni ukweli utakao bainika..Sawa na mke wanapotoa hoja ya kuongeza kipengele cha kupimwa Ukimwi ktk physical check up yenu ya mwaka. Mume unakataa na kusema tupime tu afya zetu inatosha, hilo la tukipima Ukimwi itaharibu mahusiano yetu!..Mahusiano yataharibika vipi ikiwa huna shaka ya mmoja wetu kuwa na Ukimwi?. Hivi kweli mtu anapotoa hoja ya kupima Ukimwi huwa ana nia ya kujenga chuki au ni jambo bora kwenu wote kiafya.

Kitendo cha kuondoa dini kupachikwa kwamba ni agenda ya Waislaam, hizi ni propaganda tulizozisikia hata wakati tunadai Uhuru wetu miaka ya 50s. Wakoloni wakiwatumia makanisa na baadhi ya Wakristu walieneza uongo ktk harakati za waislaam kudai Uhuru ati wakati nchi yenyewe haiko tayari. Wakatugawa hadi makundi ya kina Marealle na Fundikila ili mradi kusiwepo na Umoja lakini mwisho wa siku kwa kutumia busara za waasisi wa chama chetu TANU tuliweza kuvuka na kushinda ya firauni. Siku zote Uislaam ni kusimamia haki ya wananachi wake na tunaposema wananchi wote wahesabiwe kwa kuweka vifungu vya tofauti zao haimaanishi tunataka kujua Waislaam ni wangapi isipokuwa ndio njia halali ya kujua WATU wako na ktk MAZINGIRA yapi ili ituwezeshe tupange mipango yenye taarifa za kweli na zote sio nusu nusu..

Kuna umuhimu mkubwa wa kujua kuna watoto, vijana na wazee wanaokaribia kustaafu kiasi gani, hii haina maana tunawatenga wazee au watoto. Tuna wanawake kiasi gani, Na wala sii vibaya kujua Wakerewe kama kabila lina watu kiasi gani (pengine tunaisha na kupotea) hivyo mila na desturi zetu zipo hatarini, taarifa za uhamiaji wao nje ya kisiwa cha Ukerewe kama nilivyo na shauku ya kujua kuna Wazanzibara wangapi Tanganyika au Wabara waliohamia Zanzibar. Umuhimu wa kujua hivyo upo sana tu na ndio nadhani leo tunaweza kuwa na majibu sahihi ya hizi kero za muungano..Hii haina maana italeta chuki na uhasama isipokuwa ukweli utawezesha ujenzi bora wa taifa kwa kuelewa tamwimu hizi badala ya kuogopa yasiyokuwepo.Haijawahi kutokea ktk historia ya dunia hii wananchi kuanza chuki kutokana na taarifa za sensa, huu ni uzushi mtupu..

Hakuna kitu hicho na wala hakipo isipokuwa ni fear factor inayotumiwa na baadhi ya wadau hasa wa huo mfumo Kristu kutishia watu na kwa faida zao wenyewe.. Kipengele cha DINI, KABILA, JINSIA, UZAWA, WAGENI WAHAMIAJI, UMRI, KAZI ama AJIRA, ELIMU na kadhalika hivi vyote kwa pamoja vinahitajiwa sana ktk kutafuta solution ya matatizo ya Watanzania. Tusitafute wachawi wakati sisi wenyewe ndio wachawi tulofundishwa kuchukia watu wengine hata kama jambo hilo ni kwa faida yetu sote..
 
Serikali sikivu...sasa subiri spin doctors waingie kazini kufanya vitu vyao....tusitegemee kabisa kusikia kauli, "Zoezi la kuhesabu watu nchini halikufanikiwa."

Mpaka sasa, idadi kubwa ya waislamu wamegoma laivu bila kujificha. Msikubali kudanganywa. Watu wengi nilio ongea nao wameniambia wamekataa kuandikishwa. Nimeaongea na mwandishi mmoja wa sensa akaniambia hali ni tete serekali imekula hasara kwa kiburi chao. Tunasubiri mswada bungeni wa kutokua na imani na rahisi. Tuchague raisi mwengine.
 
Eh,,,,,,,wamekataaaaa,,,wamakataaaaje????aaaaaa,wamekataaaa Kuhesabiwaaaaa
 
Back
Top Bottom