888I
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 472
- 581
Wadau,
Tuna msemo maarufu: "Namba Hazidanganyi." Kwenye nchi yoyote, takwimu (data) ndiyo msingi wa uhalali (legitimacy). Lakini ukiangalia Takwimu za Uchaguzi wa Oktoba 2025 na Takwimu za Watu (Sensa 2022) na Hali ya Mtaani (MO29, D9), nabaki na swali:
Je, Tanzania tumeamua kukanusha Sayansi ya Hesabu?
Hebu tulinganishe namba tatu muhimu ambazo zinaleta utata mkubwa:
Utata Mkuu: Kura Milioni 30+ kutoka kwenye jumla ya wapigakura wanaofaa Milioni 35-37 ina maana kuwa asilimia kubwa sana ya Watanzania wenye sifa ya kupiga kura walijitokeza na kumpigia kura mgombea mmoja!

1. Takwimu ya Watu (Sensa) vs Takwimu ya Kura
- Sensa ya Watu (2022): Tanzania Bara na Visiwani tulikuwa na jumla ya Watu wapatao Milioni 61.7.
- Makadirio ya Wapiga Kura: Kwa kuzingatia umri wa kupiga kura (miaka 18 na zaidi), idadi ya wananchi wanaofaa kupiga kura inakadiriwa kuwa kati ya Milioni 35 - 37 tu.
- Kura za Samia (Uchaguzi 2025): Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ilitangaza kwamba Rais Samia alipata kura zaidi ya Milioni 30 (karibu 98% ya kura zote halali).
Utata Mkuu: Kura Milioni 30+ kutoka kwenye jumla ya wapigakura wanaofaa Milioni 35-37 ina maana kuwa asilimia kubwa sana ya Watanzania wenye sifa ya kupiga kura walijitokeza na kumpigia kura mgombea mmoja!
2. Upendo wa Mtaani (Kura) vs Ukweli wa Maisha
Kama kweli Rais amechaguliwa na kura Milioni 30+, ambazo ni karibu Nusu ya idadi yote ya Watanzania (Wazee, Watoto, Vijana), tungetegemea Nini?:- Mitandaoni (Online Presence): Mitandao ya kijamii (X, IG, FB na Hapa JF) ingetawaliwa na maneno ya kumpongeza na kumuunga mkono Rais, kwa kuwa vijana wengi wangekuwa wamempigia kura. Badala yake, mitandaoni kuna Malalamiko mengi ya wazi na lugha ya kejeli dhidi ya uchaguzi na utawala.
- Mtaani (Street Reality): Mtu anayependwa na Mil 30+ kwenye taifa lenye ujumla ya watu 70+Mil asingehitaji Wanajeshi na Polisi kufunga miji ili kulinda sherehe yake ya Uhuru (D9). Viongozi wenye kura hizi huandamaniwa kwa hiari, siyo kwa woga.
3. Hitimisho: Namba Hazidanganyi, Lakini Zimepindishwa
Namba hazina uwezo wa kudanganya, bali wanadamu ndiyo hupindisha namba kwa maslahi yao.- Kama kweli asilimia kubwa ya Watanzania wako nyuma ya Serikali kwa mujibu wa sanduku la kura, basi Serikali haihitaji kutumia nguvu, vitisho, wala kuzima intaneti,kufunga comments kusikilizwa.
- Hali ya sasa, ambapo kuna vifo, mauaji (Oktoba 29), na kutengwa kimataifa (Azimio la EU) dhidi ya ushindi wa "kura za kihistoria," inathibitisha kuwa namba zilizotangazwa zimepoteza uhusiano wake na ukweli wa maisha ya Watanzania.