*dodoma makarani wakosa vitambulisho, madodoso
*singida nako wakosa vitendea kazi na kofia
*dar makarani watishia kugoma, kisa posho
*jk, dk. Bilal, maalim seif, dk shein wahesabiwa
sensa ya watu na makazi iliyoanza jana nchini kote, iliingia dosari baada ya kutawaliwa na kasoro mbalimbali. Taarifa zilizopatikana jana kutoka katika maeneo mbalimbali nchini, zilisema baadhi ya makarani hawakuwa na vitendea kazi na hivyo kufanya kazi kwa wasiwasi wakihofia kutoaminika kwa wananchi.
Taarifa zilizopatikana kutoka mkoani dodoma zinasema kuwa, zoezi hilo la sensa lilikumbwa na dosari baada ya baadhi ya makarani kulalamika kutopewa vitambulisho.
Mbali na vitambulisho, makarani hao wamedai kuwa na uhaba wa madodoso hali iliyosababisha baadhi yao kupewa madodoso machache.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya makarani hao walisema kuwa, hali hiyo inaweza kusababisha washindwe kufanya kazi hiyo ya kuhesabu watu kwa ufanisi kutokana na kutoaminika kwa baadhi ya wananchi.
Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mmoja wa makarani katika kata ya hombolo, alisema hadi jana alikuwa hajapata kitambulisho wala fulana za kumtambulisha kuwa yeye ni karani wa sensa.
sasa sijui kama tukienda huko kwenye kuhesabu watu watatuamini na kukubali wahesabiwe au watakataa kwa sababu hatuna vielelezo, alisema.
Akizungumzia kasoro hizo, mkuu wa mkoa wa dodoma, dk. Rehema nchimbi, alikiri kuwepo kwa kasoro hizo.
Alisema kwa upande wa vitambulisho ni kweli vilikuwa havitoshi na kuwa vilitarajiwa kuwasili jana mchana.
upo upungufu wa vitambulisho na majaketi ambapo vifaa hivi vilichelewa, lakini vitawasili leo mchana
(jana), alisema.