Ni punde Raisi wetu katoka kuelezea umuhimu wa sensa na kuwaomba na kuhimiza watu wahesabiwe. Ila kuna jambo moja kwa upande wangu sijamuelewa vizuri. kaulizwa swali na waandishi wa habari Je, watafanya nini kwa wanaosambaza sms kushawishi watu wasihesabiwe, jibu alilotoa ni rahisi kweli kwa hadhi yake, kasema "nasi tunatuma sms kuwashawishi wakubali kuhesabiwa, tutapambana nao hukohuko kwenye mitandao, tena zinatumwa kwa jina langu (raisi)" kiukweli pamoja na maelezo kuwa hao waliopo msikitini si watatoka tuu kama wamejifungia na wakitoka watahesabiwa. Binafsi naona kama kunamchezo wa kuigiza, kama kweli sheria ya uchaguzi inaelekeza nini cha kufanya kwa waliokiuka hili zoezi si muda wa kubembelezana. Kubembelezana sana huku kwa mambo ya msingi yanapoteza muda na kuchelewesha maamuzi ya msingi! NAPENDEKEZA HATUA KALI ZICHUKULIWE KWA WOTE WALIPOKIUKA WAZIWAZI.
MIMI NIMESHAHESABIWA, NAKUSHAURI NAWE UWE TAYARI KUHESABIWA!