Sensa 2012: Yanayojiri

Sensa 2012: Yanayojiri

Endeleeni kuwachagua hao ma RAHISI wenu ndo maana hii nchi haiendelei..
 
Mimi na familia yangu si wa-isilamu lakini hatujaesabiwa, nimekaa nyumbani mpaka nimechoka sasa: Ngoja niende mitaani kucheki mechi.
tabata in Dar es salaam
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Katavi, mimi nipo safarini kikazi na wamekuja hoteli saa 8 usiku wakitaka wote tubesabiwe na waingie vyumbani wakati wahudumu Wa hoteli walipatiwa form kuandikisha waliolala hapo siku leo. Duh!!!

Dah....!! Sasa wale waliokuwa na madada poa ilikuwaje? Nao wanahesabiwa??
 
Hapa mtaani wapo waliogoma na wameambia waende kwa mjumbe jioni kutoa maelezo.
 
zoezi Dar limefeli kabisa waislam wengi bado wamesimamia msimamo wao wa kutohesabiwa, nimepita misikitini nimekuta watu wengi wakiendelea na ibada kwa siku saba, mfano kata ya magomeni nyumba zilizoandikwa ni 30 kwa mujibu wa karani wa sensa nyumba nyingi hawataki kuandikishwa.
 
Aisee hao watu wa sensa wako wapi? sijaona mtu mpaka muda huu; ina maana nimelazimishwa kugoma kutokuesabiwa!!!!!!!!
 
Mpaka sasa, idadi kubwa ya waislamu wamegoma laivu bila kujificha. Msikubali kudanganywa. Watu wengi nilio ongea nao wameniambia wamekataa kuandikishwa. Nimeaongea na mwandishi mmoja wa sensa akaniambia hali ni tete serekali imekula hasara kwa kiburi chao. Tunasubiri mswada bungeni wa kutokua na imani na rahisi. Tuchague raisi mwengine.
Zoezi ndiyo limeanza leo. Vuta subira...
 
Ni nani aliyekupa mamlaka ya kutuongelea wakazi wa Dar? mimi na Familia yangu tumeshahesabiwa tena utamu wenyewe na karani wa sensa ni mwislamu na nyumba za jirani zangu ni waislamu. unadhani utamdanganya nani hapa JF. uliona Elimu ghari sasa umejaribu ujinga angalia ulivyo ghali zaidi.
 
MZIMU una uhakika na taarifa yako?!
mtaani kwetu ni wengi waislam na wamekubali kuhesabiwa!

hao wanogoma ni wajinga wanaofuata mkumbo!
 
Last edited by a moderator:
Serikali ndo itaona raha na umuhimu wa ubabe badala ya utoaji wa elimu
 
Mie najiandaa kubandika bango langu la "Nyumba hii ni ya waislam hatuhesabiwi" ili huyo kalani wenu asijisumbue kufika hata uwani kwangu.

Mgomo wa kuhesabiwa uko pale pale!.. Baadhi ya waislam hawatoi ushirikiano wowote kwa mawakala!.. Hali hii nimeiona leo ktk eneo la changanyikeni... na kusikia baadhi yao wakitamka kwamba hawatahesabiwa. Tutegemee kusikia hili kwenye taarifa ya habari!.........
 
Wilaya mpya ya buhigwe hawaja anza sensa siku ya leo trh 26 tatizo hawa pata vifaa ikiwemo tshert vitambulisho pamoja na fedha za kazi kwa. kasulu watu wamepokea vizur swala la sensa lakn makaran hawana sare na baadh ya vifaa
*my take*
sensa vip nchi imeshindwa
source jamaa yangu karan
 
Kwani zoezi la sensa linamalizika lini?? mi najua kuhesabu watu ni siku moja au????
Linamalizika siku saba. Mimi nmeshahesabiwa ila kuna jirani zangu wengine hawajahesabiwa kwa sababu walikuwa hawapo. Ila jamaa wamesema watarudi tena. Ndiyo maana nasema tuvute subira...
 
Tatizo elimu ni duni.mm na zani kama wangekuwa wameelimika nazani wasinge goma kwani niwaulize wezangu sensa ngapi zimepita na wamehesabiwa leo ndio wagome. Haaaaaaaa kuna kitu kimejificha tu
 
Nimesubiri kuhesabiwa tangu asubuhi hapa Mbezi beach mpaka mida hii hakuna cha karani wala mjube kapita,sasa najiuliza kama wasipokuja leo itakuwaje maana mimi na mume wangu ni watu wa kuhangaika na tukitoka wote kunabaki mlinzi?
 
Back
Top Bottom