Kuna msichana mmoja alinipiga ngumi, sijui ni ngumi ile sijui ni kitu gani, alinipiga usoni miwani ikavunjika, daaahhh, aisee nilikunja ngumi kwanza iliyoshiba, nikaivuta nyuma huku nimemshika nguo kifuani, yaani nilivuta ile ngumi iliishia hewani anaiangalia sikumpiga, huku nikiwa na hasira sana, niliondoka machozi yakinilenga kwa ile hasira.
Kuna wanawake huwa wanajaribu kukufanya uwapige au uwatukane muanze kutukanana na hii inasababishwa na baadhi yao wanatokea kwenye mahusiano ya namna hii, unakuta watu waliokuwa nae au familia anayotokea kuna mambo hayo.
niliondoka hatukuonana kwa siku kama 4, hakuwahi kunitukana wala kujaribu kunipiga, nilimfundisha mapenzi sio ngumi wala kutukanana..
Mkuu we acha tu mahusiano yapo very complicated usizungumzie upande mmoja tu.