Selfika na JF: Snap it. Show it


Tulia mama kula maisha...

Mumeo yupo atakuja kwa wakati Mungu aliopanga...
 
Ukiacha watu wakupangie cha kufanya kwenye maisha utajikuta unaingia pabaya, kwenye ndoa hamna kuwahi wala kuchelewa muda ukifika utaingia tu...

Na ukiwa desperate unaweza usiolewe au ukapata mtu ambaye si sahihi ..

Oh yeah ndoa haihitaji haraka ..
Binadamu hawawezi kuacha kuongea kabisa .
Binafsi sina haraka ndo kwanza sina habari wacha tu waongee .
 

Umemaliza...

Barikiwa sana..
 
Mimi ni mvivu sana kutembea.
Kwahiyo sijulikani sana...ila hata nikitoka, Kwa wanaonijua sidhani kama wanaweza kuuliza maana nipo siriazi mno



Kazi unayo

Anha sawa
Mimi natembea ila si sana halafu mimi rahisi kuongea na watu hivyo ukinianza tu lazima nikujibu hahaha .. I enjoy mingling muda mwingine .
Ukauzu naufanya mtaani huku napoishi ila ukinikuta nje huko naongea huyo
 

Kuchagua lazima uchague sio kila mwanaume anafaa kuwa baba wa familia...
 
Ukiacha watu wakupangie cha kufanya kwenye maisha utajikuta unaingia pabaya, kwenye ndoa hamna kuwahi wala kuchelewa muda ukifika utaingia tu...

Na ukiwa desperate unaweza usiolewe au ukapata mtu ambaye si sahihi ..
Kuna work Mate mmoja bana alilazimisha ndoa wakafunga ya serikali na aliyemuita mumewe...
Ilikua 2016 kaona madam A ameshaolewa B ameshaolewa C ameshaolewa...akamwambia mtu wake nimebaki madam Mimi tu staff akafosi kamlazimisha mwanaume aliekuwa nae kipindi hiko nae alikua mwalimu mwenzie mpaka wakaenda kufunga ya serikali ilimradi tu asibaki madam pekeake ambae hajaolewa Wakafunga. Balaa likaanza ikawa ni visa na vituko tu humo ndani ikafikia pahala likizo kila mmoja anaenda anakojua yeye na hakuna kuulizana wala kumaindi mwenzio likizo ikiisha wanarudi wanaendelea na drama ndoani...
Ikafikia hatua kila mmoja akawa analala chumba chake hali ikawa mbaya zaidi mwanaume akawa analeta wanawake humohumo ndani kwenye chumba chake.
Mbona mwanamke aliomba uhamisho ghafla bila kutaka. mpaka leo wana hiko cheti cha serikali hawajaenda kuvunja ndoa ila kila mmoja anaendelea na mahusiano mengine huko aliko!!
Halafu alikua yule mtu wa show off masaa yote ofisini ni "Mimi me wangu Mimi mme wangu.. mimi na mme wangu Mimi na mme wangu utadhani wengine hawana waume au hawajaoa na kuolewa!!!! Mbaya zaidi sijui tuseme mwanaume hakumpenda au sijui hata tusemeje.
Mtu mmeamua kufunga ndoa nyie kama nyie wawili badae wewe mwanamke ukampeleka mumeo kumtambulisha kwenu wanamtambua ila yeye mwanaume hana hata dalili ya kukupeleka kwao ukiuliza utanipeleka lini unajibiwa acha kiherehere cha kutaka kujulikana hapo mwanaume huyo ana watoto wawili alishazaa na wanawake wawili tofauti huko Nyuma kabla hawajakutana na baadhi ya likizo eti anaendaga huko kusalimia watoto zake anakaa likizo nzima ikiisha anarudi kwako !! Mshahara wote hana habari za kupanga maendeleo nawewe ndiokwanza anaangalia watoto wake wewe unabaki tu kulia nanafsi yako! Alihama bila kupenda mbona!
 
Maskini pole zake madam. Ndoa sio jambo la kukurupuka wala kulazimisha inatakiwa itokee wote mmeridhiana kuingia huko.
 
Maskini pole zake madam. Ndoa sio jambo la kukurupuka wala kulazimisha inatakiwa itokee wote mmeridhiana kuingia huko.
Alivyokuwa muongeaji sasa!!!! Ni Yule wa kuwananga wenzie yani aibu ilikua yake mbona sasahivi tangu ahame ameshatutambulisha wanaume kama watatu hivi mwezi huu unatambulishwa huyu mwezie ujao yule.... kiukweli ndoa sio mchezo sio suala la kukurupukia ndoa zina mengi mno!
 
Kabisa na usiolewe sababu fulani kaolewa au nawaona wenzangu angalia nafsi yako pia Omba Mungu akupe kulingana na hitaji la moyo wako bila hivo hutoboi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…