Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,582
- 1,105,383
1. Mfumo dume. Bado umetamalaki. Ndiyo maana mwanaume anaoa...na mwanamke anaolewa. Na bahati nzuri/mbaya kitakwimu waolewaji ni wengi kuliko waoaji...yeah kwa utaratibu sahihi... Lakini changamoto ya umri pia itawatesa sana wanawake na jamii sijui kwanini huwa inawachukulia tofauti wanawake ambao umri umeenda ila hajaolewa tofauti na mwanaume ambae umri umeenda ila hajaoa... Hivi Kwanini??
2. Kibayolojia. Mwanaume anaweza "kuzaa" wakati wo wote hata kama ana miaka 80 kama bado mitambo yake ya nyuklia inafanya kazi. Kwa hivyo presha kwake siyo kubwa kivile. Mwanamke yeye ana kikomo cha muda japo anaweza kuzaa hata mpaka akiwa na miaka 45+ - hasa kwenye nchi za wenzetu huko ambako kuna huduma bora za afya. Inashauriwa sana kuwa mwanamke apate mtoto wa kwanza kabla hajavuka 35 kwa sababu baada ya hapo viishu vya hapa na pale kuhusu uzazi vinaanza kujichanuza. Miaka 35 kwa mwanaume ndiyo muda sahihi pia wa kutulia na kuanzisha familia lakini ndo kwanza utawakuta mabro bado wanagawa dozi mtaani. Ukimuuliza kuhusu ndoa utasikia bado najipanga kaka...na hakuna anayemshangaa.
3. Jamii yetu bado inafungamanisha heshima na mafanikio ya mwanamke na ndoa...na watoto. Naamini hali hii itabadilika kwa kadri jamii inavyopiga hatua za kimaendeleo. Mfano; Marekani sasa karibia nusu ya wanawake hawataki kuolewa na hata wanaoolewa zaidi ya nusu wanaishia kwenye talaka....na wengine hawataki watoto kabisa hata kama wakiolewa. Hawa wana vigezo vingine vya kupimia heshima na mafanikio ya mwanamke; na ndoa na kuwa na watoto siyo vigezo vyao vikuu.



