Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Watu hudhan tunachagua 😔😔😔😔, lkn huweza vaa kiatu n kiatu et kisa unashda na kiatu. Yapasa upate kiatu saiz yako ili kiskubane njian ukakivua ukaanza tembea peku, ndoa n safar ndefu kabla ya kuianza yapasa kujipanga haswa usje kuishia njiani.

Hatuchagui bali tunasubir sahh kwa wakati sahhi 😊😊😉.......
Uchaguzi ukizidi sana nalo ni janga
 
Watu hudhan tunachagua , lkn huweza vaa kiatu n kiatu et kisa unashda na kiatu. Yapasa upate kiatu saiz yako ili kiskubane njian ukakivua ukaanza tembea peku, ndoa n safar ndefu kabla ya kuianza yapasa kujipanga haswa usje kuishia njiani.

Hatuchagui bali tunasubir sahh kwa wakati sahhi .......

Well said sissy , Asante kwa mchango wako
Hakuna kuchagua wala nini , mambo mengine yanahitaji subira .. sio baadae mbeleni uanze kulalamika nilikuwa nawahi wapi .

Ndoa sio lelemama ....
 
Selfika

20220421_094628.jpg
 
Ila hawa watu wanao pressurize ndoa jamani
Mtu haumfahamu lakini anavyokujibu sasa
" Bado hujaolewa eeh , wewe endelea kuchagua tu , utazeekea nyumbani " .
Haya maneno yanaumiza sana aisee .
Hivi ni kwa nini? juzi juzi hapa kuna classmate wangu nilikutana nae ktk stori ananiambia kaolewa na ana watoto wawili mimi vipi nikamuambia sijaolewa wala sina mtoto akaanza kunisema tatizo nachagua sana imagine ni mwanamke mwenzangu ananisema hivyo. Sijui hii kitu inasababishwa na nini nachukia.
 
Hivi ni kwa nini? juzi juzi hapa kuna classmate wangu nilikutana nae ktk stori ananiambia kaolewa na ana watoto wawili mimi vipi nikamuambia sijaolewa wala sina mtoto akaanza kunisema tatizo nachagua sana imagine ni mwanamke mwenzangu ananisema hivyo. Sijui hii kitu inasababishwa na nini nachukia.
Tatizo nyie ndio mnakuja kuwa michepuko ya hao waume zao
 
Ooh Asante sana kwa neno hili
Umenena vyema aisee .. mambo mengine hayahitaji haraka kabisa .

Sema jamii inayotunguka ndo shida maana kila unapoenda hilo swali huwezi kuliepuka kabisa bado ndugu nao watakuuliza vipi kulikoni ?
Bado hapo unaona rafiki zako wana familia zao
Wewe upo .. hakika si rahisi unaweza kuanza kujiona kama una nuksi fulani hivi wakati sio .

Kikubwa ni kuwa mvumilivu na kusubiri muda sahihi ukifika .. mambo mengine hayawezi kubadilika katika jamii zetu .

A quote from Dada Vaswani
Marriage is a commitment for life.. It is a permanent, lifelong relationship.
Almost kila mtu anakuwa na ndoto, maono, matamanio, matarajio n.k.Na tunaweka na timeline kabisa kwamba hadi muda huu niwe na 1,2,3,4. Sasa wakati unapanga mambo yako, usisahau kuwa Mungu na yeye ana mipango yake tena ambayo tunaamini na kujua kwamba ni myema kuliko ya kwetu. Ikitokea mipango yako haijakamilika kibinadamu lazima ujisikie vibaya; lakini usije ukaishia kuwa mlalamishi na mnyonge kwa sababu hujapata vitu fulani; utaishia kuwa an ingrate. Tatizo letu huwa tunahesabu sana baraka za wengine ambazo tunaziona ni kubwa zaidi; tunasahau kuhesabu baraka zetu ambazo nazo kuna watu wanaziangalia na kuzitamani. Comparison is the thief of joy.

As a result tunajikuta tunakuwa watu wa kulalamika na desperate. Kama ambavyo Mimi mzazi sipendi mtoto ambaye atakuwa hanishukuru, ananilalamikia tu kwa sababu ya kitu fulani ambacho sijaweza kumpatia; definitely hata Mungu anachukizwa na watoto wake wasio na shukraniz bali walalamishi. So utaishia kulalamika tu badala ya kuenjoy baraka ambazo Mungu amekupa. "Praise and be Raised, Complain and Remain.

Ubaya zaidi binadamu huwa haturidhiki; Leo utahitaji kitu fulani desperately, kesho ukishakipata unataka tena kitu kingine ambacho huna. Ingawa kwa wanawake ndoa ndiyo kama lifetime achievement kwetu; Leo utaililia wee, ukishakipata unahamia kwenye tamanio la kuwa na watoto, then mume ana uwezo kiasi gani mbona mume wa mwenzio kamfanyia hiki mkewe/familia, then watoto wanasoma shule gani, watoto wa marafiki zenu wanasoma shule fulani, mara nyumba and the list goes on. So kwenye maisha most likely hakuna siku utakuwa na Kila kitu unachokitaka; ni wewe unaamua kuridhika na kuvienjoy vichache ulivyobarikiwa.

Kubwa zaidi we have to believe and honor God's time. Yeye atakupa hiyo ndoa kwa wakati ambao anaona ni sahihi zaidi kwako. Inawezekana ungekuwa umeshaolewa kwa wakati ambao unautaka wewe; leo ungekuwa mjane au divorcee tayari. Na hata Mungu akiamua kutokukupa ndoa kabisa; shukuru tu; ni wangapi ambao ndoa zao zimekuwa sababu za vifo vyao? Naamini wangejua yaliyopo mbele yao, wangeamua tu kubaki kuwa single. Tujifunze kuwa watu wa shukrani aisee

Kuna a certain sermon by Joel Osteen kuhusu kuwa na positive perspective. Alisema wengi wetu tunaona maisha yetu like a boring routine; unaamka Kila siku, unakwenda kazini/biashara then unarudi nyumbani. Kila siku inakuwa hivyo kiasi kwamba tunachukulia kama ni kitu cha kawaida tu, nothing exciting. Lakini kumbe hiyo boring routine ni baraka kubwa sana; wangapi wanalala na hawaamki tena, au wakaamka wakakuta baadhi ya viungo havifanyi kazi; wangapi wanatafuta kazi/biashara ambayo kwako imeshakuwa boring? So kumbe ukiamua kuwa mtu wa shukrani; una vitu vingi sana vya kukufanya ushukuru. Kuna vitu tunavi-overlook sana, lakini ni vitu vya msingi mno, ni baraka kubwa mno kwetu;

1. Umebarikiwa upendo wa familia yako, ndugu marafiki. Una wazazi, kaka, dada, bibi n.k. Ni kama kitu Cha kawaida tu kila siku; ila siku akiondoka huyo ndugu ndiyo utagundua kuwa umepoteza baraka kubwa kiasi gani. Mimi binafsi nikisikia mtu anaita "baba" na baba yake akamuitikia; natamani nimwambie ni kiasi gani amebarikiwa kwa sababu ni baraka ambayo mimi sina tena. Kuna moments za furaha sana unabarikiwa nazo, lakini unaishia kuwa na simanzi like I wish baba angekuwepo hapa.Though I'm grateful niliienjoy baraka yangu to the fullest.

2. Afya. Ukiwa na afya njema then uone watu wanaoumwa serious; utajiona wewe ndiyo mbarikiwa dunia nzima. Ukipata changamoto ya kiafya; haki unaweza kumwambia Mungu chukua vyote niachie tu afya yangu.
Kuwa mzima, unapumua vizuri; ni baraka tosha kabisa, unapaswa kushukuru.

3. Peace of mind. Kuna watu Wana almost Kila tunachokitamani lakini hawana amani ya moyo. Kuwa na amani ya moyo aisee ni baraka kubwa sana, and no amount of money can buy that.

So ukiamua kuwa positive kila kitu utakiona kwa upande chanya sana. So unaweza tu kuchukulia kuwa huu muda ambao hujaolewa ndiyo muda mzuri wa wewe ku-add value kwenye maisha yako. Tangu ukiwa mdogo una ndoto na maono yako binafsi, ndiyo muda wa kuyatimiza sasa. Ukishaolewa mambo yanabadilika kwa kiasi fulani; mnaanza kutembea kwenye maono ya mume sasa na sio ya kwako (kwa % kubwa). So kuna vitu au ndoto zako ambazo zitamezwa na maono ya mume.

Pia una wakati mzuri wa kufanya chaguo sahihi la mume; kiakili unakuwa umekomaa sana. Mimi binafsi naamini ningeolewa in my early 20s ningekuwa divorcee sasa hivi. Kuna vitu vingi vya msingi ambavyo ningevi-overlook na vingekuja kunitesa sana; what matters to me at that time ni kwamba tunapendana. Lakini sasa hivi ndiyo naona; love alone is not enough; kuna vitu vingi sana vya kuviangalia. With age vigezo vyangu (vya msingi) vilikuwa vinaongezeka kwa kweli; kwa sababu akili yangu ilikuwa imekomaa kuchanganua mambo; unayaangalia mahusiano kwa jicho la kesho na kesho kutwa na sio leo hii ya tunayosema tunapendana.

Ni sawa kutamani au kuomba vitu fulani ambavyo hatuna; but tusijistress sana juu ya tusivyonayo hadi tukakufuru. Tuwe watu wa shukrani. Sio Kila tunamwendea tu Mungu kumuomba, hakuna siku tunamwendea kwa shukrani na sifa.

C.c Carleen upitage na huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ni kwa nini? juzi juzi hapa kuna classmate wangu nilikutana nae ktk stori ananiambia kaolewa na ana watoto wawili mimi vipi nikamuambia sijaolewa wala sina mtoto akaanza kunisema tatizo nachagua sana imagine ni mwanamke mwenzangu ananisema hivyo. Sijui hii kitu inasababishwa na nini nachukia.
Kuna rafiki zangu wawili
Kwa nyakati tofauti wananiambia
Hivi D si uzae hata katoto kamoja!?

Tumbo ninalo Ok, nazaa na nani sasa? Hawa watoto wa mama mkwe waliolamba ugolo? Hapanaaa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom