Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Oooooh hapo sawa mlongo, ila daah najisikia vibaya wazazi wakiachana, huwa tatizo kwa watoto
Na kuna mazingira ambayo ni even worse kwa watoto; hata kama wanalelewa na wazazi wote wawili. You simply traumatize the innocent kids. Na wakati mwingine ni bora tu muachane kuliko kuja kuchomana gunia za mkaa
 
vita zangu utaweza bina...!!!nikipenda nafalll mpk nakua mwehuu ila nikiacha naacha kama sijawahi kukuonaa!!!
Ile unaulizea huna kwenuuu!!!!maana sio kwa matukio hayoo unayopigwa

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Yaani wewe ndio mimi kabisa
Mtoto wa mtu asije tu niletea drama jamani...mbona ntachizika kwa stress..ukizingatia huyo mtoto wa mtu ndio nategemea awe baba.


Mungu ni mwaminifu sana.
 
Napenda sana fasihi na nimesoma vitabu vingi sana. Vya Shaaban Robert vyote, vya Kezilahabi vyote, vya Musiba vyote, vya Mohammed Said Abdullah vyote, vya Ngugi karibia vyote, vya Achebe karibia vyote...na vingi vya falsafa...

Kulikuwa na sababu kwa nini Fasihi ilikazaniwa sana katika akademi za Wagriki wa kale japo mkazo hasa ulikuwa kwenye Hisabati. Ni kwa sababu, pamoja na falsafa, fasihi inapanua sana uwezo wa kufikiri na kujenga hoja. Inakufanya uyaone maisha na malimwengu katika mawanda mapana; na kuona masuluhisho mengi kwa matatizo yale yale yanayokukabili...ndiyo maana ni nadra sana kwa watu waliosoma sayansi kuwa viongozi wazuri kwa sababu wao humwona binadamu kama mashine tu inayojiendesha kwa kufuata kanuni maalum jumuishi zilizosimama tisti na huwa wana tabia ya kutumia maguvu. Kumbe kama wangesoma fasihi na falsafa wangetambua kwamba binadamu ni kiumbe tata sana ambaye kamwe hawezi kubanwa na mfumo au mkondo mmoja wa kufikiri na kimaisha.

Tuje tukutane shem tuongee haya mambo huku tukitafuna kuku watamu wa pale kiotani Tango...Na wanangu akina Minza wawepo
na fasihi nafikiri ndo ilitumika na kina Aristotle kipindi hiko kufikikisha ujumbe kwa watawala
Unaandika vzr sana yaani una maarifa mapana sana tena mnoo!!

Karibu sanaa tena sana watakuwepo wanakusubiri kwa hamu ankoo!!!

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Wallahi sijisifu mstari wa mwisho ndo ilivyo yaani!!namheshimu to core mpk mwinga mmoja ashawahi uliza huyu mama Minza mbona anapendwa japo hayupoo!w
Naweza kua nilikua na weakness zangu nyingi pia siwezj sema!
Ila wamama wa kisukuma wakikupenda utakula vyan ndani ,shimba,wigeleko na t elly ,wamama zenu wako poa sana hongereni

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Baby mama wangu alinizunguka aisee. Akaenda akamchimbia mama kisima cha maji bila mimi kujua. Na vitu vingine vingi. Sikukuu zote mimi siombwi kitu kumbe ni mwinga wake keshafanya. Yaani walikuwa wanapendana hatari. Mpaka mama akiumwa anatafutwa yeye kwanza na siyo mimi...hata baada ya kutemana naye bado wakabakia kuwa karibu; and this was super awkward to me. Yaani alikuwa anamwona kama binti yake kabisa. Mpaka wengine wakawa wanasema pengine kwa vile mimi ni kitinda mimba basi alikuwa amehamishia upendo huo wa last born kwa huyo binti.

Kwa hiyo naelewa sana shem. Wakikupenda hawa wazee basi wamekupenda na wakikuchukia mtiti wake pia ni shida...Ni lazima pia shem una roho njema, mwenye heshima na upendo. Vinginevyo msingeelewana hivyo. Hongera shem!
 
Back
Top Bottom