Nimecheka. Ila if you bag yourself a good man now.....(uning'ate sikio)
Yeah huu ni muda wako wa ku-add value kwenye maisha yako. Una ndoto, maono na matamanio yako; ndiyo muda wenyewe sasa. Kesho ukishakuwa na familia; ulichokifanya na kukijenga leo ndiyo kitakuja kukusaidia huko mbeleni. Unaweza ukaja kulazimika kuacha kazi/biashara, kwa sababu ya familia. Ongea thamani kwenye maisha yako sasa...
Above all; ukishaolewa, mnaanza kuishi maono ya mume sio ya kwako tena. Atalitimiza kusudi lake, huku wewe ukiwa msaidizi wake mkuu. Mchungaji wangu alikuwa anatusisitiza sana tupambane angali tukiwa mabinti; kuna muda ukiwa na watoto hata muda wa kuomba vizuri huupati. Hata kuombea watoto wako, waombee kuanzia leo kabla hata hawajaja. Akiba yake itakusaidia sisi utakapopigwa na hata hiyo nguvu ya kumuombea huyo mtoto ukaikosa.
Alikuwa anatuambia. Kuna aina 3 za wanawake waliofanikiwa
1. Ambao hawajaolewa
2. Walioachika/kufiwa.
3. Waliofanikiwa kabla hawajaolewa
To be continued.....