Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Uwiii !!!

View attachment 2072135

Kumbe mziki wa Covid sio wa kitoto aisee. Juzi usiku nilifikiri this is it. I am done on this planet lakini Mungu si Athumani aisee jua likachomoza salama

Ulikuwa ni mwendo wa ku-monitor presha, kiwango cha Oksijeni na joto la mwili - indicators 3 za muhimu sana kwa mgonjwa wa Covid.
View attachment 2072137

Mwili bado haujakaa sawa 100% ila ni mwendo wa malimau na tangawizi kwa sana. Nimeweza hata kwenda jogging leo. Mungu ni mwema aisee...Maisha...Uhai!
View attachment 2072141
Polee mkuu
 
Wakuu.

Japo hatujuani lakini tunaishi kama ndugu. Na hakuna kitu cha thamani kama kuombewa na kutakiwa mema na mtu usiyemfahamu. Maombi ya aina hii huwa na nguvu sana kwa sababu huwa ni maombi ya kweli yasiyo na ajenda wala mawaa.

Napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wote mlioniombea na kunitakia mema; na uponaji wa haraka. Japo Covid hii (tena Delta mwenyewe) ilinijia kwa nguvu sana lakini kwa maombi yenu na upendo wa Mungu nimepona. Bado tu kakikohozi ka mbali lakini hata nikikimbia kifua hakiwaki moto kama hapo kabla...na viuchovu uchovu tu vya hapa na pale. Kwa jina la Yesu naamini kuwa nimeshapona

Sikuweza kumjibu mmoja mmoja lakini kwa umoja wenu napenda sana kuwashukuru mno 9.8ms squared, Heaven Sent, mahondaw, Makiwendo, Saint Anne, T 1990 ELY, Tinsley, Gregory 2000, Karma, Kashaija72, Chakorii na mawardat.

Asanteni sana wapendwa na Mungu Awalinde na kuwabariki sana. Hapa nilipo ni kama naishi peke yangu lakini kupitia kwenu nilijiona kama nina jeshi kubwa la watu wanaoniombea na kunitakia mema.

Hebu Mungu Akatubariki sote na mwaka huu mpya ulioanza ukawe wa mibaraka tele; na kila mmoja wetu akaweze kutimiza ndoto zake na malengo aliyojiwekea.

Nawashukuru sana


View attachment 2075249
Pole sana bro, mungu ashukuriwe sana, kila jambo na wakati wake,na kila jambo limpatalo mtu huacha funzo fulani na hatua fulani ya kukua,aidha kifikra kiroho au kiimani. Pole sana, ujaliwe kuwa sawa mapema.
 
Back
Top Bottom