Nadhani ni madawa ya kuongeza nguvu za kiume yaliyotamalaki kila kona. Na watu wenye tatizo hilo hupita njia za mkato tu na kufakamia haya madawa yanayouzwa kiholela hata bila kujua hasa kiini cha tatizo ni nini. Mara nyingi tatizo hilo, ukiachilia mbali sababu zinazosababishwa na mfumo mbovu wa maisha, linasababishwa na matatizo mengine ya kiafya kama shida za moyo, presha, kisukari n.k. Kupita njia ya mkato tu na kutumia haya madawa kunaweza kuwa na madhara makubwa zaidi kwa mtumiaji kwa sababu kama kiini ni moyo wenye matatizo au presha mtu anaweza kujikuta anazimika na huo ndo mwanzo wa kuimba parapanda...
Ndicho nilichomaanisha best...