Watu wengi hawajafahamu kuwa self-respect ni kitu muhimu sana. Kuliko kufika huku sometimes ni vizuri mmoja akakaa kimya, hii kudhalilishana siyo nzuri kabisa. Unaweza ukawa unamtukana mtu yeye akatake personal akaenda kujidhuru mbele ya safari. Mambo ya cyberbullying kwa nchi nyingi ni kuvunja sheria za mtandaoni, lakini hapa kwetu watu hawachukulii serious kabisa.
Kuna mtu anaweza kuwa anakufahamu halafu akapitia uzi akasoma maneno machafu unayopost mtandaoni ikaathiri hata career yako ama heshima yako. Na hata kama hatufahamiani ni vizuri kuheshimiana tu na kuepusha kufika mbali na kutoleana maneno machafu. Tunakuwa kama hatujaelimika.