Selfika na JF: Snap it. Show it

Ndugu yangu. Mambo yalibumburuka pale bustani ya Eden na li Abeli kumuua nduguye Kaini baadaye. Tangu hapo ni kizaazaa tu kuanzia vitani huko mpaka kutoana roho kwa mtu mmoja mmoja hata kwa sababu za kijinga ajabu. Na kwa wanasiasa hawa uchwara kukolimbana (kwa waziwazi au kurogana) wala siyo jambo la kushangaza.

Wewe unaongelea katika kiwango cha juu cha urazini kwenye upendo wa kimalimwengu lakini katika uhalisia wake binadamu ni mnyama katili sana. Na ukiangalia kwa umakini na ujumuishi wake, unaweza hata kukosa maana ya maisha yetu hapa duniani. Kwamba eti tumezaliwa tufanye kazi, tule, tunywe, tugegedane na mwisho tufe. Inashangaza sana...

Ila hawa wanaofanya haya mara nyingi mwisho wao huwa siyo mwema. Huwezi kumwaga damu isiyo na hatia halafu ukabakia salama. Karma will always find you....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…