Selfika na JF: Snap it. Show it

Katakata mabamia loweka kidogo na maji. 'Sikumbuki kama yanachemshwa or not.

Ila ule utelezi jau [emoji23] thoe nywele ilieleweka na nilipata mara 2 tu.
Oooh ahsante,nitafanya maana raia wananiambia upele unamuota asiye na kucha[emoji16]nataka nianze kuwekeza kwenye nywele[emoji2902][emoji2902][emoji2902]
 
Ahsante,,,ya bamia unatumiaje?,nielekeze
Mahitaji
[emoji261]Bamia kumi (10)
[emoji261]Mafuta ya maji (African Black castor oil au coconut oil au olive oil)
[emoji261]Juice ya Tangawizi
[emoji261]Asali

Jinsi ya kuandaa
[emoji263]Osha bamia zako vizuri kuondoa uchafu wote
[emoji263]unaweza kukata kata kuwa vipande vidogo vidogo au ukamenya tu (kuexpose undani wake)
[emoji263]Weka kwenye sufuria yako safi
[emoji263]Ongeza maji kiasi (kikombe kimoja au viwili vinatosha) na ufunike
[emoji263]Chemsha kwa dakika 10 hadi 15 mpaka ile gelly au ute wa bamia uwe umetoka wa kutosha
[emoji263]Epua na uache ipoe kwa dakika kadhaa
[emoji263]Baada ya hapo chuja kuondoa vipeke na upate gelly tuu

Kama unatengeneza steaming
[emoji263]chukua ute ulioupata gawanya mara mbili
[emoji263]Nusu ya kwanza changanya na tangawizi na asali na mafuta yoyote ya kimiminika (hasa Castor oil)
[emoji263]Baada ya kuosha nywele kwa shampoo (hakikisha nywele zako ni safi) paka mchanganyiko kwenye nywele zote
[emoji263]Vaa shower cap au steamer na ukae kwa dakika 30+
[emoji263]Osha kwa maji mengi
[emoji263]Chukua ule mchanganyiko uliobaki changanya na mafuta kijiko kimoja hapa utakua umepata leave in conditioner
[emoji263]Nywele zako zikiwa mbichi na safi pakaa vizuri kuanzia kwenye ngozi hadi kwenye ncha.
[emoji263]Chambua vizuri nywele zako kidodgo kidogo kuhakikisha imeingia vizuri kwenywe nywele zote.
[emoji263]Unaweza kusuka mabutu (bantu knots) au twists za njia mbili au tatu au nywele za mistari kawaida nywele lazima ziwe na unyevu kabisa.
[emoji263]Ukiona zinakauka unanyunyiza maji tena.
[emoji263]Ukimaliza acha zikauke vizuri utaendelea kupaka mafuta yako kama kawaida ili kuzifanya zing’ae.
[emoji263]Ukifumua unapata mawimbi mazuri unaweza kubana utakavyo nywele zako.
 
Ahsante Sana,ubarikiwe naanza kazi[emoji120]
 
Process ndio ndefu hivi? Me nilimix bamia na maji tu.

Nikipata muda nitajaribu..
 
Hapo bamia ilisaidia dia.

Mimi mvivu sana kushughulika na nywele, hizo ulizoona hapo nimezikata mwezi ulioisha mwishoni.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]duuuh umekata!!!

Huwa natamani kunyoa,lakini nikiwaza jinsi ya kuanza kusuka vikiwa vidogo,naishiwa pozi

Hizi zangu zina miaka miwili,nimezipunguza mara moja
 
Dunia ina mambo hii jamani!! Watuhumiwa nao wanatuhumu wengine[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji2216][emoji2216][emoji2216][emoji2216][emoji2216][emoji2216]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…