Selfika na JF: Snap it. Show it

Kabisa mkuu kusoma siyo kukurupuka
 
Kwahiyo unguja ni tofauti na mjini magharibi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kijiografia ni kisiwa kimoja ila kiutawala ni mikoa mitatu tofauti kuna Mjini Magharibi, Unguja Kaskazini na Unguja Kusini ndani ya kisiwa kimoja

Visiwa vya Zanzibar vinajumuisha mikoa mitano ambayo ni Mjini Magharibi, Unguja Kaskazini, Unguja Kusini, Pemba Kaskazini na Pemba Kusini

Sasa Mjini Magharibi na Unguja Kaskazini na Kusini kijiografia ni mikoa iliyoungana kwenye kisiwa kimoja wakati Pemba Kaskazini na Kusini ni kisiwa kilichojitenga peke yake lakini hivyo visiwa vyote kwa pamoja vinaitwa visiwa vya Zanzibar
 
Kwahiyo unguja ni tofauti na mjini magharibi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeona sasa hapo Anne

Hicho kisiwa cha juu ni muunganiko wa mikoa ya Pemba Kaskazini na Pemba Kusini, na hicho cha chini ni muunganiko wa mikoa ya Mjini Magharibi, Unguja Kaskazini na Unguja Kusini

Ila visiwa vyote hivyo viwili kwa pamoja vinaitwa visiwa vya Zanzibar

Daah nyie ualimu ni wito
 
Lakini hiyo mjini magharibi si ipo unguja.

Na unguja na Pemba Ndiyo kwa pamoja inaitwa Zanzibar.
Yaani nia yangu ilikuwa tu kujua km anaishi unguja au Pemba.

Asante

Kuwa mwanafunzi ni wito zaidi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…