Ooh! Habari za hovyo kabisa hizi...
Kama binadamu hatuna la kufanya isipokuwa kumuombea marehemu pumziko jema na lenye heri. Na kwa wapendwa walioachwa; hebu Roho Mtakatifu Ajulikanaye pia kama Mfariji Mkuu Akawapoze mioyo yao na kuwapa faraja na matumaini katika kipindi hiki chenye giza na maumivu makali.
Na kwenu
Heaven Sent na/au
Mshana Jr. Saint Anne ni memba mwenye mahusiano mema na watu wengi; na anajulikana sana hapa. Anzisheni uzi kamili wenye taarifa hii ili habari hizi ziweze kuwafikia watu wengi. Na cha muhimu zaidi, toeni mwongozo wa jinsi ya kutoa rambirambi ili tunaoweza kufanya hivyo tufanye hivyo mara moja.
Asanteni na poleni