Selfika na JF: Snap it. Show it


Kwa kweli waugawanye tu huo mkoa

Poleni kwa yaliyowakuta aisee! Nimegundua kila binadamu aliyekuwa akajielewa ni lazima apitie tukio fulani la aibu maishani mwake kabla hajafa aidha mbele za watu au nyuma za watu lakini hilo ni lazima!

Eehh ndugu yangu maisha yenyewe ndiyo haya haya. Mie nimeamua kusamehe tu na kupotezea and now it is well with with my heart.
 
Kuna watu kadhaa walishaniambia pia ila siku tulia maanani saaana.


Basi itabidi uanze kutilia maanani sasa kuwa na wewe ni comedian

Kuna comment yako moja hivi SYB alikuwa amebadili avatar akakuquote ukamuambia airudishe ile ya siku zote. Sasa namna ulivyomuambia (nimesahau) na zile emoji ulizoweka aisee nilicheka sana siku ile nikajisemea tu haki huyu sijui anapuliza kile chenyewe cha Jamaica.
 
Hapana...pombe ikipendwa na wanawake huwa siigusi,ndio maana hata serengeti lite sigusi kabisa bora ninywe maji
Hahaha basi tunafanana! Mimi pombe hizi wanazosema ni nyepesi hazina tofauti na juisi eti kisa hazina hangover basi eti mimi ndiyo naziona chungu na huwa nazinywa basi tu!

Mimi pombe kama Zanzi na Amarula zinanishinda sababu ya kuwepo na ile ladha ya maziwa maana mimi na maziwa fresh ni mbingu na ardhi aisee hata ile harufu yake tu huwa sipendi kuisikia! Savanna ndiyo kabisa naionaga mbaya kinome ila eti naambiwa ndiyo kipenzi cha wawanawake wengi hapa mjini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…