Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Suala la kutunza mazingira Morogoro ni la kimila.
Misitu ya asili ya mkoa huo bado inatunzwa na kuzalisha mvua za kutosha kila siku.
Ndiyo maana mpaka sasa bado wameweza kuhifadhi maji mengi kwenye mito ya mkoa huo kuliko mkoa wowote ndani ya jamuhuri ya Tanzania.
Upo sahihi chief,nimetembea mikoa mingi nchini,ila nafurahia sana maisha na mandhari ya mikoa hii
Morogoro
Kilimanjaro
Mbeya
Iringa
Arusha

Ni Kati ya mikoa huwa napenda sana uoto asili wake. Pia nadhani ile kampeni ya kupanda miti irudi tena,tusije kuwa jangwa siku za mbeleni.
 
Hadithi inasisimua sana.
Ila daaa!! Mkoa wa Morogoro ni mkubwa sana.

Tumetoka Dar saa 12 asubuhi tukaingia Moro mjini saa 2:00. Ifakara saa 7:30, Mahenge saa 1 usiku, Mwaya saa 4, Iputi saa 5, Ilonga Selous Game Reserve saa 6:30 usiku.
Mkoa huo huo mmoja unatembea masaa kibao
Duuh saa sita unusu usiku? Wakati hapo Dar-Mbeya ushafika ushalala na uchovu wa safari ushapoa!
 

Si unaziona ila akili zako

Khaa ndiyo nini kunichekesha hivi mtoto wa mwanamke mwenzio? Nimeanza huo mstari wa kwanza tu nimecheka kwa nguvu sasa hadi namaliza comment yote ikabidi niweke kwanza simu pembeni ili nimalize kucheka!

Eti Morogoro ni kubwa kuliko Tanzania daah kiukweli naungana na wale waliosema huo mkoa ugawanywe jamani. Kwa kweli huo utalii wa ndani nimeupenda yaani kama nakuona vile ulikuwa unaserereka na kibegi.

Mngekuwa maeneo ya mjini mjini halafu watu wangeona hilo tukio haki mngeshikwa uchawi maana wabongo hatuchelewi! Mie hizi safari ndefu za siku kadhaa ndiyo nazipenda ila tu huo usafiri uwe na kila kitu ndani mfano sehemu za kula na kulala ila siyo ule usafiri ambao utakulazimu kushuka kwenda kula au kulala na ndiyo maana mie napenda sana treni!

Hahaha nilimaanisha mwenye picha ndiye alinielewa tukayamaliza yule aliyesambaza kwa kweli sijawahi kumtafuta wala kumuuliza chochote hadi leo nimeona nimsamehe na nijikalie tu kimya! Ila kiukweli kupatana ni jambo jema sana mwenyewe huwa sipendi malumbano na nikiona naelekea kugombana na mtu basi ni either nitajishusha au nitakaa kimya tu ili tusifikie kwenye ugomvi!
Karma Moro ni kubwa mnooo aise...ni kama imekaa namba 8 hivii kho!!!!
😁😁😁kwahiyo mwandiko umekuchekesha hahahaha ulikuwa umemiss kucheka 😁😁

Yap usafiri w moja kwa moja ni mzuri sana sio ule wa kwenda kuchimba mizizi huko na kununua fudi khoooo...

Ohooo ingekuwa Town ningeshakuwa star sasa hivi maan ningetapakaa dunia nzima kwa kipindi kifupi mno..kila mtu mwandishi wa habari aiseh...nikilikumbuka lile tukio aiseh 😁😁😁na nikijiangalia...basi utukufu namkabidhi Bwana 😁😁

Ohooo nilijua ni yule aliyesambaza ndo mmeyamaliza...ila sio mbaya sana cha muhimu ni Amani tu.mAmbo mengine yanatokea maishani kwa ajili ya kitupa fundisho
 
Back
Top Bottom