Tuweke picha ila heshima ni Muhimu.
Dogo picha zako hazina maadili,una uhuru na jana nilisema binadamu wote ni sawa ila si sawa kuweka hizo picha.
Sikuingilii ila jiangalie sana,njia uliyoichagua si nzuri,bado unayo nafasi ya kurekebisha,Mungu ni pendo, ndiye njia na anatuonyesha njia...huko ulipo sipo kabisa
Mungu bado anakuhitaji,ubadilike.
Hakuna heshima yeyote niliyovunja humu, hizo picha zipi zisizokua na maadili? Kwan ukosefu wa maadili n kuwa LGBT? najua kanuni na taratibu zote za hii forum, wala sijakiuka hilo. Hizo picha nilizoweka ilikua ndan ya comment ambayo nilikua namjibu mtu nka ambatananisha na picha ili aaone uhalisia wa kile anachokizungumzia,
Haikua haja ya watu wengine kuhangaika na kufurukuta kuhusu hilo kwani halikua linawahusu, na sidhan km wangekua buzzy na mambo yao binafsi km wangepata na chance kujadili suala ambalo kwao ni tatizo au haliwapendezi.
Umetoa hoja ya kutaka mabadiliko kwangu, unadhan wee ndo unaweza kunibadilisha kwa hayo maneno yako kutoka kwenye vitabu fulani? Mabadiliko yatafanywa na maamuzi yangu mie mwenyewe binafsi km nikitaka. Halafu hakuna hoja nyingine inayoweza kutetea wakati wa pingamizi ktk suala hili zaidi ya DINI?
kuhusu hoja ya DINI kwangu haina nafasi wala mashiko, labda kuwepo na hoja nyingine mbadala naweza kukubali kudadavua, unadhan kila mtu ana imani na hicho unachokopigania ktk pingamizi la suala hili?
Huko kwenye dini mie mwenyewe muumini mzuri tyuuh, nimeanza kushiriki ktk masuala ya dini tangu mdogo nikiwa na miaka 8, nimeshiriki shirika la watoto (KIPAPA), nimetumikia kanisani, nimeimba kwaya. na nimekulia familia yenye msingi imara ktk maadili na malezi.
Lakini yote hayo hisia zangu hazihusiani na hilo, na siwezi kufanya kitu ambacho sina ashiki eti niridhishe jamii inayonizunguka kwa kipi na ili iweje? Naishi vile mie nataka maisha yangu yawe, ili hali sivunji kanuni, taratibu na sheria za nchi zilizowekwa.
Samahani sana kwa maelezo haya, km nitakua nimekukwaza nisamehe tyuuh.