Ishi maisha yako, fanya unacho kiona ni sawa,
Ila kuna umri utafika utakuwa na huo uitaji..
Alafu mbali na hvo pia kuolewa ni bahati
siku mungu akikutunuku utaolewa tu wala usiwe na wasiwasi
mimi nilijikomit kwa mahusiano ambayo nilipenda mpk kufikia hatua ambayo niliona naenda kufa niache maisha, nilimuombea sana nilifunga na kusali kwa ajili yake lkn alibadilika kiasi kikubwa sana kiasi kwamba kila mtu aliniona naenda kufa kisa mapenzi ila siku niliyo muacha wala hakuna aliye nishauri tena..
Toka hapo sijui kubembeleza mausiano kwa ajili ya kutaka ndoa naamin mungu akikupa wako kila kitu kinaenda vzuri
Nashukuru nimepata
Kwa hyo kama unajiona haueleweki ipo siku utaeleweka tu mpenzi na utaeleweka kwa mtu ambaye mungu anakuletea sio unaye mtaka wewe