Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Na mfano mwingine halisi ni huyu anayejiita Heaven Sent. Kuna wakati huwa natafuta tu baadhi ya comments zake na kuzisoma. There is something special about her (upako, wisdom, akili kubwa, ubinadamu...) na nilipogundua kuwa ni Mnyaki nilishangaa sana.

Wanyaki barikiweni sana kwa kweli
Thats very true
She is heaven sent indeed
 
At the end of the year
20201230_181456.jpg
 
Na mfano mwingine halisi ni huyu anayejiita Heaven Sent uliyemtaja. Kuna wakati huwa natafuta tu baadhi ya comments zake na kuzisoma. There is something special about her (upako, wisdom, akili kubwa, ubinadamu...) na nilipogundua kuwa ni Mnyaki nilishangaa sana.

Wanyaki barikiweni sana kwa kweli
Amina barikiwa na wewe
 
Oohh kumbe hii ndiyo iliyokuwa hofu yako? Basi ndiyo maana nikahisi tu kuwa lazima ulinielewa vibaya!

Sikiliza my dear kinachoongelewa humu JF huwa kinabaki kuwa cha humu humu JF! Hayo ya huko nje sisi hatuyajui mimi sijui wewe unafahamiana na nani na nani haufahamiani naye nje ya JF!

Na hata niliposema mtu chake ndiye mwanaume pekee unayembebisha humu JF nilimaanisha ni ile kiJF JF tu kama wanavyofanya watu wengine! Na siyo kwamba eti nimemaanisha wewe na mtu chake mnadate nje ya JF na wala sijawahi kuhisi hivyo!

Mbona wapo watu wengi tu humu wanabebishana na hawafahamiani kabisa nje ya JF wengine hata pm tu hawajawahi kwenda? Hapo nilikuwa nataka kumtania mtu chake tu kuwa mbona analalamikaga eti mademu wa JF hawamkubali wakati wapo wanaomkubali!

Tena yeye ana bahati amepata mwanamke anayembebisha yeye peke yake tofauti na wanawake wengine ambao wanabebisha kila mwanaume hadi hao wanaume wanaobebishwa unakuta wanaanza kuoneana wivu! Ambao nao najua ni ule ule utani wa humu humu JF tu!

Kama nilivyosema mimi humu JF sijui nani anafahamiana na nani na nani hafahamiani na nani na wala hakuna couple ninayoijua humu JF zaidi ya Smart911 na mahondaw na ni kwa sababu wao huwa wanajitangaza! Wengine wote wanaobebishana humu mie huwa nachukulia ni kama wanataniana tu!

All in all mimi na mtu chake hatufahamiani my dear wala hata pm hatujawahi kwenda lakini humu jukwaani tumeshachitchat mara kadhaa na huwa namuona ni mtu poa sana! Mimi simjui wala yeye hanijui hivyo hata mambo ya mahusiano yake mimi siyajui na utani wowote ninaomtania humu basi mie nachukulia ni wa humu humu tu!

Kama yuko mtu mwingine aliyeelewa vibaya hicho nilichoandika mimi sijui namsaidiaje kwa kweli! Kama nilivyosema kuwa binadamu huwa tunaelewa kile tunachotaka kuelewa sisi na si kile kilichokusudiwa kueleweka!
Kama mimi chama la wana nabebisha kila mtu hapa hmnga ubaguzi
 
Back
Top Bottom