Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Kuna mahali kakuita Karma.. umeona?
Nimejikuta nachekaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha niliona ila sikushituka sana sababu tangu nimebadili ile id hata mwezi haujesha na pia sikuwa nimeangalia kajiunga lini, ila pale aliposema endiwo (in Zoë's voice) ndiyo pakanishitua hadi ikabidi nikaangalie kajiunga lini maana hilo neno humu sijalitumia muda mrefu.
 
hiyo statement bora umewahi kuisema mwenyewe, yaani nusu nikuambie hapa kesi ya nyani umeleta kwa ngedere.

nimekumbuka kuna mtu alianzisha uzi wake, ukatoa comment moja hiyo hadi alijaa sukari nikashangaa tu "Jael sitaki mazoea na wewe", nikasema uwii huyu dada ataja kuua watu kwa hasira na majibu yake haya, maana sikuelewa ile comment yako na kutaka mazoea vinahusianaje.
Hiyo itakuwa uliota kwakweli.

Tafadhali sana usilete ushahidi.
 
Si mtu anaona ukimuona sura yake basi ni kama umeiba nyota yake
Hahahaha khaa nani kasema hayo yote, wabongo tuna imani za ajabu jamani.

Hapana mkuu mtu kutokukutumia picha yake sidhani kama inahusiana na kuibiana nyota, labda inawezekana hayo mambo yapo ila mie siamini kwa kweli.

Ni vile humu hatufahamiani sasa ukisema kila anayekuomba picha yako umtumie utafahamiana na wangapi, isitoshe humu hatuaminiani sababu ya huu mtindo wa kuchomoleana betri.

We siyo mgeni humu, utakuwa unajua na umeshaona baadhi ya watu waliochomoleana betri sababu ya kukubali kutumiana picha kirahisirahisi tu.
 
Back
Top Bottom