Selfika na JF: Snap it. Show it


Kwa Kweli mi nimekutana na masela wengi humu JF na Kwa Kweli tumepiga deal za maana na wengine tupo kwenye magroup ya WhatsApp tunajifunza mambo kibao kutoka Kila mmoja wetu. Nimewahi unganishwa kazi kadhaa na hela ndefu tu, JF sio mchezo, Au ni mimi tu ndio lucky
 
Tatizo la mtu kukuanika humu kwa ID mpya ni la mtu ambaye kwanza hajakuwa na hajielewi kabisaa!!!

Joanah nafikiri hilo unalijua sana tuu kutokana na watu unavyowaona pm! Miandiko tuu inatosha kukuambia tabia ya mtu!

Lengo la kufahamiana huwa ni la watu wawili, kama ni urafiki ni siri yenu ila ambalo huja kuleta shida ni mahusiano yakiingia kati hasa wale wasiojitambua dear!!!
 
Labda uko na bahati mkuu... Nyie wenyewe kwa wenyewe hamnaga shida, sasa issue inakuwaga me na ke!
 


Sakayo mie kuangalia mwandiko wa nani ni mwema na wa nani sio mwema sijui kwasababu kuna pretenders wengi

Jambo ambalo nazidi kujifunza ni kutrust nobody

Napenda sana kuwa na marafiki,lakini mimi sio risk taker enough kuanza urafiki na mtu wa humu hadi kukutana nae

Nina moyo mwepesi sana wa kuumia,jambo dogo linaweza kuniumiza sana

So ni heri kubaki tusiojulikana ili kustay away from trouble na kuumia
 
Hembu agiza togwa hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…