Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Post M-alone upo??
Punga mkono moyo wangu upate amani,,Usije tu kuwa ulikuwepo huko Bukoba

👋👋 Hio kazi changamoto za hapa na pale zipo nyingi... Now I'm not in the industry,
One day nilikuwa naruka na tulikuwa tumechelewa na kila mtu alikuwa na shauku ya kuondoka, nikatizama cockipit pressure ipo good, nikacheki fuel ipo good kucheki engine gauges haipo sawa, haikuwa kwenye RPM ile inapaswa kumbuka hapo nipo kwenye runway, nikazidi kukimbia runway nilikuwa naona gauges(RPM) zinapanda kwenye level inayotakiwa ikawa inanipa matumaini nikazidi kutembea, taratibu ndege ikaanza kunyanyuka.

Nilikuwa nimevuka v1, nikisema v1 speed pilots wanaelewa ni ile maxmum speed ukiwa kwenye runway ambapo bado unakuwa kwenye uwezo wa ku reject ndege isiendelee kuruka(takeoff) tokana na umbali/urefu wa runway, uki exceed v1 uwezo ni mdogo wa ku reject take off kwa maana hakuna enough runway left ili u stop. Hii ipo kwa sababu kuna issue kama engine failure,blown tires n.k, kwenye take off speeds kuna v1, vr, v2. na kila ndege ina take off speeds zake.

Kichwani kwangu kuna maswali na vita inayoendelea ndani kwa ndani nikiwa kwenye takeoff run, niruke? niache?, hakuna mtu anajua, asee niliamua abort takeoff na nika cancel ile flight, nili cut power chaap ndege ikarudi kwenye runway ikasimama mbele mwishoni mwa runway

Kweli ningeweza kuruka lakini engine haikuwa sawa, kuliko kuja kusema sorry ni bora kuwa safe, kitu kilichonitisha sana sio ku abort takeoff bali ni ile vipi kama ingetokea engine failure wakati wa ku climb, ingekuwa ajali mbaya mno, abiria hawakujua lolote. 🙂
 
Back
Top Bottom