Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Hii itaonekana kama utani lakini inagusia jambo la muhimu sana. Kuna mambo hayapaswi kuwekwa kwenye CV hasa kama unaomba kazi ya maana kwenye mashirika ya kimataifa; na kwingineko. Na kinachowaponza wengi ni hizi barua za hawa wanaoitwa referees/recommenders. Huwa wanaandika mambo ya ajabu sana.

Kuna miongozo mingi mtandaoni kuhusu CV ya maana inavyopaswa kuonekana. Ni vyema kufuata miongozo hiyo kama unaomba kazi kwenye NGO na mashirika mengine yenye mawanda mapana.

NB: Siku hizi CV wala haziangaliwi na watu hasa katika hatua za mwanzo mwanzo. Zinaangaliwa na kompyuta. Na kama habari za msingi hazipo juu kwa margins zinazotakiwa CV yako haitavuka hata ule mchujo wa kwanza maana software haiwezi hata kudaka zile personal info tu za mwanzo mwanzo...
 
IMG_20220630_161007_429.jpg
 
Asante sana , kwa maelezo muhimu kama haya, naamini yatatusaidia vijana wengi. Ni kweli mie huwa napokea cv nyingi kwenye email ya boss wangu, huwa naitumia mie. Ni huruma sana, kuna cv huwezi rudi isoma mala mbili mbili, ukiitazama tu unaachana nayo
 
Ni tatizo.

Niliwahi kukaa kwenye selection committee kwenye NGO fulani iliyokuwa inatoa scholarships za kusoma Masters kwa vijana kutoka Africa na Middle East. Mimi nilipangiwa kushughulikia waombaji kutoka East na Central Africa. Mbona nilichoka

Kuna tofauti kubwa sana ya kiweledi kuhusu mambo ya msingi kati yetu hata na Wakenya tu hapa. CV zao zimeandikwa kitaalamu sana na zinajitahidi kujibu maswali yote ambayo mtu unaweza kuwa nayo. Ni professional CVs.

Sisi unakuta mtu amekazana na hobbies kibao eti swimming, listening to gospel and rap music and fishing wakati mambo ya msingi hajayagusia.

Njoo kwenye recommendation letters sasa. I know the applicant and s/he will do well in her/his studies mtu kamaliza. Unachukua recommendation letter ya Mkenya ina kurasa tatu profesa anaelezea jinsi anavyomfahamu applicant kwenye personal na professional level...

Mambo haya yanaweza kuonekana kama madogo lakini ndiyo yanatukwamisha sana Wabongo kiasi kwamba ukienda duniani huko kwenye mavyuo makuu na mashirika mengi utakuta wamerundikana Wakenya tu na Wanaijeria.

Huwa inaniuma sana!
 
Back
Top Bottom