Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,582
- 1,105,383
Dah!Achana na mambo ya BMI ndugu yangu. Fanya mazoezi kwa afya, furahia maisha na uwapendao, epuka stress za rejareja Kisha kula ugali wa kutosha.
Utaambiwa usile hichi, acha hiki, lala masaa matatu, usivute sana pumzi, sijui kunywa supu ya maboga, wote tunakufa na miaka Ile Ile, hakuna anaeishi miaka 300. Hata hivyo unataka uende na mapafu safi huko tuendako unatarajia kuyauza?
Uzito wangu nachezea 65kg -70kg Kwa urefu wa 76 cm.
Kula ugali ng'wana wane.
Nimecheka sana aisee kwa sababu ulichokisema ndiyo MO yangu hapa duniani. Huwa natumia karibu kila kitu kwa wastani isipokuwa tu nilivyojaribu vikanishinda na ambavyo najua kuwa vina madhara ya moja kwa moja.
Na huyu daktari siyo mara yangu ya kwanza kugombana naye. Yaani ukienda hata umeongeza kilo 5 tu unalooo utasemwa mpaka ukome. Sema tu nimetoka naye mbali sana na ameshaniokoa na scares kibao vinginevyo ningekuwa nshatemana naye.
Binafsi huwa nafanya vimazoezi na kula vizuri ninapoweza ili kuwa na afya na kujikinga na magonjwa haya yanayoweza kukwepwa kwa kubadili mfumo wa maisha mf. presha na kisukari. Mambo ya BMI na hizi vurugu zingine ni za huyu MD. Shwaini zake halafu!
Nitauzingatia ushauri wako na tarehe 30 June nitaleta mrejesho.
Wabeja (Asante)








