Sekta ya Afya nchini kunufaika na msaada wa Dola za Marekani Milioni 600 (takriban Tsh. Trilioni 1.4) kutoka Global Fund

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
835
1,000
Serikali ya Tanzania itanufaika na msaada wa dola za Marekani milioni 600 zitakazotolewa na Taasisi ya Global Fund mwezi Januari mwakani kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na maradhi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria katika kipindi cha miaka mitatu.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkuu wa Mfuko huo Barani Afrika Bw. Linden Morrison, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dodoma.

pix 8.JPG

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Global Fund Barani Afrika Bw. Linden Morrison


Amesema kuwa fedha hizo sawa na takriban shilingi za Tanzania trilioni 1.4 zitatumika kuimarisha afya kwa kupambana na magonjwa ya Ukimwi, Kikufua Kikuu na Malaria ambapo vifaa tiba na vitendanishi mbalimbali vitanunuliwa kupitia msaada huo katika kipindi cha miaka mitatu (2021-2023).

Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka 15 ambacho taasisi yake imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania, Mfuko wake tayari umetoa msaada wa dola za Marekani bilioni 2 kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya hususan katika mapambano dhidi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Taasisi hiyo ya Kimataifa ya Global Fund kwa mchango mkubwa iliyoipatia Tanzania katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo hasa malaria, ugonjwa unaoongoza kusababisha vifo vya watanzania wengi.

Dkt. Mpango aliahidi kwamba fedha hizo zitatumika kikamilifu na kama ilivyokusudiwa ili zilete matokeo chanya kwa kuwafikia walengwa nchini kote.

‘‘Nimefurahi kwa sababu nina matumaini kuwa tumepata nguvu ya kupambana na magonjwa haya makubwa, ili Watanzania wawe na afya njema na waweze kujenga uchumi wa nchi yao’’ Alisema Mhe. Mpango.

Aidha Dkt. Mpango alisema katika kikao hicho wamejadili namna ya kuboresha zaidi ushirikiano uliopo kati ya pande hizo mbili ikiwemo kuangalia namna ya kutoa msamaha wa kodi kwenye vifaa yakiwemo magari ya kubebea wagonjwa na dawa zinazoingizwa nchini na Taasisi hiyo kwa ajili ya mradi huo.

“Aidha, Ili kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Taasisi ya Global Fund, nchi itahakikisha inakuwa na ushiriki mpana katika Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko huo ili sauti ya nchi iweze kusikika zaidi” aliongeza Dkt. Mpango

Kuhusu ubadhirifu wa zaidi ya dola za Marekani 400,000 zinazodaiwa kufujwa na baadhi ya Watendaji wa Serikali wanaotekeleza mradi huo hapa nchini, Dkt. Mpango ameuahidi Mfuko huo kwamba Serikali itachunguza na kuwachukulia hatua kali watu wote waliohusika na vitendo hivyo.
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,964
2,000
Kiukweli hizi Taasisi za Marekani zinavyotusaidia, mfano US Aid, Global Fund, Millennium Challenge Account, etc, wanatusaidia sana, ni kama malaika mkombozi fulani mfano watu wangejua gharama za vidonge vya ARV, Kifua Kikuu na Ukoma, na kujua ni Marekani wanatupa bure na sisi tunazigawa bure, hivyo nchi kama Marekani, Uingereza, EU wanapotusaidia, tunawaita ni nchi wahisani au nchi wafadhili ila pale wanapotukosoa kwa madudu yetu, then wanageka ni mabeberu!. Hivyo mtu mmoja yule yule akifanya mema ni malaika, akifanya mabaya ni shetani!.
P
 

masozist

JF-Expert Member
Nov 19, 2019
321
500
Kiukweli hizi Taasisi za Marekani zinavyotusaidia, mfano US Aid, Global Fund, Millennium Challenge Account, etc, wanatusaidia sana, ni kama malaika mkombozi fulani mfano watu wangejua gharama za vidonge vya ARV, Kifua Kikuu na Ukoma, na kujua ni Marekani wanatupa bure na sisi tunazigawa bure, ila Marekani inapotukosoa kwa madudu yetu, then wanageka ni mabeberu!.
P
Haha haha nakuelewa sana njaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
447
1,000
Zitto siyo WB, hizo hoja zenu wapuuzi wa UVCCM ungezipeleka huko WB. una Naomba Pesa kama wafadhili,alafu waki kunyima mna waita mabeberu. wakati vigezo vya hiyoo misaada huyu Mungu mtu wenu ana vipuuza
Utasomesha wazazi wewe acha ujinga
 

Fibanochi

JF-Expert Member
Jun 28, 2018
352
1,000
Kwa hiyo kwa msaada huu tunakubaliana tuwaiteje Sasa " mabeberu" au " wahisani"?.
After all , hili siyo jipya, global fund wamekuwa kwa muda Sasa wakitusadia kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya hususani kwenye sekta ya afya kwa kutoa bure dawa za ARV, bila wao pengine tungepoteza nguvu kazi kubwa Sana Kama taifa..Naamini ktk Kila mtu Alie humu ana mtu wake wa karibu anaenufaika na dawa hzi au pengine hata yeye binafsi.

Wamarekani wataendelea kuwa wakubwa zetu siku zote, hakuna namna tunaweza kuwakwepa. Huu msaada utaetolewa kikamkati zaidi, nafikiri ni reminder tu kwetu kuwa "fanyieni kazi tuliyowaambia or else".

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
447
1,000
Kiukweli hizi Taasisi za Marekani zinavyotusaidia, mfano US Aid, Global Fund, Millennium Challenge Account, etc, wanatusaidia sana, ni kama malaika mkombozi fulani mfano watu wangejua gharama za vidonge vya ARV, Kifua Kikuu na Ukoma, na kujua ni Marekani wanatupa bure na sisi tunazigawa bure, ila Marekani inapotukosoa kwa madudu yetu, then wanageka ni mabeberu!.
P
Si wazungu wote ni Mabeberu wanaotusaidia lazima tuwaite wafadhili lkn wakija kinyonyaji kama Accacia wale ni Mabeberu mbona mnaogopa sn Unyonyaji wa Accacia haujahalalishwa na Nchi lakini kikundi cha wanyonyaji ndio Mabeberu yaani IMPERIALISTS
 

Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
583
500
Zito atawaandikiaa tena barua hao maana alivyo na roho mbaya huyu Mrundi
Marekani anasaidia masikini kwenye masuala ya afya hata kama anapinga naye. Juzi tu Iran naye kapewa upenyo wa kuagiza dawa na vifaa tiba. Usishangae huu mfuko wa Global Fund ambao ni wa hao hao marekani kusaidia masikini kama Tanzania kwenye masuala ya afya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom