Serikali imetenga jumla ya Tsh: bilioni 899.4 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kuajiri na kuwajengea uwezo Wahudumu wa Afya

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Na. WAF - Dar Es - Salaam

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetenga jumla ya Tsh: bilioni 899.4 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kuajiri na kuwajengea uwezo jumla ya Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wapatao 137,294 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

Hayo amesema Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdori Mpango leo Januari 31, 2024 kwenye Uzinduzi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii uliofanyika katika kituo cha Mkutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam.

“Utekelezaji wa Mpango huo utafanyika katika kipindi cha Miaka Mitano kwa awamu ambapo mwaka wa kwanza 2023-2024 zaidi ya wahudumu elfu 28,000 watafikiwa na baadaye wastani wa wahudumu elfu 27,324 kila mwaka kwa kipindi cha miaka Minne mfululizo kuanzia mwaka 2024-2025 hadi 2027-2028.” Amesema Makamu wa Rais Dkt. Mpango

Aidha, Dkt. Philip Mpango amezielekeza Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Mamlaka nyingine zinazohusika kwa kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi madhubuti wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ili uweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Dkt. Mpango amewasihi viongozi wote wanaohusika katika ngazi zote kuhakikisha zoezi la kuwachagua wahudumu hao wa Afya ngazi ya jamii linafanyika kwa kufuata vigezo na taratibu zilizowekwa ili kupata wahudumu wenye sifa stahiki watakaotekeleza majukumu hayo na kuwataka watakaopewa jukumu la kutekeleza mpango huo, kujiepusha na vitendo vya upendeleo, rushwa au ukiukwaji wa taratibu.

“Wahudumu wa Afya mtakaopewa dhamana ya kutekeleza jukumu hili zingatieni weledi na kujituma pamoja na kutoa rai kwa jamii kuupokea mpango huo na kuthamini huduma za wahudumu wa aAya ngazi ya Jamii kwa kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kulinda na kuboresha Afya katika jamii.” Amesisitiza Makamu wa Rais Dkt. Mpango
 
Hizo Ajira mnatoa lini maana vijana wamechoka na story za ajira….
Na hawa wahudumu wa afya ngazi ya Jamii watakuwa na sifa gani?
 
Kwenda kuchezea hela tu za walipa kodi wapi duniani wahudumu wa afya wanaokotwa barabarani.

Hao wahudumu wa afya ngazi ya jamii wanaenda kuwa na majukumu gani hadi usaili ufanyike bila ya vigezo vya qualifications.

Kuna watu kwenye huduma ya afya kweli wanaweza kufanya kazi bila ya national syllabus na knowledge kutolewa na taasisi ya elimu.

Habari tu inakwambia HR huko wizarani washatengeneza policy inayoenda kuwa disaster sijui wametumia gani ku-justify utaratibu wa sandakalawe kupata hao watu.

It’s rocket science kubaini TNMC awakushirikishwa kwenye ku-design hiyo training wala recruitment process. Ndio maana watu wamekuja na utaratibu ambao sio tu unaenda tengeneza wahudumu below par, bali ghasia kwenye recruitment process.

Watch this space
 
Back
Top Bottom