BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,118
Tanzania na Global Fund zimesaini mikataba minne ya misaada yenye thamani ya dola za Marekani milioni 606.9 sawa na zaidi ya shilingi trilioni 1.4 kwa ajili ya kupambana na maradhi ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Malaria na uimarishaji wa mifumo ya afya nchini.
Mikataba hiyo imesainiwa Jijini Dodoma kati ya Waziri wa Fedha, Dkt. @mwigulunchemba1 na Mkuu wa Global Fund- Afrika, Linden Morrison.
Waziri Nchemba amesema msaada kutoka Global Fund umepangwa kutekelezwa kwa miaka mitatu ambapo mpaka sasa Tanzania imepokea misaada kwa vipindi vinne ambavyo ni Julai 2012 – Desemba 2014, Julai 2015 – Desemba 2017, Januari 2018 – Desemba 2022 na Januari 2021 -Desemba 2023.
"Miradi inayotekelezwa kupitia msaada wa Global Fund kwa kipindi cha kuanzia Januari 2024 hadi Desemba 2026 itatekelezwa na Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha inaendelea kuwa Mpokeaji Mkuu wa Sekta ya Umma na Management and Development for Health (MDH) ni Mpokeaji Mkuu wa pili kwa Sekta Binafsi," amesema Waziri Nchemba.
WIZARA YA FEDHA