SEKESEKE: Wapangaji Majengo ya CDA Dodoma wanatimuliwa muda huu

SEKESEKE: Wapangaji Majengo ya CDA Dodoma wanatimuliwa muda huu

Haaahaaaaa! uwiii, hivi wewe huwa unafikiria nini?! jamani kweli hii picha na matukio yanayoendelea sasa, napendekeza hii picha ndio ingetumika kwenye maofisi ya serikali, hii ndio iwekwe fremu ikae ukutani. Dodoma wameonja nguvu ya mkuu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Walifukuza wanafunzi UDOM, kumbe walijua serikali inataka kwenda pale wakatafuta jinsi ya kusaidia chemba za maji taka kutopasuka hovyo kama Dar, wakatimua watoto wa watu sasa zoezi la kuunguza watu linaendelea kwa style tofauti tofauti kazi ipo.
 
Dah! Huu ni uonevu wa hali ya juu. Kisa kukurupuka kwa mtu mkurupukaji kunaleta matatizo makubwa sana kwa wakazi wa Dodoma.
 
JPM anakazi bado ya kutumbua majipu yanayo nyanyasa wananchi, kama hawakupewa taarifa kabla.
 
Hawa jamaa walishapewa notisi muda mrefu wakaenda mahakamani lakini mwenye nyumba (CDA) aling'ang'ania kuwatoa kwenye hizo nyumba. Ila sababu ya kuwatoa haifahamimiki ni ipi.

Duh kumbe, ni enzi zile walizoea kupiga muda now basi. Haya wasilalamike
 
Hv walikuwa wanafukuzwa kweli mbona nimeona kama walikuwa Wanasomeshwa namba vile? Wacha waisome nambaeeeeeeee!
 
Hizo nyumba mbona chakavu Sana..ndio watahamia huko wageni??
kuna rafiki yangu alikuwa anaishi pale kwenye hayo maghorofa,tangu zamani sana wana mgogoro na CDA wanaambiwa wahame hawataki,CDA wanaita vikao hawahudhurii.jamaa aliniambia CDA wamesema wanataka kuyarepair hayo majengo maana yamechakaa sana so wakatakiwa wahame.hii kesi ina miaka so sioni kama kuna mtu kaonewa hapo.tatzo kupenda dezo maana kodi bei rahisi nyumba vyumba cjui vtatu sebule choo bafu kila familia/mpangaji mmoja,pale hata watu waliojenga hawakuachia vyumba,wengine wakitaka kuondoka wanampangisha mtu kwa chajuu.ukitaka kujua mtu kaonewa au laah,ielewe kwanza situation nzima.naona hapa watu wanalalamika tuu.
 
Si uungwana kabisa
kwa mimi ninayeishi maeneo karibu na maghorofa hayo,naoana hawajaonewa maana walishaambiwa wahame sijui tangu mwaka gani,kila siku vikao mara kesi ipo mahakamani.kila nikipita mitaa ile mida ya jioni nasikia mtu akiongea na kipaza sauti kuwa wakazi wa pale wanatakiwa wahame.hawataki na nasikia kwa kipindi kirefu sana huku kesi ipo mahakamani walikwa hawalipi kodi,tatizo ni kupenda dezo,ona sasa adha waliyoipata wametimuliwa harakaharaka.
 
Hivi tunaelekea wapi ..kila hatua inayochukuliwa na serikali watu wanaingiza siasa. Hata kwa hili!! Mwenye nyumba amekupa notice uondoke kwenye nyumba yake kwasababu anataka kufanya ukarabati mkubwa .. eti ukakataa ..akijakukutoa kwakutumia nguvu unalalamika.. tuache siasa kwa mambo kama haya..
mkuu watu wanapenda kulaumu bila kujua undani wa tatzo,wamuulize mtu yeyote anayejua wakazi wa pale walipewa hati ya kuondoka tangu mwaka gani atawaambia.oooh namba inasomwa,kweli inasomwa ila kwa swala hili hakuna aliyeonewa.mwenye nyumba kakupa notice uhame akarabat mjengo hutaki,nyumba yako?
 
Back
Top Bottom